JEETU agonga mwamba! ktk EPA na Bank M | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JEETU agonga mwamba! ktk EPA na Bank M

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, May 7, 2008.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi Bank M ni ya nani vile?
  NEEEEWZZZZ today!!!
  OMBI la mfanyabiashara Jeetu Patel anayetuhumiwa kuwa kinara wa ufisadi katika kuchota mabilioni kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutaka hisa zake alizowekeza katika Benki M aziuze kwa raia wa Falme za Kiarabu, halijapata kibali kutoka Benki Kuu (BoT).

  Badala yake, BoT imesema ombi hilo bado liko kwenye mchakato wa
  kutathmini wanahisa wa benki hiyo, kitendo kinachoelezwa kuwa kinahusisha wadau mbalimbali.

  Februari mwaka huu, Jeetu kupitia Benki M alipeleka maombi BoT ya kutaka kuuza hisa hizo kwa Tarek Al Asharam baada ya kuenguliwa katika umiliki wa benki hiyo.

  Benki M ilimwengua Jeetu katika umiliki wa benki hiyo kutokana na kukumbwa na tuhuma mbalimbali za kughushi na kujipatia mabilioni ya fedha kwa njia ya uongo. Kwa sasa, anachunguzwa na vyombo vya dola baada ya kutajwa kushiriki katika kuchota mabilioni ya EPA.

  Kurugenzi ya usimamizi wa mabenki katika BoT imesema mchakato wa kutathmini wanahisa katika benki hiyo unawahusisha wadau mbalimbali na itachukua muda mrefu kukubali au kukataa maombi hayo.

  Jeetu kupitia kwa makampuni yake ya Noble Azania Investments Limited (NAIL) anamiliki asilimia 20 ya hisa za benki hiyo zenye thamani ya Sh bilioni 1.3, wanahisa wengine kwenye benki hiyo ni Negus Holdings Ltd (Sh bilioni 1.3b), Africarriers Ltd (Sh bilioni 1.3), Equity and Allied Limited (Sh bilioni 1.3), Kumar (Sh milioni 650) na Nair (Sh milioni 650).

  “Tunapenda kukujulisha kwamba hisa za Benki M bado hazijabadilika na zinamilikiwa na wanahisa wale wale,” ilisema BoT katika barua yake iliyosainiwa na A. Kobelo na A. Ukhotya ambao ni maofisa katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki.

  Kurugenzi hiyo ilisema hizo zinazomilikiwa na mfanyabiashara huyo ambaye jina lake kamili ni Jayantkumar Chandubai Patel, hazijauzwa wala kuhamishwa kwa mmiliki ye yote.

  Benki M ilipeleka maombi ya kumwengua Jeetu kutokana na matakwa ya kisheria chini ya sheria za benki ya mwaka 2006 na kanuni za taasisi za fedha ya mwaka 1997. Taratibu za BoT zinaeleza kuwa maombi ya kuhamisha hisa ni lazima yafanyiwe tathmini kufuatana na vifungu na kanuni zilizo ndani ya sheria zilizotajwa hapa juu.

  Kwa mujibu wa sheria ya benki ya mwaka jana, leseni ya kufungua na kuendesha benki haiwezi kutolewa kwa mtu mwenye historia au rekodi ya makosa ya jinai, kufilisika, kukosa uaminifu au hujuma kwa Serikali.

  Watu wengi wamekuwa wanaishutumu BoT kwa kutoa kibali cha kuanzishwa kwa Benki M wakati mmoja wa wanahisa wake ambaye ni Jeetu akiwa na rekodi ya kushiriki kwenye makosa ya jinai.

  Kifungu cha 12 cha sheria za benki na taasisi za fedha kinasema mtu anakoma kuwa mkurugenzi na mmiliki wa benki iwapo atabainika kuwa amefilisika au atakapotiwa hatiani kwa makosa ya kughushi au ya kutokuwa mwaminifu. Katika kifungu hicho pia inaeelezwa kuwa mtu anakoma kuwa mkurugenzi wa benki iwapo ataondolewa na bodi ya benki husika.

