Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
33,262
96,421
Mate, Habari.

Kwenye familia zetu kumekua na nadharia inayosema kua watoto ambao ni wa kwanza kuzaliwa hasa watoto wa kiume kwamba hua hawana Akili, ni mapepe,ni watundu na mara nyingi hua hawana mafanikio mazuri kiuchumi (pesa) na kijamii (familia). Ni kweli, Mara nyingi wazaliwa wa kwanza hua (HASA WA KIUME) hua na maisha Vulnarable hasa katika mafanikio ya pesa,familia zao,elimu,tabia nk. Watu husema kwamba eti kwakua mtoto alikua ni wa kwanza kwenye familia hivyo alidekeshwa sana hadi ikapelekea akili yake kudumaa na kua mjinga,wengine husema kwakua ni mwana wa kwanza hivyo mayai na mbegu yalikua hayajakomaa ipasavyo kutoa mtoto mwenye akili,

Wengine huenda mbali zaidi na kusema kwamba watoto wa kwanza akili zao hua hazijatulia kwakua eti wakati wanzaliwa mlango wa uzazi wa mama ulikua haujatanuka hivyo ilipelekea wakati mtoto anatoka tumboni kichwa chake kiligandamizwa na mlango wa uzazi ili kipite hivyo akili ya mtoto nayo ikawa Compressed, Hence ndio maana watoto wa kwanza hua akili zao hazijatulia na hua hawafanikiwa sana maishani kama wadogo zao….WRONG!

Nadharia na dhana hizi zote ni ongo na potof, ni kweli kwenye familia zetu wazaliwa wa kawanza wana matatizo mengi ila mtatizo yao hayasababishwi na chochote nilichoorodhesha hapo juu au chochote unachofikiria wewe. Kuna sababu nyingine kubwa ndio inafanya wazaliwa wa kwanza wawe hivyo mnavyoona walivyo.

GENESISS

Ili tujue sabau kuu ya wazaliwa wa kwanza kua hivyo inabidi turudi nyuma hadi kipindi cha ukombonzi watu kutoka misri, Israel walipokua Sinai Mungu aliongea na Mussa kuhusu wazaliwa wakwanza Hesabu 3: 13.”Kwakua wazaliwa wa kwanza wote ni wangu, katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wote wa kwanza katika nchi ya misri nikajiweka wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israel, wa wanadamu, na wanyama watakua wangu; mimi ndimi BWANA.

Pigo la mwisho la Mungu kwaPharaoh lililofanya hadi wana wa Israel kuruhusiwa kuondoka lilikua pigo la kua kila mzaliwa wa kwanza wa watu wa misri, hivyo basi hapo kwenye kifungo hicho mungu alimwambia Musa kwamba kila mtoto, mnyama,mavuno,mapato ya kwanzakatika taifa la Israel yatakua ni mali ya BWANA yaani wanatolewa kumtumikia BWANA maisha yote kama ni mazao au mifugo wanatolewa kama sadaka ya kuteketezwa. Lakini baadae kidogo Mungu alibadirisha sharia(torati) hiyo, aliwachukua watu wa kabila zima la WALAWI WA KIUME na kuwafanya wao ndio watakaokua wanatoa makuhani na watumishi wa kumtumikia. Alifanya hivyo kwa ajili ya Uaminifu aliouonyesha kuhani wake Aaron (haruni) aliyekua anatoka kabila la Lawi. Lakini akasema kila mzaliwa wa kwanza wa makabila mengine watatakiwa kumnunua kwa kutoa sadaka mbele ya bwana. Aliyasema hayo katika Hesabu 3:41

Ikimbukwe kwamba Yesu Kristo alikua ni mzaliwa wa kwanza mwanaume katika familia ya Bwana Joseph na Bibi Mariamu, hivyo basi kama ilivyo agizwa katika torati ya Mungu nimeeleza hapo juu Yesu alitakiwa akatolewe kwa Bwana hekaluni ila wazazi wake walitoa sadaka hekaluni. Kwakua familia ya Joseph ilikua maskini hivyo haikuweza kumudu kutoa ng’ombe,mbuzi,kondoo walimtolea Mungu sadaka ya NJIWA WAILI Yesu akarudi katika familia, Refer Luka 2:22. Swali ni je kwanini anatakiwa mzaliwa wa kwanza tu sio wa mwisho au wapili? Lakini tukumbuke mada yetu inataka tujue kwanini Wazaliwa wa kwanza kwenye familia ndio hua wanaonekana na matatizo. Tuendelee…

