TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 4,975
- 15,316
Kuanzia mwaka 1920 -1933 pombe zilipigwa marufuku nchini Marekani. Ilikua ni kinyume cha sheria kuzalisha, kusafirisha au kuuza pombe nchini humo. Lengo lilikua ni kupunguza matatizo yaliyokua yanatokana na ulevi kama uhalifu, rushwa, matatizo ya kijamii, mporomoko wa maadili, afya duni nk pia kupunguza gharama za kuhudumia wafungwa waliotokana na matatizo ya ulevi.
Matokeo:
Hakuna manufaa yoyote ya maana yaliyopatikana. Uhalifu uliongezeka, rushwa ziliongezeka, magereza yalizidi kujaa wafungwa na serikali ilipoteza kiasi kikubwa zaidi cha kodi. Wanywaji wengi walihamia kwenye matumizi ya dawa za kulevya, bangi, na pombe za kienyeji zilizotengenezwa vichochoroni ambazo zilikua hatari kiafya.