Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
35,478
Points
2,000
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
35,478 2,000
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

1560352748124-jpeg.1125671


1560352770973-jpeg.1125673


1560352792846-jpeg.1125675
 
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,506
Points
2,000
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,506 2,000
Viatu vya Samaki nakuheshimu saana
 
Ahmad Abdurahman

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
773
Points
1,000
Ahmad Abdurahman

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
773 1,000
Jana tulikutana kwenye thread moja, nkakutana na maneno yako tu mafupi nanukuu;
"Life fucks us thus why nobody dies virgin"

nakumbuka mbali sanaaaa. Maisha yangu yalikua kama huyo jamaa 99%.

Mungu amtangulie milango ifunguke.
 
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,506
Points
2,000
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,506 2,000
Daaaa nimesoma huku machozi yakinivizia.
Hasa nikikumbuka mwaka 2012 nilimaliza chuo July na Desemba mwaka huohuo nikapata ajira mpaka leo maisha yanasonga.
Hee mwenyezi mungu waangalie viumbe wako hawa wanaohangaika mtaani na vyeti vyao vizuri.
Asante kwa mchango ni matumaini yangu namba umeiona utafanya yako mkuu
 
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,506
Points
2,000
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,506 2,000
dah inaumiza sana aisee,,,
hivi serikali haiwezi ku fund tech startup hata za watu watano watano,ili kusaidia vijana
AU hicho sio kipaumbele kwao,,,,,halafu unakuta limtu kama musiba wanalifadhili pumbavu zao.............
Bob, tupunguze hasira. Fanya kumsadia ndugu yetu hapo juu
 
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,506
Points
2,000
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,506 2,000
Jana tulikutana kwenye thread moja, nkakutana na maneno yako tu mafupi nanukuu;
"Life fucks us thus why nobody dies virgin"

nakumbuka mbali sanaaaa. Maisha yangu yalikua kama huyo jamaa 99%.

Mungu amtangulie milango ifunguke.
Aisee sijui kama unajua ni kiasi gani naumia kuona watu wanaumia kiasi hiki! Huyu jamaa simjui but niko tayari kuuza kuku wangu nimtumie hata buku!!
Babu yako naelewa kila kitu. Kuzeeka kote huku nshakwepa mishale mingi
 
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,506
Points
2,000
Robot la Matope

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,506 2,000
Naamini JF hatushindwi kitu! Maxence Melo mkurugenzi wetu mpendwa naomba utuongoze tuonyeshe nguvu ya JF
 
Ahmad Abdurahman

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
773
Points
1,000
Ahmad Abdurahman

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
773 1,000
Aisee sijui kama unajua ni kiasi gani naumia kuona watu wanaumia kiasi hiki! Huyu jamaa simjui but niko tayari kuuza kuku wangu nimtumie hata buku!!
Babu yako naelewa kila kitu. Kuzeeka kote huku nshakwepa mishale mingi
Mkuu najua sana hizo shida, zinaumiza, zinakatisha tamaa,...unadharaulika, unakejeliwa, unatukwana, unadhihakiwa, unanyanyaswa kwa maneno. Sitaki kukumbuka. Nampa pole. Dunia ni duara.
 

Forum statistics

Threads 1,304,903
Members 501,587
Posts 31,531,248
Top