Je, Zitto Kabwe alijisahau na kuanza kuung'ata mkono unaomlisha?

Jibu ni ndiyo Mimi niliwahi kuandika humu kwamba Kati ya wanasiasa wa nchi hii Zitto ni mchumia tumbo namba moja. Kwamba alikuwa anapiga makelele kwa sababu mianya ya kupiga hela aliyozoea wakati wa serikali ya Kikwete ilikuwa imezibwa.
 
Bila kuiba kura hakuna CCM iliyoko madarakani.
Kwa hiyo badala ya kuisifu CCM iangaze kwa ukweli wake hakisi kuwa iko haoo ilipo kwa uporaji wa maamuzi ya wananchi!
Wizi wa kura ni maneno ambayo tumeyasikia tokea mfumo wa vyama vingi nchini uanze.

Hawa wanaibiwa kura tokea mwaka 1995 lakini kila uchaguzi hawakosi. Wapo tu!
 
Story yako sio mpya . Hii story ipo tokea mfumo wa vyama vingi uanzishwe lakini kinachoshangaza wanaodai kuibiwa kura kila uchaguzi wapo!
Mleta mada, CCM sio chama cha siasa, uchaguzi (uchafuzi) wa mwaka huu wapinzani walipambana na Tiss, polisi, jeshi, wakurugenzi, wakuu wa wilaya/mikoa

Ccm kama ccm kwenye uwanja huru ni wepesi kama karatasi
 
Kama kweli CCM wanajiona wana ubavu, ilikuaje wanaiba kura kijinga tena mchana kweupe? Nadhani CCM hawana nguvu yeyote, zito amewachapa asubuhi tu na wala hawajashinda.
na huo ndio ubavu wenyewe. Baada ya vita watu huangalia ushindi na si jinsi gani ushindi ulipatikana. Tukubali tukatae CCM ndio imeshika dola na tukiendelea kuichekea itatawala mpaka vitukuu vyetu.
Sasa hivi muda wa kupimishana mabavu umepita maana CCM itashinda tu kwa njia zake zizijuazo zenyewe.
Wa kuitoa CCM madarakani sio wanasiasa kama kina Zitto maana wote wana bei yao, wakilipwa wanaufyata.
Atakaekuja kuitoa CCM madarakani ni mlalahoi wa chini kabisa asiekuwa na jina wala cheo, maana huyo ndio muhanga hasa wa siasa mbovu za CCM zikisaidiwa na hao wanaojiita wapinzani.
 
Mwami Zitto ni one man show, hata wadhifa wake kwenye chama ni KIONGOZI WA CHAMA, ni zaidi ya Mwenyekiti wa Chama.
Lakini kubwa ya yote Zitto hana upande,na hiyo ndio siri ya mafanikio yake.
Ndio maana aliungana na Lissu wa Chadema kususia nafasi ya viti maalum vya Chadema akisisitiza Chadema ni sister party, lakini akaja kukubali ACT kuingia serikali ya Mseto Zanzibar.
Huyo Mwami haoni aibu kubadirisha mtizamo au msimamo wake kwa kipindi kifupi,yaliyomkuta Membe yanafurahisha.Membe hakutegemea Zitto atamkana mchana kweupe kuwa sio mgombea wa ACT,bali Lissu wa Chadema tena katikati ya kampeni.
Zitto ni survival wa siasa za Bongo kwa kipindi kirefu mbeleni.
 
Nilisimamia uchaguzi huu, ki ukweli ninajua kila kitu juu ya kilichotokea na juu ya wizi ulivyofanyika, hakukuwa na uchaguzi, ilikuwa ni ujinga tu.
Uliiba wewe na sio CCM,
Huwezi shindana na mtu hana miguu kisha umwibie,
Chadema ni nyumbu ambao ukiwaonyesha mto wa maji wanatumbukia woye bila kujua urefu wa mto na mamba kiasi gani wamo.

Kama mmeibiwa basi hata nyie mngefikisha hata milioni 8 hapo ungeweza kulalama, uzidiwe milioni 10 kisha useme umeibiwa?
Nyumbu mna shida sana.
 
Back
Top Bottom