sindiswa
Member
- May 14, 2022
- 11
- 87
Bila kupoteza muda niende kwenye mada.
Nimekutana na matukio mawili yaliyonifikirisha na kunifanya nikaribie kwenu ili nipate mawazo yenu
Binafsi nimewahi kudate huko nyuma baada ya kumaliza masomo ya chuo siwezi kusema yalikua serious kwasababu bado nilikua sijapata kazi na kufikia malengo yangu mbali mbali niliyojiwekea. Nimefanya kazi sehemu kadhaa nikapata nafasi ya kwenda nje kujiendeleza kielimu. Baada ya kurudi Mungu hamtupi mja wake nimepata kazi nzuri nikafanikiwa kuanza ujenzi na sipo sehemu mbaya nikijaliwa mwisho wa mwaka nahamia kwangu.
Niwe tu mkweli mimi ni mchakarikaji haswa , sio wale wadada wanaopata vitu kwa kwa kutegemea wanaume hapa nilipo ni bidii yangu na support ya wazazi. Sasa katika maisha ya kazi nilibahatika kukutana na kaka ambaye katika kuzoeana tulianzisha mahusiano ambayo kwa namna moja yalikua serious ( ama ndivyo nilivyoyatafsiri) tulikua huru na wazi na baadhi ya nduguze walinifahamu.
Huyu kaka baadae katika ukaribu wetu alijua kwamba nimejenga na nina kabiashara kangu kaongeza kipato japo sikua najivuna lakini alianza kuonyesha inferiority na ikawa chanzo cha ugomvi. Nikisafiri kikazi alikua muda wote anapiga video call na voic call nikajua mahaba kumbe alikua na wivu na vitu kama hivyo mwishowe tulishindwana maana ikitokea kupishana anasema unaringa sababu una gari, umejenga etc kwa hiyo nikagundua hajiamini na anawivu hata usiopaswa ( kuna wakati alisema niache kazi kwasababu nasafiri sana) kitu ambacho kilipelekea mimi kukosa furaha na hatimae nikaumaliza mwendo.
Juzi tu nimekaa na rafiki yangu wa karibu ambae ni single mom wa baby girl mmoja mume alifariki mapema mno ila ni mpambanaji haswa na kwao wanamsupport sana kwa hiyo mambo yake si haba ana kazi nzuri, ana kwake , usafiri na mwanae anaishi nae vizuri sasa katika kufuta upweke akakutana na mkaka wakaanza mahusiano.
Miezi michache mbele mkaka akamwambia dada najiskia vibaya kuwa na mwanamke alienizidi anajiona ha-fit kwa huyu dada ( yani sio wa level zake) na anaona kama dada atamuacha afate wa size yake. Ninavyomfahamu rafiki yangu yuko humble sana na ana aibu yani sio mdada wa mjini .
Ameumia kuachika kisa tu mwanaume anahisi hawaendani vipato ( Mwanaume ni mwajiriwa private) , ni wiki inakata mwanaume kakata mawasiliano.
Ina maana siku hizi wanaume wanaogopa kukuta mwanamke ana kila kitu? Wanaona watadharaulika ama wanaona watachitiwa? Karibuni tujadili kwa lugha ya staha na heshima.
Ikiwezekana ushauri utolewe nini kifanyike kwa dada anaejikuta katika situation ii na vijana wafanyaje ili wasihisi hawana nafasi kwa wadada waliowazidi status.