Je, wapinzani ni wakombozi?

Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.
 
So what's the correlation between being a Freedom fighter and International cooperation? Anyway,You are very Right!!!
 
Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.

hapo kwenye blue angalau ulikuwa unajaribu kusema kitu,
ila hapo kwenye RED, labda ulitaka kutumia past tense ila ukajisahau..Vita ya uhuru wa nani tena. wazee walishatupatia uhuru. Vita ni kuondokana na umaskini, ujinga na maradhi.
 
kama ni kupigania uhuru basi ni bora uende zimbabwe kwa mugabe!nadhani huyo ndiye mtawala bora na chama chake
 
Uhuru upi tena?wa kujitawala na kuamua mambo yetu bila kuingiliwa!?Una uhakika waliopigania uhuru ndio wana uchungu na nchi yao?Ktk wapigania uhuru ni nani unaemjua alishirikiana na Nyerere kuupigania uhuru?Unajaribu kuwashawishi watu humu Jf lakini wewe unaonekana una chuki na Chadema,pili utakuwa umetumwa sbb ya njaa zako,Inamaaana hukuona chama kingine cha kukishutumu?Kwangu wewe ni mnafiki mfuata bendera,usiejitambua na mengine mengi.Fikiri kabla ya kudumbukia humu Jf
 
MzeewaHoja Mbona unaniaibisha? Hivi una maana watakapokuwa wametoweka hao walioupigania uhuru itabidi tukawaite wakoloni waje watawale tena kidogo ili tuupiganie tena?? Au ndiyo yale yale mawazo ya mfumo wa kifalme unataka kutuambia kuwa sasa tutawaliwe na familia zilizoupigania uhuru?

Hebu fanya kazi kidogo ya kujieleza ili tufahamu na sisi hizo sera zao ulizoziponda namna hiyo. Huenda wakajitokeza wakakusaidia kuzielewa. Maana usije kuwa kwenye lile kundi tulilokwishasema litahitajika kupelekwa jela ya kufundishwa demokrasia na haki zako mwenyewe. Maana kuna waliolewa CCM wanahitaji matibabu.

Wengi sana hapa ukiona wanatetea sana CDM wala si wanachama wake, ila kimefanikiwa angalau kusimama chenyewe kijasiri na bila kuogopa kukipinga Chama tawala kwa kulegalega kwake. Sasa wewe ni Chama kipi umeona kinaweza zaidi?? Hebu jiulize, ukiiondoa CDM leo, Tanzania mara moja tunarudi pale pale, "zidumu fikra za Mwenyekiti!" NAKUSHAURI UFIKIRIE TENA UMECHELEWA KIDOGO MZEE MWENZANGU.
 
SIJUI una maana gani kusema kuwa cdm si wapigania uhuru...Hivi ulitaka wapigania uhuru waendelee kuishi hata lini?
Mbona nchi hii kwasasa haihitaji sana watu waliopigania uhuru miaka ya 60?..kinachotakiwa kwa sasa ni kuikomboa nchi hii kutokana na ukoloni mamboleo, ambao unaletwa na chama tawala ccm!...Hujui kuwa adui yetu mkuu ni ccm mkuu...hujagundua kuwa pamoja na kujivua magamba bado hawajabadilika??
 
Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.

Hao waliopigania uhuru na wenye uchungu na nchii ndio hao wanofisidi nchi? Hao ndio wenye sera za kuwainua wananchi? MzeeWaHoja?????
 
Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.
So unataka kuwaambia wana JF kuwa Riz1, Nape, Hussein Mwinyi, Kigwangala, na wengine wa kariba yo ndo waliopigania uhuru wa nchi hii na kwa hiyo wana uchungu na Bongo?? Unaonaje ukienda kulala kwanza huenda ukaota kama wazee wa vikombe juu ya mustakabali wa taifa.
 
Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.

nahisi itakuwa si busara kushindana na mtu ambye kashanunua jeneza lake. huu ni wakati vijana tunataka kuijenga nchi yetu hatuna muda wa kupigishana kelele na wazee kama nyinyi amabao tangu uhuru mpaka leo mmeshindwa hata kutupatia umeme wa uhakika.
 
Hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiWengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.Ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.

Inabidi wapigania uhuru waishi miaka 200 ili waweze kuviongoza vyama, ila ndugu umesahau vita yetu sasa ni umaskini, njaa, elimu na ufisadi na viongozi wa cdm ni majemadari wa kweli kwenye hivi vita na wanamudu mapambano, swala la kimataifa sijui unalitazama labda ufafanue
 
Sasa wewe Mungu akurehemu. Natambua na naamini kuheshimu uhuru wa mawazo lakini haya yako siwezi kuita mawazo ya kuheshimu.

Mkombozi wa mwananchi ni mwananchi mwenyewe. CDM ni mkusanyiko wa wananchi hao wanaohitaji ukombozi.
 
hawana sera nzuri ya kumuinua mtanzania kiuchumiwengi wao sio wapigania uhuru wa nchi. Sio walioshiriki kikamilifu na uhuru wa tz. Kwa hivyo uchungu wao kwa nchii hii ni mdogo sana.ushirikiano wa kimtaifa upo mbali.

usharobaro ndo chanzo cha kuongeza idadi ya division zero tanzania....hujui kujenga hoja f,ala wewe, unakurupuka tu na njaa zako na ufinyu wa uelewa na kuja kupost ush,enzi hapa....em nenda kaoge huko alaa....
 
Upinzani unaoonekana sasa hivi upo na sura mbili, ndani ya CCM kwa CCM na CCM against CHADEMA.

