tHe NapSTer of Tz
Member
- Mar 30, 2007
- 86
- 1
Toa mifano kidogo (mingi siyo vibaya) ili kujenga kesi yako au kile unachobase swali lako. Na kwa vile wamo humu nina uhakika hawatasita kukujibu.
The real question is "Kuna waandishi wa habari Tanzania?"
Waandishi wa habari wa Tanzania wengi wanafanya kazi vizuri kabisa, ukiondoa wahuni wachache wanaotumiwa na mafisadi kuandika kile ambacho mafisadi wanataka kiandikwe au kisiandikwe katika magazeti yaTanzania.
Magazeti ndiyo yamekuwa mstari wa mbele kufichua uozo mbali mbali wa hali ya juu uliokuwa ukifanywa na viongozi mafisadi wangazi za juu akiwemo fisadi Mkapa. Wamekuwa mstari wa mbele katika kuibua uozo wa mbali mbali ndani ya BoT kama vile EPA, fisadi mkono kulipwa bilioni 8 ambazo hakustahili, fisadi Mzindakaya kupatiwa mkopo na BoT pamoja na kwamba BoT hawatoi mikopo kama hiyo bali benk za biashara, gharama kubwa kupita kiasi za ujenzi wa Twin Towers, kuajiriwa kwa watoto wa 'viongozi ambao hawana quaifications zozote za kuajiriwa BoT na mengi mengineyo yakiwemo ya mkataba wa Buzwagi, Richmond n.k.
Hata mabalozi mbali mbali wa nchi za wafadhili zikiwemo US, UK, Holland, Germany, Denmark n.k. wamewasifia waandishi wa habari wa Tanzania kwa kufichua maovu mengi ndani ya CCM na SIRI KALI. Hata wanahabari wa CNN na BBC mashirika makubwa ya habari duniani huwa wanafanya makosa mara nyingi na kuomba samahani.
Hivyo tusiwakatishe tamaa waandishi wa habari wa Tanzania ambao wengi wao wanafanya kazi yao vizuri sana ukiondoa wahuni wachache.
WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Musa Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau wasomi wazalendo na wacha Mungu mnaoheshimika, bado wananchi wanawalilia.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/8/2/makala1.php
Nafahamu kabisa Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Dk. Hassan naye ni mswahilina mzuri na anayeheshimika ukiachia nafasi kubwa ya usomi aliyonayo, amebeba dhamana kubwa ya kuiongoza bodi inayojali na kuzingatia kwa dhati haki za binadamu.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/8/2/makala1.php
Mimi bado napata shaka katika hayo ya kufichuwa maovu!... Wanafanya wao wynyewe au wanalipwa na wakubwa, na kambiwa nani wamharibie jina!... na kuongeza uongo kidogo!.....
Maana ukiamuliwa kuondesha sehemu! waandishi wa habari ndio weapon nzuri....
Habari wanazoandika ni SADIKI ukipenda!!!
7. Absalom Kibanda – The editor of Tanzania Daima is really an attack pit-bull that Freeman Mbowe unleashes once in a while. (Deodatus Balile is a pitbull for Rostam Aziz). The problem with Kibanda is the "Mbeya problem". He hasn't gotten over the fact that Mwandosya lost to JK fairly and squarely in 2005.
Lakini siku za nyuma kuna mwana JF alitoa analysis juu ya waandishi Tanzania na alimzungumzia mhariri wa TANZANIA DAIMA au tuseme gazeti la FREEMAN MBOWE kwa kusema hivi:
source: https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13378&highlight=Stan+Katabalo
need i say more?
kituko cha TANZANIA DAIMA wikiendi hii:
Ok inawezekana ikawa mara moja ni bahati mbaya...lakini huyu mwandishi wa gazeti la Mbowe akakisha likaendelea kuonyesha ujinga na uvivu wa kufikiri na kufanya research kwa kudai hivi:
UKWELI WA NANI MWENYEKITI WA BODI YA NSSF HUU HAPA:
http://www.nssf.or.tz/board_of_trustees.php
Jamani tuache ushabiki halafu tuangalie hili gazeti FREEMAN MBOWE LINAVYOOAJIRI makanjanja
hivi huyu kweli ndio Dr MUSSA HASSAN au kajibadilisha?