REASONS

Mtoto wa kwanza anapozaliwa anakua Endowed ,Entrusted and Blessed with God katika uongozi na uangalizi wa wa familia na watu wanaomzunguka kiroho na kimwili Mungu kamchagua mzaliwa wa kwanza kwakua yeye ndio future na msimamamizi wa familia husiki baada ya wazazi kuishiwa nguvu au kufariki. Kwa sababu hiyo basi mtoto wa kwanza amezaliwa akiwa na Baraka tele maishani pia kapewa extra knowledge na potential kubwa kuliko watoto wengine ili aweze kuongoza familia yake baada ya wazazi.

Ndio maana Mungu alipowapiga wamisri pigo la mwisho walisalimu amri wakawaachia waisrael maana pale Mungu alikua ameteteresha future ya familia. Pia alitaka wazaliwa wa kwanza kutoka familia ya waisrael kwakua mtoto wa kwanza ukiwa umempata hua unakua na upendo wa ajabu kwake na Mungu anapenda umtolee kile kitu ambacho ukikitoa kinakuuma sana maana yake kina thamani kubwa sana kwako, ndio maana babu yetu mzee Ibrahimu anachukua point kua baba wa imani kwakua aliweza kumtoa mwanae wa pekee aliyempata uzeeeni kabisa Issack .

Kwenye familia zetu wazaliwa wa kwanza hua na akili za kuzaliwa na wana upendo wa hali ya juu kwa wadogo zao, utakuta kaka/dada yupo tayari asisome ili ndugu zake wasome vizuri, hufanya kila kitu kuhakikisha wadogo zao wanasimama vizuri kielimu kwa kuwasomesha na kimaisha kwa kuwapatia mitaji au kuwatafutia connection. Yupo tayari mkewe asiavae nguo kwenye Eid au Xmass ili tu wadogo zake walipiwe ada, ukikuta mzaliwa wa kwanza anayejitambua na kusimamia majukumu yake hufanya kila kitu ili tu ndugu zake wasipitie tabu alizozipita na wazazi wake wakati anazaliwa.

Kwa sacrifice zote hizo wazaliwa wa kwanza wanazozitoa ili familia/ukoo usiaibike kiroho na kimwili ndio maana wao utakuta wana maisha magumu kuliko wadogo zao, bahati mbaya wadogo zao wengine wakishafanikiwa hua hawamjali tena kaka/dada yao baadae wanaanza kumuona kama kaka yao Dishi limeyumba kiasi Fulani au ana gundu la maisha au anapenda kuwapiga mizinga…Wanasahau hapo walipo ni kujitoa kwa kaka/dada yao mkubwa kiroho na kimwili. Lakini wazaliwa wakwanza wanaelewa kwamba wazazi watakufa siku moja,yeye atakufa siku moja,na ndugu zake watakufa siku moja ila Legacy that is what lives on..Familly that’s what matter. Ndio maana wanaendelea kupigania ndugu zao wasiamame kabla yao. Mkubwa ni jalala

Nini kinafanya maisha ya wazaliwa wakwanza kuwa Vulnarable..?


Kuna mwimbaji injili anaimba kwamba “Mungu anafanya kampeni na shetani anafanya kampeni” ni kweli mwisho wa siku kila mmoja anataka apeleke Hesabu zae. Shetani ndio adui mkubwa wa wzaliwa wa kwanza, Shetani unapozaliwa tu anakua ashajua mtoto huyu ana potential gani maishani hivyo mappema sana ataanza kumuwinda mtoto huyo ili amuharibu. Atafanya kila njia kukupata ayafanye maisha yako vibaya. Wakati Mungu anahitaji roho yako ila sio mwili wakoyeye shetani anataka vyote viwili…Anajua kabisa roho yako hawezi kuifikia kwakua ni roh yenye Uungu hivyo atautumia mwili wako zaidi kuua roho yako yenye potential hapa duniani, Akishauharibu mwili roho inabaki haiwezi tena na inakua rahisi kuipeleka roho nje ya kusudi kuu la mungu maana roho inahitaji mwili kutenda. Mwili ukiwavizuri basi roho yako inaweza kutenda yapaswayo kwa uafasaha..lakini pia mwili wako ili utende kazi inahitaji ROHO ILIYO IMARA.

