MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Kwa mtu anayezijua vizuri siasa za nchi hii lazima atakuwa anajua kuwa bila ''mkono'' wa CCM, Zitto Kabwe asingekuwa hapa alipo kisiasa!
Ukweli huu ndio ambao ulimfanya Zitto Kabwe kutoaminika ndani ya chama chake cha mwanzo (CHADEMA) mpaka chama kikaamua kumfukuza uanachama!
Malezi yake ya kisiasa kuanzia chuo kikuu yamefanywa na mashine/mitambo ya CCM mpaka kufikia hapa alipo.
Hata pale viongozi wa juu wa CHADEMA walipoamua kumfukuza uanachama, ni mitambo/mashine za CCM zilizohakikisha anabakia katika uwanja wa siasa ambapo alisaidiwa kwa haraka kuanzisha chama cha ACT-Wazalendo!
Kwa wale wazoefu hapa Jamiiforums nadhani watakumbuka hii mada ambayo ilileta michango mirefu na mizito kuhusu ACT-Wazalendo;
Ni CCM ambayo imekuwa ikimuachia Jimbo huko Kigoma kuanzia mwaka 2005 kiasi kwamba hata kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu, wagombea wa Urais wa CCM walikuwa hawafiki katika Jimbo analogombea Zitto kumpigia kampeni mgombea wa CCM. Hii ilikuwa inafanyika ili kumpa Zitto fursa ya ushindi!
Zitto kwa kujua au kutojua, baada ya kukaa bungeni kwa miaka 15, nadhani akadhani amekuwa ''indispensable'' na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha! Hii haina tofauti na mtoto kuanza kujipima ''ubavu'' na baba yake!
Uungwaji mkono kutoka kwa ''wapambe'' kwenye mitandao ya kijamii ulimfanya akadhani anaweza hata kuung'ata ''mkono'' unaomlisha na maisha yakaendelea kama kawaida!
Link>>>Zitto Kabwe: Niko mbioni kuanza mazungumzo na Jumuiya za Kimataifa ili kupambana na utawala wa Rais Magufuli
Wenye ''mkono'' wakaanza kumuonya kuhusu tabia yake ambayo ilianza kuvuka mipaka ya kisiasa!
Ieleweke kuwa Zitto hana tofauti na Nape Nnauye na January Makamba ambao pia wamefika hapo walipo kisiasa kutokana na mashine/mitambo ya CCM. Nape na Makamba Jr pia walianza kuung'ata mkono unaowalisha baada ya kudhani wamekuwa ''indispensable'' lakini kabla mambo hayajawaharibikia zaidi waliomba msamaha haraka sana! Kilichowatokea kila mwenye uelewa wa siasa anajua!
Zitto Kabwe alishindwa kuelewa kuwa CCM huwa haitishwi na ''kinyago ilichokichoga''! CCM is ruthlessness in the game of power politics! CCM ikiona unaanza kuhatarisha nguvu zake za kisiasa inakupa onyo au inakushughulikia!
Mwezi wa Januari 2020, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alifanya ziara katika Mkoa wa Kigoma na kusema wamedhamilia kulichukua Jimbo la Kigoma Mjini katika uchaguzi Mkuu 2020.
Yaliyotokea katika Jimbo la Kigoma Mjini baada ya uchaguzi huu kila anayefuatilia siasa nchini anajua!
Kilichobaki kwa sasa ni Zitto kujisalimisha na kuomba msamaha kama walivyofanya Nape na Makamba Jr ili arudi kwenye ''system'' ama kama atazidi kupiga kelele na kuleta siasa kali kuna uwezekano wenye chama chao wakakihitaji na anaweza kujikuta anarudi CHADEMA baada ya ACT-Wazalendo kuondoka mikononi mwake!
Zitto Kabwe anatakiwa atambue kuwa sikio haliwezi kuzidi kichwa!

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)
Dr Kitila Mkumbo anakula matapishi yake ACT kuvuruga juhudi za katiba ya Wananchi CCM yapumua, ujio wa ACTkupunguza nguvu za upinzani Wanajamvi, Siku za karibuni chama kipya cha ACT(Alliance for Change and Transparency) kimepata usajili wa kudumu. ACT inaungana na mlolongo wa vyama vya...
www.jamiiforums.com