  Jeetu kupitia kampuni tisa anatuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha katika BoT. Kampuni hizo ni Bencom International Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment. Kampuni zake nyingine zinazotajwa kutumika kwenye ufisadi huo ni Maltan Mining Company, Ndovu Soaps Ltd na Navy cut Tobacco Tanzania Ltd.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Nimrod Mkono, Februari mwaka huu alinukuliwa na gazeti hili akithibitisha kuwa tayari benki hiyo imeshamwengua Jeatu katika umiliki na ukurugenzi wa benki hiyo. “Sio mkurugenzi tena…tumeona hatuwezi kuendelea kuwa na mtu ambaye ana kashfa nyingi kiasi hicho,” Mkono aliliambia gazeti hili.

  Kutokana na kushiriki katika uchotaji wa mabilioni ya EPA, Jeatu ni mmoja wa watu wanaochunguzwa na Timu maalumu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika. Wengine katika timu hiyo ni Wakuu wa Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  source: Habari leo
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bank M ndiyo ipi ndugu yetu? tuweke wazi, unajua haya mabenki yamekuwa mengi hadi wengi wetu tuliyopo mikoani hatuyajui,
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Majizi tuu haya na kuna kila sababu ya kuwatangazia watanzani wakatae kuwa wanachama wa benki kama hizi zilizoanzishwa kwa fedha za wizi .
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Kama una akiba yako huko Bank M, basi iondowe haraka sana maana inaweza ikafilisika na wewe kupoteza akiba yako yote.
   
 5. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwita
  Sidhani kama imetandaa hadi mikoani kwa hivi karibuni lakini Bank M iko jijini Dar.Hiyo herufi M nadhani inasimama badala ya jina Mkono au Mkapa kwa kuwa wamehusishwa kuhusu umiliki wake.
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bado nafuatilia kujua uhusiano wa Kikwete na huyu Jiitu Patel! Inaonekana uhusiano wao ni mkubwa kuliko nilivyofikiria mwanzoni.
   
 7. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Filauni....Hawa majambawazi wanatuibia na with confidence wanafungua na benki humu humu??? kweli tumelala wa-tz.Hivi huyu mkono kelele zoooote ni msafi kiasi gani jamani?? Nadhani hata kule BOT ana kaharufu ka uvundo fulani.. hebu tukumbushane wapiganaji...Simuelewi hata kidogo kama Patel katolewa ukurugenzi na ushareholder kwa sababu ya kashfa nadhani naye pia alitakiwa kuwemo....Nadani hata hii benki inatakiwa kuwekwa chini ya uangalizi angalau kujua na huo mtaji shareholders walipata vipi??? Si ndio mambo ya vijisenti maelezo ya 1.2Ml wala hayaeleweki.
   
 8. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ahsante kuuliza, angalia majibu waliyoanza kukupa wakuu maana watu mikoani wakiambiwa msiwape kura hawa jamaa maana wao na ufisadi damudamu, watu hawaelewi
   
 9. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  fuatilia pls tupate data za kumkoma nyani!!!
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  MWK, ndio maana jamaa anakuwa mzito kuwashughulikia mafisadi maana na yake wanayajua pia. Akimgusa mtu tu basi na ufisadi wake utaanikwa hadharani hapo ndipo kutatokea mtikisiko ambao hatujawaji kuuona Tanzania
   
 12. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2008
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,960
  Likes Received: 20,299
  Trophy Points: 280
  Hivi ni Mkapa au Mkono, mbona wote kama wale wale linapokuja suala la kashfa.


  Muda ukifika mwenye mapengo atatafuna 'bisi'
   
 13. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni wote wawili, ndio maana benki ikaitwa M ati!!
  soma habari hii ya mwaka jana
  REVEALED: Mkapa family owns Bank M building  THISDAY REPORTER
  Dar es Salaam

  IT has now been revealed that the building housing the registered office of an upcoming new financial institution, Bank M (Tanzania) Limited, in Dar es Salaam is owned by former president Benjamin Mkapa and his wife Mrs Anna Mkapa.

