Je,Watu wanaowadharau wanywaji wa pombe za asili,ni uelewa Mdogo,Ulimbukeni au kufuata Mkumbo?

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!


Ni kwanini vinywaji au pombe za kienyeji ambazo madhara yake ni madogo hazina wanywaji wengi ukilinganisha na pombe za kisasa?

Tena ukionekana unakunywa pombe za kienyeji unaonekana wewe ni mlala hoi,hoe hae na utadharaurika miongoni mwa watu kwenye jamii!.

Pombe za asili ninazozungumzia hapa ni

1.Ulanzi
2.Mnazi
3.Mbege
4.Dengelua
5.Ulaka
6.Tende
7.Kayoga
8.Myakya
9.Kindi
10.Kang'ala
11.Ujimbi

Hizo ni baadhi tu ya pombe za asili ambazo utengenazi wake ahusishi kemikali yeyote bali ni usindikaji na uvundikaji wa vyakula tu kama mahindi,ulezi na mtama!.

Pombe hizi za asili zimekuwa hazina madhara sana ukilinganisha na pombe za kisasa zikiwemo KONYAGI,K-VANT,HANSOS CHOICE,GONGO,VISUNGURA N.k

Japokuwa Pombe ni Pombe tu lakini huwezi linganisha kimadhara hizo Pombe za asili na zile za kisasa!.

Je,ni kwanini kama ndivyo ukinywa hizo Pombe za asili zisizokuwa na madhara makubwa unaonekana Mshamba,Usiyejielewa,Masikini,fukara,usiyekuwa na akili timamu,mtu wa kijijini?

Unadhani ni kitu gani kinasababisha anayekunywa KONYAGI kuonekana Mjanja kushinda anayekunywa Ulanzi?
 
Ila gongo 🙌🏾🙌🏾
Ukinywa lazma ujidharau na udharaulike maana huwa inazeesha na kwa wapikaji wa mijini, huwa wanaongeza spirit na madawa ili iwe kali zaidi. Kwa hiyo mazingira ya uandaaji wake na ubora wake bado ni mtihani
 
Unadhani ni kitu gani kinasababisha anayekunywa KONYAGI kuonekana Mjanja kushinda anayekunywa Ulanzi?
Ulanzi unahifadhiwa kwenye ndoo, pipa na kusambazwa kwa kopo ambalo sio ajabu ukilikuta linatumika hata msalani😂😂

KONYAGI huhifadhiwa kwa chupa nzuri na safi na huvutia hata kwa kuitazama tu.

Unaweza kuona hapa mnywa ulanzi ni mchafu na mshamba mshamba 😁😁

Mnywa KONYAGI ni smart kwa sababu ya usafi wake.
 
Mbona komoni umeisahau wanatengeneza kutumia mahindi

Ila pombe za kienyeji ukinywa unasahau kuoga mkuu,sijui huwa zinashida gani
 
Package yake wapaki vizuri kushare banga/kitochi haipendezi. Lakini hao ni watu muhimu ukiwa unaenda kununua kiwanja, nyumba, shamba. Huwa wana historia ya kweli na wanajua mipaka na migogpro yoote ya eneo husika.
 
Hapo nikiendaga kijijini nakunywaga ulanzi na komoni. Ile ukiipata yenyewe iliyopikwa kwa kufuata mtaala wa cambrige unatoa gesi puani kama scania.
 
Tatizo ni mazingira yanapouzwa hizo pombe. Mara nyingi yanakuwa hovyo sana
 
Back
Top Bottom