Nichukue fursa hii kuwa mtu wakwanza kupokea baraka zako kwani hakika wewe ni mmoja kati ya wale kenda ambao huhupenda kuwaombea wenzao mema.Nawatakia maandalizi mema ya kuianza week mpya na nawaombea wote Mungu awabariki na kuwatia nguvu ktk kulisukuma gurudumu la maendeleo. Muuone wepesi kila muendapo kutimiza majukumu yenu.
Be blessed.
Habari zenu wana MMU ninaamini kabisa wote mko salama . Nina jambo nataka kushare nanyi najua halitakua geni sana kwenu wengi mmekumbana nalo kama si wote . Mmmmh ktk familia zetu nyingi huwa kuna mchanganyiko wa watotot na watu wazima . Je nyie mmewahi kumsikia huyu mtoto ambae huwa anatajwa na watoto karibu wote hasa wanapokua wamekosea ??? Ukikuta uharibifu wowote ndani ya nyumba ukiwauliza watoto basi watakutajia jina la huyo mtoto na ukijaribu kumtafuta kamwe hautampata na nimesema siku nikimpata huyo mtoto atanitambua kwa kweli . Kiukweli mtoto huyu anasumbua sana. Unajua Mtoto huyo anaitwa nani , anaitwa "SIJUI".
Nawatakia maandalizi mema ya kuianza week mpya na nawaombea wote Mungu awabariki na kuwatia nguvu ktk kulisukuma gurudumu la maendeleo. Muuone wepesi kila muendapo kutimiza majukumu yenu.
Be blessed.
Yaani nikadhani bongeeee! La story
hahahahahahahahahahaha umenichekesha mbaya zaidi ukiuliza tu anapotea hata ukijaribu kufuatilia alivaa nguo ya rangi gani utapewa jibu lile lile sijuiDah!!! kumbe hata wewe unamfahamu huyu, huyu mtu nilipata kumjua mara ya kwanza nilipoenda kumtembelea rafiki yangu mmoja hivi, huyu jamaa siku hiyo tumekaa kwao mzee wake akarudi ghafla kutoka kazini na kusema kuna document zake alizisahau juu ya kabati, ila akawa hazioni na anashida nazo kweli. Sasa kila anaemuuliza mle ndani anasema sijui......sasa mzee akawa analalamika, anawaambia watoto wake "Nikiwauliza vitu vyangu, huyu mtu anaeitwa sijui huyu sitaki kabisa kumsikia na sijui anaingilia wapi, maana akiingia tu hakuna kinachopatikana humu ndani, halafu kila mtu anamtaja yeye tu"
Hahahahah......Sio siri umenikumbusha mbali sana, inabidi nifanye juu chini nimtafute huyu rafiki yangu popote pale alipo nimkumbushe hii kitu
Nimekupata mkuu itabidi tubadili majina ya watoto kwa wale waliowaita watoto wao majina hayo. Mimi shida yangu kwanini mtoto huyu kila nyumba utamkuta na huwa yupo kwa ajili ya kuharibu tu. Wewe ukiona kitu kipo ndivyo sivyo ukiuliza utaambiwa sijui tena nillidhani anapatikana kwenye familia za kiafrica tu kumbe hata kwa wazungu yupo wao wanamwita I DON'T KNOW. Aaaaah kazi kweli kweli.Ablessed ndio mm pia nimewahi kuliona hili jina na kumbe hajapost hata post ila ni kujaza tu uMember labda uniambiwe sikujua ndio majina mnayowapa watoto yanasababisha muwapoteze hebu wapen majina mazuri, ila ukiingia JF hutayakosa majina hayo ndio ujue jamii Forum ni zaidi ya ujuavyo
Sijui
Junior Member
Add as Friend Send Private Message Add to Ignore List Find latest posts Find latest started threads View Conversations Likes Received (0) Likes Given (0)
Join Date 10th October 2010 Last Activity 10th October 2010 17:31 Avatar