Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 37,107
- 55,524
- Thread starter
- #21
1. Nikupe mfano. Kuna watu wengi tu wali-mine bitcoin siku za mwanzoni mwanzoni bila kujua kitakachotokea na baadae wakatajirika.
2. Richard Branson alipokuwa kijana alitaka kuanzisha jarida la wanafunzi. Akaanzisha jarida lililoitwa Student ili wanafunzi waweze kuandika masuala yao. Ili kupata fedha za kulichapisha alianza kuuza rekodi za muziki kwa bei nafuu kwa kutumia posta. Lakini (KWA BAHATI)wakati huo kulitokea mgomo wa posta nchini Uingereza na wateja wakaanza kuja moja kwa moja ofisini kwake kuchukua rekodi walizoagiza. Tukio hilo la bahati lilimfanya atambue kwamba anaweza kufungua duka la muziki, na hapo ndipo alipoanzisha biashara iliyokuja kukua baadaye kuwa kampuni kubwa ya Virgin Group
Kwa asilimia fulani nakubaliana na hoja yako, ila cha muhimu, bahati haiwezi kuja kwa mtu asiyejishughulisha au kwa yule ambaye hakuweka mazingira ya kupokea bahati kama itakuwepo. Ule uwezo wa kutengeneza mazingira, ambao wengine hawana huo uwezo, ile ni akili.