Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Mimi Ni mzaliwa wa kwanza Vita ninavyopigana kwenye Hilo life MUNGU tu anajua.

Naamini nitashinda soon maana mimi akili ninayo sio kilaza

Sio mnywaji

sio mlevi

Sijawahi vuta hata kipisi Cha sigara

Ila shida yangu iko pale Kati patamu

Kwakweli MUNGU nipiganie niachane na hij kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Ni mzaliwa wa kwanza Vita ninavyopigana kwenye Hilo life MUNGU tu anajua.

Naamini nitashinda soon maana mimi akili ninayo sio kilaza

Sio mnywaji

sio mlevi

Sijawahi vuta hata kipisi Cha sigara

Ila shida yangu iko pale Kati patamu

Kwakweli MUNGU nipiganie niachane na hij kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti pale kati patamu 😂😂😂😂
Jikite kwenye muvi na muziki kama mimi bro unaweza kuyashinda. Si unajua if you doubt your power..you power your doubt.
Kikubwa ni kuweka nia ya dhati
 
Asante kwa kunikumbusha hili jambo. Am totally touched by each and very point of your thread. Juzi tu mama kanikumbusha "Mwanangu kumbuka wewe ni lango katika familia, ukipigwa wewe wenzio wote nyuma huku watatetereka"
Sasa ni muda wa kubadirika na kuchukua maamuzi for once and for all
I love you Jesus
 
Kuwa 'mtoto wa kwanza'...

Ukiwa mtoto wa kwanza, na unajua hili ni nini katika maisha -- nadhani katika huu uzi unaweza 'kuviruka vistori stori' vyake... Mimi kama mtu pia ni 'mtoto wa kwanza'.

Ukweli hasa, si lazima mtoto wa kwanza awe 'maalum sana'; kujitambua na kujielewa kunatosha kumgeuza yeyote kutoka kwenye hali moja hadi ingine yakufikia... Kuna suala la kukua na kukuzwa na jamii; pia kukomaa na kujichagulia... Japo kuna mambo ya kiutamaduni katika kuthamini nafasi ya 'uzaliwa wa kwanza' -- katika jamii za kiliberali, hili la 'kiutamaduni' linapoteza mashiko... Tunalea watoto wetu kwa kadri tunavyojitahidi kuwasoma na kuwatia wepesi katika njia na mapito yao...

Watoto wetu wanazaliwa na uwezo na tunu tofauti, kuzingatia haya kwa mfano -- suala la 'mkubwa kwa mdogo' tunamalizana nalo kwa kujitahidi kuwajengea 'kuthaminiana na kujaliana'... Mtoto wa kati anaweza kufungua njia hata mwenzake wa kwanza kulingana na fursa na mawezekano ya kidunia, hasa ya leo, ikiwa yeye 'nyota' yake ni ya kutangulia... Mtoto wa kwanza akitunza kuwa mwaminifu na muadilifu, anaweza kuwa kiungo cha ndugu wote na si lazima yeye awe tajiri wa hali na mali.