Nitawakosoa nyinyi ambao mnatumia lugha chafu kwenye siasa na kutoa ushauri kwenu nyote:

Ni hivi, unapokuwa huna hoja hutatoa mtizamo sahihi wa kile unachokisema matokea yake unapotaka kudraw attention utatumia matusi na lugha chafu kuwafanya watu waone hisia zako bila kujua zimeletwa na nini.

Chadema mna watu wazuri saaana na watu wabovu kupitas maelezo. Kitakachowasumbua sana ni kile ambacho baadhi yenu wanakifanya na si kizuri kwa chama chenu, kutumia jazba na matusi kujenga hoja. Ninawataka wana CDM wooote kujipanga, someni hoja za CCM kama mpinzani mkuu, angalieni yale ambayo mnaweza mkayafukia kwa hoja zenu mpya na nzito. Na hii ndiyo ilikuwa siri ya ushindi wa kishindo wa Baraka Obama pamoja na mapungufu yoooote ya kihistoria na "kihadhi" ya kugombea uraisi.

CHADEMA kichwa sasa lazima kiwaume kujua mgombea anayeuzika katika uraisi ujaon ni nani? Maana kwa sera zenu za mgombea ni mara moja safi, democrasia ya kweli, nani atakayezidi uzito wa Dr. Slaa katika kuuzika? Ukiniuliza mimi, nadhani ni mojawapo wa vijana ambao kifikra wako fresh an wana moyo wa kuthubutu hata hoja zao mpaka sasa zinamwelekeo na mvuto wa hali ya juu, tunawaona kwneye vyombo vya habari. Sio Zito tafadhali! Shida mtakayoipata ni kuwa hawa CCM wanoongoza tayari walishaichakachua katiba na kulazimisha nchi hii iongozwe na wazee zaidi. Hivyo kwa hoja yangu kampeni ya Katiba mpya isilale iwe kipaumbele mpaka mate ushindi.

CCM imechafuka inanuka na imejaa matope, kwasababu tu wako baadhi ya watu walijimilikisha chama. Na hii kafara anayojitoa Nape, haiwezi kusahauliwa na wanachama wake, ama sivyo watakuwa wamekosa fadhila. Achilia mbali udhaifu fulanifulani aliyonao ambao upo pande zote za siasa wa kutumia personality ya kiongozi wa upinzani kujenga hoja badala ya sera. Anafanya kazi nzuri kweli kweli Bwana Nape kwa CCM kwa sasa na wako wengi tu ndani ya CCM hawapendi anachofanya maana kinaharibu yale matope waliyojipaka ili wasionekane huko waliko.

CCM mna nafasi ya kushinda iwapo tu mtagawanyika kati yenu na kikazaliwa chama kipya kikiwa na wanamabadiliko wa kutosha ndani ya chama. CCM imepoteza umaarufu kwelikweli kwasababu za siasa za Makundi. Maana shida yenu CCM mlijikita sana kweney mfumo wa serikali na usalama hivyo inawawia shida upinzani kupata ushindi wa kweli. Ila kwa hivi mlivyo tayari kama kutafanyika utafiti wa umaarufu wa chama na uongozi, hamtaamini matokeo yake.

Msijidanganye nchi hii mnaipeleka pabaya msisubiri mkajikuta mmechelewa, ongezeni kasi ya mabadiliko, na wale wanaoona wanaweza kujiengua basi liwepo kundi kubwa la kutosha kuleta nguvu ya upinzani wa kweli.
 
Mimi ni mtanzania ambae nimekua nikifatilia sana sias za hapa kwetu Tanzania.kutokana na hali legelege ya CCm,Chadema imekua ikijiongezea umaarufu kwenye jamii.ndio nikapata swali hiv Chadema ni Option au ndio solution??
 
Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano amefanya mambo mengi mema sana Tanzania, ila unajua kwanini hayaonekani na kwa nini upinzani unapata nguvu ya ajabu hata kama hawajajipanga kivile? Kwakuwa alianzisha vita na maadui zake, kwa nia njema, akakosa ushirikiano wa dhati wa vyombo husika kutekeleza aliyokusudia, sasa vita hiyo imegharimu muda wake mwingi kiasi kwamba hata hotuba zake hazina mvutao tena, anatoa hotuba zinazowa-address maadui zake sio wananchi! Kwa sasa sidhani kama ana muda wa kufuatilia yale aliyoota wakati anaingia tu madarakani ambapo wote tulisisimka na kusema hapa huyu ndiye tuliye mtaka, aliyoota maana kwa muda uliyobaki anasumbuliwa zaidi namaadui kuliko maendeleo. na hasa ukizingatia anajua adui akiingia madarakani anaweza kumdhalilisha kama akina Zambia na wenzake.

Pole sana Mh Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Mungu akupe hekima ya kukinusuru chama chako, na kulinda maslahi ya nchi hii na si yamaadui zako bila kujali hoja hiyo inatoka chama gani!
 
Mpaka leo uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki:
1. Kwa nini bila aibu tume ya taifa ya uchaguzi iamue kwamba itabandika orodho ya wapiga kura siku moja kabla ya kupiga kura badala ya siku saba kama sheria inavyoelekeza?
2. Kuna vituo 55 bandia vya kupiga kura! Kwa nini?
3. Kitendo cha kiongozi wa CHADEMA kukamatwa na kupigwa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na wana CCM! Kwa nini?

Kwa nini wapinzani wana tabia ya kunyamazia vitendo kama hivyo halafu wanakuja kulalamika baada ya uchaguzi?

Ni lini watanzania wataamua kupinga vitendo vya kihuni kama hivi vinavyotendwa na chama tawala?

Kwa nini wapinzani wanalamimika bila kuchukua hatua?

Bado kuna siku kama 9 kabla ya uchaguzi, kwa nini wapinzani wasipinge hivi vitendo kabla ya uchaguzi kuliko kujiandaa kuja kulalamika baada ya uchaguzi?

Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom