Jeffery Samson Mkuki: Msomi wa Chuo Kikuu anayehangaika kijijini bila ajira

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,043
2,000
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

1125671

1125673

1125675
 
Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
3,735
2,000
Ubarikiwe kwa kuibua hili.....
Geofrey Samson Mkuki (katikati) ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, katika fani ya uhandisi wa Mawasiliano (BSc. in Telecommunication Engineering) mwaka 2013. Kidato cha 4 na cha 6 alifaulu vizuri kwa kupata daraja la kwanza (division 1).
_
Lakini anaishi maisha ya ufukara na ukiwa kijijini kwao Mkiwa, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida. Geofrey hana wazazi (baba na mama yake walishafariki). Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia hiyo ya watoto watatu, hivyo anawajibika kuwalea na kuwatunza wadogo zake.

Tangu amalize elimu yake amekua akihangaika kupata kazi maeneo mbalimbali bila mafanikio. Mwaka 2013 aliajiriwa kama kibarua katika kampuni moja ya mawasiliano lakini baada ya mkataba wake kuisha alirudi nyumbani Ikungi. Baadae alipata ajira ya muda shule ya sekondari Chifu Senge kama mwalimu wa Physics na Hesabu. Baadae serikali ilipiga marufuku waalimu wa 'part time' akaamua kurudi kijiji kwao Mkiwa.

Kwa sasa anajishughulisha na vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza-Dar ili aweze kujikimu kimaisha na kuhudumia wadogo zake.

Kiongozi wa Oparesheni ya Chadema, jimbo la Singida Mashariki Francis Garatwa na Diwani wa Kata hiyo John Siuhi wamemtembelea Geofrey nyumbani kwake leo.

Licha ya kujishughulisha na vibarua vya kubeba mizigo, Geofrey ni mtaalam mzuri wa Computer na uhandisi wa mawasiliano, na amekua akisaidia kutengeneza computer za baadhi ya watu kijijini hapo.

Geofrey anatamani kutoka katika lindi la umaskini lililomvaa lakini haoni njia. Geofrey ni mfano halisi wa tatizo la ajira kwa vijana wengi nchini. Wapo vijana wenye elimu nzuri lakini kutokana na changamoto ya ajira wameshindwa kutumia ujuzi wao kulisaidia taifa na kujisaidia wao wenyewe.

Kama umeguswa na maisha ya Geofrey kwa namna yoyote na unadhani unayo nafasi ya kumsaidia (either kumtafutia kazi au mtaji wa biashara) unaweza kupiga Simu yake ya mkononi kwa nambari 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Credit: Francis M. Garatwa View attachment 1125842
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,639
2,000
it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Hiyo kawaida ki bongo bongo.. watu wengine tulishachuja zaidi ya huyo lakini tukasema aluta continua na sahiv mambo fresh tu.. akomae asingojee huruma ya watu
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,639
2,000
Kwema Mzee baba. Shuta shuta mwendo wa ngiri, hakuna kulala, ukipepesa kidogo wanakomba mboga na vyombo wanakuachia uoshe.

Si unaona vijana wanavyopigika za ugoko huko?
Amina mzee baba... maisha yalivobadilika hivi usipojiongeza lazima ule za ugoko.. inatakiwa kijana usikae kiboyaboya ukisikia forex chomeka ndani, ukiwa betting chomeka ndani ukiliwa sepa hamia pengine mpaka utusue
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
13,601
2,000
it is a puzzle indeed. But, hii sio mara ya kwanza kusikia hizi habari za wahitimu kukosa ajira,tuhangaike kutafuta ufumbuzi na sio kuignore magnitude ya hili tatizo..
Am I missing something here?

....Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa...
 
Mti Mtu

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,470
2,000
sasa hapo mm cjaelewa kabisa... hii post inamaanisha nn?? yaani mtu mpaka alifikia hatua ya kuajiriwa akaacha... sasa aloshindwa kuwachukua hao watoto ili aishi nao?? na ukomo wa kuitwa yatima ni miaka 18... ukizidisha hapo ww siyo yatima!! sasa huyu jamaa hapaswi hata saidiwa kabisa... labda kama zimemluka akili zake
 
aldeo

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
954
1,000
JEOFREY SAMSON MKUKI KIJANA "MSOMI" WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ANAYEHANGAIKA KIJIJINI BILA AJIRA.

Alihitimu Elimu ya Chuo Kikuu (University Of Dodoma) Mwaka 2013 kisha akaelekea zake Dar Es Salaam kujitafutia Riziki na baadae akaamua kurudi Kijijini kwao alikozaliwa. Kule UDOM, Jeofrey alisomea (BSc.Telecommunications Engineering) na Vyeti vyake vyote kuanzia Kidato cha Nne hadi Chuo Kikuu anavyo huku Kijijini.

Kijana mwenzetu Jeofrey Samson Mkuki ni Mkazi wa Kitongoji cha Imiga, Kijiji cha Mkiwa, Kata ya Mkiwa, Wilaya ya Ikungi huko Mkoani Singida. Jeofrey Mkuki ni Yatima asiye na Wazazi wake wote wawili maana walishatangulia mbele za haki.

Wakati nafika Eneo anakoishi Jeofrey Mkuki huko Mkoani Singida, niliambatana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi anayeonekana Pichani upande wa kulia. Huko Kijijini, Jeofrey anaishi na Wadogo zake wawili ambao wanamtegemea na anajishughulisha na Vibarua vidogo vidogo ikiwemo kupakia Mizigo kwenye Magari na kuuza Mkaa karibu na Barabara Kuu ya Mwanza to Dar Es Salaam.

Kijana Jeofrey Mkuki ni Mtu mwenye Akili zake timamu na kwa mujibu wa Majirani zake na Viongozi wa Serikali wa Eneo anakoishi akiwemo Mheshimiwa Diwani wa Kata hiyo niliyeambata naye, wanadai hajawahi kupatwa na tatizo lolote la Kiafya, ingawa ukiutazama muonekano wake unaweza usiamini kama ni Kijana mwenye Elimu ya kiwango cha juu kiasi hiki.

Kwa mujibu wa maelezo yake yeye mwenyewe, Jeofrey anasema, "niliamua kurudi huku Kijijini kwa sababu, wadogo zangu hawa bado ni wadogo na kama unavyoona Wazazi wote hawapo, iliniuma sana nikaamua nirudi huku. Huko Mijini nilipata Ajira kwenye Mashirika ya Mambo ya Mawasiliano na nilikuwa nazunguka Mikoani, lakini kutokana na hii familia unayoiona, ndio hivyo tena Mheshimiwa, lakini natamani Siku moja niwe tofauti na hivi niliyake. Alieleza Mkuki.

Kijana Jeofrey Mkuki aliwahi kufundisha kama Mwalimu wa kujitolea wa Masomo ya Sayansi kama vile Basic Mathematics na Physics katika Shule ya Sekondari Senge maarufu kama Chifu-Senge iliyopo Singida Mjini Mkoani Singida. Nilipomuuliza kwa nini asiendelee kufundisha, Jeofrey alisema ni Maisha tu yamemvurugia mambo yake na akafikia hatua hii ingawa bado ana wazo la aina hiyo.

Aidha, Jeofrey Mkuki pia ni Mtaalam mzuri wa Computer na wakati nafika Kijijini kwao anakoishi huko Mkoani Singida, nimemkuta akiwa na Computer yake aina ya Laptop HP anayotumia kwa ajili ya Shughuli zake za binafsi.

Kwa Mawasiliano zaidi na Jeofrey Mkuki wa Singida unaweza kupiga Simu yake ya Mkononi 0746440462 au Email: mkukijs@gmail.com

Au unaweza kuwasiliana na Diwani wa Kata yake ya Mkiwa Mhe.John Siuhi 0745865904.

Francis M. Garatwa,
Kiongozi wa Oparesheni ya Chama,
Jimbo la Singida Mashariki.
Ikungi, Singida - Tanzania.
12 June, 2019.

View attachment 1125671

View attachment 1125673

View attachment 1125675

Hapa Kuna kitu kidogo naomba tuelewane na kukubaliana tunaamini kuanzia darasa la Kwanza mpaka umefika chuo na kuhitimu NI mengi amekutana nayo pili ametembea sehemu nyingi na ameona mengi.

Hivi mtu mwenye degree kichwan anarud kijijini anakuwa Hana tofauti na mtu ambae hakwenda hata darasa Moja HV huyu elimu yake inamsaidia nn? Alisoma kujibu mtihan au alisoma kuongeza maarifa kichwani,. Huyu jamaa kashindwa hata kujiposition Kama mtu aliesoma na kufanya hata umiddleman kwa wenye navyo ili ajitengenezee kesho yake?

Degree inashindwa kumuumizisha kichwa awe wakala wa mabasi au mfugaji mwenyetija hata Iwekuku au mbuzi?

Fursa ya dengu alizeti na mazao mengine ameshindwa kuitumikisha degree yake imsaidie?

Jambo jema amerudi kijijini manaake karudisha mpira kwa kipa kwasie ambao tusharudishaga mpira kwa kipa huwa tunakaza kweli ili isiwembwai tukaonekana niaje pili Hali yake ya kifamilia ilimfanya awe mpambanaji KWASABABU alikuwa Hana Cha kupoteza Bali tofauti ya elimu ilibidi itumike kutatua changamoto zake na familia yao na I we fursa kwa Kijiji kizima.

Hapa Kama usomi ndo huu naomba watu tujitafakari vizuri.
 
Top Bottom