Mrs. Blandina Nyoni
Board Chairperson
National Social Security Fund
Dar es salaam
hivi wanashindwa kuingia JAMII FORUMS kutafuta referencing kama KUBENEA na MWANAHALISI?
What a shame!
http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/9/7/habari35.phpTanzania Daima, Alhamisi, 7 septemba 2006
Nyoni Mwenyekiti Bodi NSSF
Na Jamal Zuberi, MAELEZO-Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Blandina Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Ladislaus Komba, Nyoni anachukua nafasi ya Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga Juma.
Taarifa hiyo imeeleza pia Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana amewateua wajumbe 11 wapya kwenye bodi hiyo.
Wajumbe hao ni Nicholaus Mbwanji (ATE), Ally Mwinyimvua (Benki Kuu) na Nicholas Kingazi (CRDB) ambao wanawakilisha waajiri, wakati Nestory Ngula (TUCTA), Boniface Nkakatisi (TUICO) na Adelgunda Mgaya (RAAWU) wanawakilisha Vyama Huru vya Wafanyakazi.
Wengine walioteuliwa kuiwakilisha serikali ni Dk. Mussa Assad (Kitivo cha Biashara na Uongozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Ekingo Ekingo (Wizara ya Maliasili na Utali), Ezekiel Maige na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
Bodi hiyo mpya itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Septemba mosi mwaka huu.
GT
watakwambia wewe ni mnafiki na huwatakii mema ktk mafanikio ya kisiasa na kihabari,kwani wewe hujui kua Tanzania daima ndilo gazeti pekee ambalo halitumiwi na RA na siku zote linaandika ukweli mtupu.
Mkamap na mwenzio GT, munajikaanga kwa mafuta yenu. Hiyo mada ya huo waraka wa kina Mkapa na wenzake, ulijadiliwa kwa kina murudi na kuisoma vyema. Tukirudi kwenye mada husika kuhusu waandishi wa Tanzania, nadhani mukiwa munatenda haki, munaweza kurudi na kuangalia habari zote zilizoandikwa na Majira na Rai kwa wiki mbili zilizopita, mutaona ni aibu tupu. Angalia Majira habari walizoandika kuhusu Wangwe, utaona siku ya Press Conf ya Kina Lipumba waliandika stori na baada ya siku mbili wakarudia habari ile ile tena kwa uzito mkubwa, hapo sijui hao ndio wanaokusudiwa kuandika habari kwa kutumwa, au munazungumzia kina nani? Angalia Majira wanaandika wakimnukuu Paul Kyara, bila kuwaambia wasomaji Kyara ni nani na alitokea wapi kabla ya kuanzisha chama chake na kauli zote za Kyra zina mrengo gani!! Huo ndio mfano hai wa uchafu katika fani ya habari. Vinginevyo urudi nyuma na mifano hai ya jinsi, Sumaye, MWandosya, Malecela, Kitine, Kigoda, Dk. Salim na wengine wengi walivyoathiriwa vibaya na matumizi mabaya ya vyombo vya habari na walioshiriki kutunukiwa japo sasa wameonekana udhaifu wao na mifano ipo wazi. Vinginevyo musilete mjadala wa kujadili HEWA toeni mifano watu wajadili na kuona PUMBA na MCHELE ni upi
JF,
Watanzania wengi wanapoamka asubuhi kwenda ofisini, kabla hawajaingia ofsini wanatupa macho yao kwenye vichwa vya habari vya magezeti!!!
Tukiangalia kwa kina tutaona kwamba waandishi wa habari wa Tanzania wananguvu kubwa sana. Yaani mpaka hatari! Waandishi wa habari wamekuwa wakimanipulate habari nyingi na tukizipindua wanavyotaka wao!..
Watanzania wanasoma sana magazeti. Na infact wanaamini sana magazeti!
Waandishi wetu wakobiased ile mbaya!...... Hawa hawa waandishi wanaotuandikia habari za viongozi mafisadi wao wenyewe wengi wao ni mafisadi na wanafanya kazi na hao (hidden) expert fisadis!...
Waandishi ama mass media ni chombo muhimu kwenye jamii!!! Jee tunakubali kutawaliwa na waandishi waongo,mafisadi na wanafki waliokosa uzelendo kazi kuchochea fitna na uhasama baina yetu?