Ukitaka kuharibu Jf inatakiwa umpige Max ukimshinda moderator wote watakimbia, ukitaka kuiangusha treni yote anza kuangusha kichwa chake(injini) ndipo mabehewa nayo yataanguka yote ukianza kungusha mabehewa yaliyo nyuma kichwa cha treni kinaweza kuyaweka sawa mabehewa na safari ikaendelea. Ukitaka nyoka afe mapema usijiahangaishe na mgongo piga kichwa nyoka atakufa haraka. Shetani anajua hizi mbinu zotenaye hua hajiahangaishi na mabehewa hua anaanza Injini. Shetani lengo lake ni kuangusha treni (Familia) kiroho,kiuchumi, na kijamii hivyo anachofanya anaangusha kichwa/injini (mzaliwa wa kwanza) kisha mabehewa (ndugu) huanza kuanguka. Kwanza kabisa anaanzakum distract mtoto toka akiwa mdogo kwa magonjwa mbalimbali, akienda shule anamuwekea vikwazo ili tu asisome inavyotakiwa akaja ku-Retrieve potential yake. Baadae atamletea vikwazo kama kutokujiamini, aibu,kutokuweza kuongea/kujieleza,hofu na uoga. Shetani anaweza hata kutumia hata wazazi,ndugu au majirani ili tu aharibu potential ya mzaliwa wa kwanza coz anajua mtoto akisimama katika njia yake anayotakiwa kuwa basi anaweza iongoza familia kwenye mwangaza mwisho shetani ashindwe kukusanya mapato yake ya kwenda na watu gizani.

Utakuta mtoto wa kwanza ulevi,bangi ,uhuni,ubishoo,kamari,wizi,na mengine mengi mabaya anayo yeye. Unakuta hana future ya maisha yake au akili za shule hana kawa kituko cha familia, hapo ndio watu wanaanzisha ile dhana ya kwamba mzaliwa wa kwanza kwenye familia hua hawana akili aua hawajatulia. Kumbe si kweli! Shetani anakua ameshawin maisha hayo ya mzaliwa kwanza…

Je mzaliwa wa kwanza aiepuke vipi mitego ya shetani..?
  • Malezi stahiki kwa mtoto toka kwa wazai
Hope mwajiuliza kama Mungu kaumba mtot akiwa na potential zote hizo kwanini anarusu shetani aje amuharibu kijana? Jibu ni kwamba huko juu nimeeleza kwamba ili mwili uweze kukwepa mitego ya shetani basi mwili unahitaji roho iliyo imala. Roho inaweza kuulinda mwili usishambuliwe na sheani na mwili ukishashambuliwa basi roho inakua haiana uwezo tena. Eg mwili ukishashambuliwa na pombe,bangi na madawa ya kulevya basi hauwezi kufanya yale roho inayotaka kutenda kama vile Kuaishi katika kusudi kuu la binaadamu kuumbwa. Hivyo basi ili mtoto ambae bado yupo kwenye himaya ya wazazi inabidi apate malezi yanayofaa toka kwa wazazi. Kama wazazi wakiwa na imani iliyo thabiti na wanaelewa mtotot wao anatakiwa awekwe vipi ili aishi maisha bora huko baadae basi wanaweza kumuokoa tokakwenye mikono ya shetani. Wazazi inatakiwa watengeneze misingi imara kwa watoto wao ili baadae waje kuongoza familia kama inavyotakiwa. Nyumba iliyojengwa kwenye msingi imara haiwezi tetereshwa na kimbunga wala tetemeko.
  • Elimu ya kiroho na kimwili itolewe kwa vijana
Waliopewa dhamana ya kuwalea vijana kiroho na kimwili watoe elimu kadri iwezekanavyo, wawafundishe elimu ya utambuzi wajue kusudi la maisha yao na wajue kwanini wapo hapa duniani. Binafsi sijui kama sisi tuliozaliwa miaka hii ya 2000s tunayajua haya masuala ya mzaliwa wa kwanza na kusudi la maisha. Tunajua kuvaa kamatia chini,kuvaa suruali zilizochanika magotini,kupiga picha location na kupata likes Fb ndio kila kitu maishani. Kwa kipindi hiki cha teknolojia na Artificial intelligence inaanza kutumiwa widely na watu wa kawaida sijui kutakua na kizazi cha aina gani kama Elimu ya utambuzi kiroho isipotolewa ipasavyo. Ila yote tutayashindwa kwa imani thabiti maana mtu mdogo anaweza kutoa kivuli kikubwa, mwanga wa tochi dogo au kibatali unaweza kufukuza giza kubwa ndani ya nyumba. Siku zote Giza haiwezi shindana na mwanga..ila yote hayo yatawezekana kutokana na imani yako au Uimara wa roho yako.
  • Deliverance
Sasa kuna wakati wewe mzaliwa wa kwanza unaweza kua umeyafanya mambo mawili niliyoainisha hapo juu au hukuwahi kufanya kabisa maishani mwako na maisha yako yamekua totally miserable huoni pa kutokea maisha yako yamejaa giza ila unatamani kutoka huko ulipo utembee katika njia ya kusudi lako, Fear not God got you coverd!

