Je, wajua kwamba uchawi huvaliwa kama nguo?

Mshana Jr,Hivi Mchawi anaweza kuficha Uchawi wake hata kupelekea Waganga kuamini kuwa hana Uchawi?

Kwanini Wachawi wengi wanaishi miaka mingi sana hapa Duniani?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapana sio rahisi kufanya hivyo kwa wazee wa busara wengine na wana kilinge...
Wanaishi miaka mingi kwakuwa wanaishi simple, hawana changamoto za kimaisha, wanapata almost kila kitu bure na kwa namna fulani uchawi wao unawalinda

Jr
 
Hapana sio rahisi kufanya hivyo kwa wazee wa busara wengine na wana kilinge...
Wanaishi miaka mingi kwakuwa wanaishi simple, hawana changamoto za kimaisha, wanapata almost kila kitu bure na kwa namna fulani uchawi wao unawalinda

Jr

Maana kuna Jirani yangu alihisiwa ni Mchawi.Akaletewa Mtaalamu kumtoa Uchawi,cha kushangaza Mtaalamu hakukuta kitu.

Lakini Watu wanahisi labda alificha uchawi,maana waliokutwa na mambo ya kishirikina wakienda kwa Waganga wanaambiwa huyo Bibi ni Mchawi,lakini wakifika kumtoa uchawi hawauoni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi huwa kuna uwezekano wa mtu mchawi kukuwekea kitu cha kudhuru kwenye chakula bila yeye kukukaribia? Au kwa maana nyingine mchawi aweza kujifanya asionekane kwa macho ya nyama hivyo kukuwekea sumu kwenye kitu unachokula? ...kwako Mshana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huwa kuna uwezekano wa mtu mchawi kukuwekea kitu cha kudhuru kwenye chakula bila yeye kukukaribia? Au kwa maana nyingine mchawi aweza kujifanya asionekane kwa macho ya nyama hivyo kukuwekea sumu kwenye kitu unachokula? ...kwako Mshana

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana kabisa lakini sio hawa wa siku hizi

Jr
 
Kama huyu
Unaweza kushangaa na hata kujiuliza kwamba mtu mchawi anawezaje kupigwa kujeruhiwa na hata kuuliwa na watu wa kawaida kabisa wasio wachawi
Kuna baadhi ya mambo ni lazima uvae vazi maalum yani kama watu wa maabara kwenye kemikali Kali, wazima moto, waendao anga za mbali nknk... Yaani hawa ni baadhi wafanyao shughuli ambazo vazi rasmi ni lazima kwenye uchawi na ushirikina nako ni hivyo hivyo
Kwa wale waliowahi kufika kwa waganga wa kienyeji wanalifahamu hili vema, unapoenda kwake, kama hayuko kikazi atakuchukua mpaka chumba maalum, kule atavaa mavazi maalum ndio aingie kazini
Mavazi yale avaayo ndio NGUVU na utii na ukuu wa NGUVU za giza, ndio kibali na kitambulisho cha kuweza kufanya atakayokufanya
Kwahiyo hata wale wanga na wachawi wanaosafiri usiku wana mavazi na vitendea kazi maalum kwa kazi hiyo.... Nje ya hapo ni wachumba tu.. Na ndio maana huweza kudhuriwa ama kudhurika kwa urahisi kabisa,! Ndio maana nao huugua magonjwa mengine ya kawaida kabisa ya kutibiwa hospitali za kisasa, ndio maana nao hufa vifo vya kawaida kabisa
Mchawi mshirikina ama mganga hawezi kuzivaa hizo NGUVU muda wote, ni nzito na zenye mambo ya kutisha sana, wachawi na waganga wa kweli anapokuwa amevaa NGUVU husika huona mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida na mengi yanatisha mno...... Mwili huu wa nyama hauwezi kuhimili kubeba nguvu za giza kwa muda mrefu.... Ikitokea hivyo mtu hachukui round anakufa
Wanaokufa wengi kishirikina, wakati mwingine sio kwamba kafanyiwa chochote kibaya, bali ni kubebeshwa tu zigo zito la hizo NGUVU kwa muda mrefu na hatimaye mwili kuchoka na kushindwa kuhimili uzito na kufa kifo cha kawaida kabisa
09a23ddd838cf6b93f7bd711df71600c.jpg
mganga.jpeg
 
Back
Top Bottom