  The two-storeyed office building (pictured) is located at Number 8 Ocean Road, right adjacent to the official residence of the former president and first lady (inset photos) in the city’s affluent Sea View area.

  Our investigations show that the couple bought the property, with certificate of title number 6809, from the Tanzania Building Works in 2002.

  At the time, Mr Mkapa was still the sitting president of the United Republic of Tanzania, while Mama Anna served as the country’s First Lady.

  President Benjamin William Mkapa and First Lady Anna Mkapa served in the highest office in the land from 1995 to 2005, when he concluded his second and final presidential term.

  The inconspicuous building in a quiet neighbourhood of Upanga is now listed as the registered office of Bank M (Tanzania) Limited, a new bank in the pipeline which is understood to have some rather big-name members of the local business community as shareholders through their respective companies.

  The bank, with an initial share capital of 6.5bn/-, is in the final stages of being launched after a registration process that started in February this year.

  In the meantime, there are few signs of its pending arrival, with only a hardly visible signpost on the front boundary wall of the building where it is housed, and now revealed to be owned by the Mkapa family.

  The signpost has the simple letter ’M’ printed on an austere logo.

  According to our investigations, registered owners of the bank are Jayant Kumar Patel, alias Jeetu Patel, of Noble Azania Investments Limited; Vimal Mehta of Negus Holdings Limited; and Fidha Rashid, a prominent real estate developer and car dealer with Africarriers Limited.

  Nimrod Mkono of the respected Dar es Salaam law firm Mkono & Co. Advocates, is also listed as one of the main shareholders of the bank through one of his companies, Equity & Allied Limited.
  There are also two listed minority shareholders in the name of Sanjeev Kumar, a local banker, and Bhaskaran Nair, described as a business executive.

  Records show that by February this year, the shareholding structure of the bank as officially filed was as follows: Negus Holdings Ltd (1.3bn/-), Noble Azania Investments Ltd (1.3bn/-), Africarriers Ltd (1.3bn/-), Equity and Allied Limited (1.3bn/-), Mr Kumar (650m/-) and Mr Nair (650m/-).

  When contacted by THISDAY and asked to give more details about the bank’s shareholding structure, registration and licensing status, and other details, shareholder Jeetu Patel declined comment.

  Instead, the Noble Azania Investments Limited representative referred our queries to Mkono, who has so far not been available for comment.

  Apart from his status as a top local lawyer and representative of Equity and Allied Limited company in the new bank’s shareholding structure, Mkono is also the current member of parliament for the Musoma Rural Constituency, on a CCM ticket.

  Efforts by THISDAY to contact the governor of the Bank of Tanzania (BoT), Dr Daudi Ballali, to confirm whether or not ’Bank M’ has been or will be issued with a formal banking licence, have also proved unsuccessful so far.

  But our sources in the country’s banking sector have confirmed that the process of recruiting key staff for the new bank has been quietly proceeding, apparently in preparation of its imminent formal launch.
   
 14. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Bank m ina madudu mengi sana...nimefanya kazi pale...ukiacha ufisadi pia kuna unyanyasaji mkubwa...wapo wanaolipwa vizuri sana na wapo wanaolipwa hovyo kabisa...a lot z going on pale....endeleeni kufatilia mtayajua tu.
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii habari sio ya ukweli maana hisa za Jeetu Patel ni 1.3 Billioni tu????????
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwani Sanjeev Kumar ni local banker oooops!!!!
   
 17. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  JF Data Bank ni zaidi ya CIA na KGB...
   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2013
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
 19. Baraka Roman

  Baraka Roman JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2013
  Joined: Feb 16, 2013
  Messages: 694
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bank M nayo ni mzigo

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 20. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2013
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hii benk pesa yote ni ya watanzania akuna ata senti moja ya halali.Hii nchi tunahitaji mapinduzi kwa kweli
   
Loading...