Mwalimu Mkuu/lecture (Yesu Kristo) ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya BWwana Joseph na Bibi Mariamu, yeye ndio kiongozi wa wazaliwa wa kwanza wote hapa duniani. Anajua kamba Yule mwovu anawatafuta kwa kila hali ili msiweze ku-pursue kusudi lenu, baada ya kumaliza mkataba wake wa kufundisha hapa Darasani(Duniani) akaondoka zake kwenda kuandaa mataji na vyeti (kupaa mbinguni) kwa wote ambao watakaofaulu masomo yake alijua kabisa hawa wanafunzi wangu wanakumbukumbu hafifu na wakiona mwalimu hayupo hawajisomei tena (kuishi katika maagizo ya Kristo) wanabaki kupiga fujo darasani. Hivyo alipofika huko alipoenda alimtuma Tutorial Assistance wake (Roho mtakatifu) aje kutukumbusha na kutufundisha maagizo ya Kristo kwa wale ambao tulikuja muhula ambao kristo hayupo.

Tutorial Assistance alitufundisha kitu kipya kwa sisi tulioingia muhula mpya mwalimu mkuu akiwa hayupo, Alitufundisha kitu kinaitwa deliverance kwa Kiswahili rahisi ni kupokelewa Upya. Wewe mzaliwa wa kwanza Ukishafika ile sehemu tunaita the point of no Return maisha yako yamejaa taabu na mahangaiko Yesu kristo kupitia roho mtakatifu anatoa huduma hiyo ya kuwapokea upya wale wote ambao wamepote maana yeye ni mchungaji mwema kondoo wake mmoja akipotea atahakikisha anamtafuta na kumrudisha kundini…Hivyo Yesu kristo kupitia Roho mtakatifu amewaagiza watumishi wake kuwa na siku maalumu au vituo mbalimbali vya kupokea wale wote waliopotea. Ukienda hapo wataformat Had Disk Drive yako (roho) na kufuta cockies na caches (roho za giza) zote zisiweze kukufuata tana.

Ukitoka hapo unakua mtu mpya na unaweza kuishi katika kusudi lako kama mzaliwa wa kwanza ila kamwe usisahau Uimara wa Roho yako ndio unaohitajika kuweza kuishi katika Kusudi lako kama mzaliwa wa kwanza.
107-1075952_my-heart-is-broken-alone-and-crying-boy.jpg

The End…
[Comment, Like and Share)
~Da’Vinci

El maestro.
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
33,262
96,421
Mkuu unamanisha wa kwanza kuzaliwa kutoka kwa Baba au kwa Mama???
Maana mtu anaweza akawa wa 1 kwa mama yake ila kwa baba yake ni wa 8,na akawa wa 1 kwa baba yake ila 8 kwa mama yake.
Mkuu as long as unajitambu kua wewe ndio mkubwa katika familia yenu basi hii inakuhusu. Haijalishi kwa mama au kwa baba.. Ilimradi una watu wanaokuita dada ua kaka.

Lakini kwa mujibu wa nukuu zangu za Holly Scriptures najua kwamba kipindi hicho Mussa anapewa agano hilo ilikua ni aghalabu ntu kuzalia nje. Bila ndoa.
so Ndio maana sheria ilikua specific mno kua mzawa wa kwanza wa familia ya ndoa kwakua walikua hawazai bila ndoa.

Mambo yanabadirika Mungu analegeza sometimes ili kuendana na wanawe
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
33,262
96,421
Umeelezea vizuri ila kwa wakristo, mzaliwa wa kwanza ni Yesu na sisi wote tunakuwa wazaliwa tunaofuata , kwaiyo ukimwamini kristo unakuwa huesabiki km mzaliwa wa kwanza .
Simply and Clear
ila ni nzaliwa wa kwanza kiroho kwetu
Gratitude
 

Similar Discussions

143 Reactions
Reply
Top Bottom