Mtoto wa kwanza anaweza asiwe na 'nyota' ya kisomo... Wadogo zake wakawa na kisomo, Je, elimu si ni 'kiongoza' --ikiwa si ni 'ufunguo' wa 'maisha'? Mtoto mwenye kisomo cha kutosha anaweza kuwa 'mshauri' na 'mwongoza' mzuri, haijalishi yeye ni wa kwanza, wa pili ama wa mwisho.... Ndivyo basi tuseme, si kuwa elimu ni 'ufunguo wa maisha' bali 'ufunguo wa maisha' upo katika dhamira ama tuiite ;nia' ya mtu kuwa ni mwenye kupenda kujifunza na kuelimika... Tunalo la muhimu kuwalingania na kuwahimiza watoto wetu -- hawa kupenda kujifunza na kuelimika kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na wenzao... Sambamba na hili ni kujitahidi kuwaambukiza hawa 'moyo wa rehema', 'akili' na 'hekima'... Hekima ni kitu bora sana maishani kwa kuwa hii haipimiki ukubwa ama udogo ;na basi hailinganishwi na 'akili nyingi ama kidogo'. Hekima ni uwezo wa kuyabayanishwa 'unalolijua' na 'usilolijua' pasipo kujikwaa na ukomo wa upeo wako kwa wakati.... Mwenyehekima ana furaha kwa machache anayoyajua na hata mengi asiyoyajua... Anaweza kutangamanisha 'Jua' na 'Mwezi' katika 'taamuli' yake ya nafsi na basi anayochachu kuona -- panapo nafasi kujifunza basi ni jambo la kheri sana; lakini panapo ujinga si ujinga ukiwa wajitambua wewe ni mjinga katika jambo fulani.... Sisi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili tuna msemo--kuuliza si ujinga... Hili ni sehemu ya kuakisi umuhimu wa hekima katika mtu anayeutambua ujinga wake na kuona si suala la unyonge kwa 'kuhukumiwa' na mwingine kuwa ni 'mjinga'.

Labda tunakosa kuelewa ilivyobora kuhusu, kuongoza, kujiongoza, kuwajibika, kuwa na umakini na kujituma maishani... Mtu yeyote aliyemakini na mwenye kujituma katika mambo ya msingi na muhimu katika maisha anaweza kuwa kiongozi... Katika Ulimwengu wa leo, ongezeko la maarifa, elimu na ujuzi unakadirisha fursa sawa kwa watu wote katika kuamua mustakabali wa maisha yao na kujichagulia. Hayati Stephen Covey, katika kitabu chake cha 'The 8th Habit' ananukuu moja muhimu sana kuzingatia hapa. Yeye anasema Kitabu chake hicho 'kiwafikie wote' -- Wale wote "Wakuu" miongoni mwetu wenye moyo wa upole na kujipiga konde , wenye kuonesha kimfano kwa jinsi gani Uongozi ni chaguo, si madaraka...

"To the Humble, courageous, "great ' ones among us who exemplify how leadership is a choice, not a position" -- Stephen Covey, The 8th Habit

Na nimlete 'Shangazi', tupate kujifunza namna gani kuzaliwa katika 'familia bora' siyo lazima iwe 'tija' ama 'nongwa' (tuseme kuzaliwa wa kwanza ama wa mwisho vilevile); bidii, nidhamu, kujituma na msimamo vitakupeleka kokote --vikwazo isiwe sababu.



Hmmm
 
Asante kwa kunikumbusha hili jambo. Am totally touched by each and very point of your thread. Juzi tu mama kanikumbusha "Mwanangu kumbuka wewe ni lango katika familia, ukipigwa wewe wenzio wote nyuma huku watatetereka"
Sasa ni muda wa kubadirika na kuchukua maamuzi for once and for all
I love you Jesus
Ahsante sana kwa compliments mkuu.
Shika sana hayo maneno ya mama..Familia inakuhitaji mno
 
Ahsante sana kwa compliments mkuu.
Shika sana hayo maneno ya mama..Familia inakuhitaji mno
Asante sana mkuu. Sitaki kumwangusha mara hii kama kuongea alishaongea sana swala la pombe na kumrudia Yesu Kristo. Ni muda muafaka now
 
Asante hujaongopa miaka 27 sina hata kitanda nahangaikia walio nyuma na wazee wangu
 
Nitajitahidi kaka japo siyo kazi rahisi maana wakati mwingine unakuta wazee badala ya kukusapoti wanaamua kukuachia ubebe majukumu yao yote
Kaka kuzaliwa wa kwanza na ni mtego..Usifurahie kuambiwa ww ndio mkubwa. Ukubwa ni majukumu.
but God will provide you kama umesimama katika nafasi yako
 
FB_IMG_15973396481075296-1.jpg
 
Back
Top Bottom