Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Huyo labda dishi limecheza, juju au ni mlevi mbwa..
Lazima sehemu moja wapo yumo.

Maisha ni mipango na ukikosea kupanga unapanga kufail.
 
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

View attachment 1125671

View attachment 1125673

View attachment 1125675
Mshaurini Ajira Portal kuna nafasi za kazi yake ajaribu huko.
 
Hapa bongo kama unataka kufa mapema nenda kasome mikozi migumigu kama hiyo. Nawashauri vijana wenzangu njoo tusome course kulingana na mazingira yetu, mfano kama kwenu wanalima komaa na PCB, CBG au CBA afu nenda zako sua maliza kaboreshe kilimo Chenu. Tuache kuriri kuwa kusoma mikozi migumu et ndo kutoboa utazeeka bure. Ila samahani kwa kutumia lugha ngumu najua nimewakera sana
 
Huyo jamaa kama kweli kasoma chuo hakuelimika
Anashindwa hata kulima alizeti eka mbili akapata japo mtaji?
Chadema mchukueni huyo awe mgombea badala ya lissu
 
  • Thanks
Reactions: T11
Yeye alipata ajira, akaacha kisa wadogo zake

Mbona haiingii akilini?

Kwanini asiwahamishie mjini aliko na ajira?

Kwanini aliacha ualimu pia?


Watu wa Chadema kuna mambo wanaandika kwa malengo ya kisiasa
 
Unarudi nyumbani kuja kuangaliana na wadogo zako? Jamaa huyu mjinga!
Pengine ana tatizo

Mwandishi kakwepesha mambo kwa sababu anazojua


Ndio maana ukisoma anajishtukia eti hana tatizo la akili
 
it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Sasa ufumbuzi gani ndugu si umeona amejishikiza kubeba mizigo?

Mambo mengine ni kunyamaza na kumshukuru Mungu kwa ulichojaliwa.
 
SIJAJUA LENGO LA HUU UZI. NIMESOMA MARA MBILI MBILI LAKINI BADO SIJAJUA MAANA YA HUU KUWEPO HUU UZI HUMU. DIWANI KAENDA KUMUONA. KAENDA KUMUONA ILI IWEJE? HII HABARI UMEKUTA WAPI?
HUYO DIWANI HANA AKILI. HUU NI ZAIDI YA UDHALILISHAJI MAANA KAMA MTU HUTAKI KUMSAIDIA NI BORA UKAMUACHA NA MAISHA YAKE NA SIYO KUMUWEKA KWENYE MEDIA ILI WAPATE SIFA.
HUU UZI NIMEUSOMA ILA SIJAFURAHISHWA NAO KABISA. DADA YANGU UMEFANYA JAMBO JEMA LAKINI UMEFANYA UDHALILISHAJI PAMOJA NA HUYO DIWANI. MTU ANAHANGAIKA NA MAISHA YAKE AMEKONDEANA. WEWE UNARUSHA HUMU SIJUI UPATE LIKE AU NDIYO UJULIKANE ZAIDI?
KIUFUPI
WEWE, DIWANI NA HAO WALIOCHAPISHA HIYO HABARI WAMEFANYA TUKIO LA UDHALILISHAJI. KAMA MTU HUWEZI KUMSAIDIA ACHANA NAYE NA SIYO KWENDA KAMERA UPATE SIFA.
Chadema hao wanaokoteza vichaa vijijini waonekane wako na wanyonge
 
it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Sidhani kuwa issue ni kukosa ajira
1. Aliajiriwa shirika la mawasikiano na kuamua kurudi kijijini kusaidia wadogo zake. Je asingewasaidia akiwa kwenye hiyo ajira?
2. Alikuwa Mwl Senge secondary japo kujitolea .Akaacha. huyu asaidiwe kisaikolojia sio tu kumpa pesa au mtaji kuna hitaji zaidi ya hilo. Nalo ni matibabu ya akili
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom