Je, wajua kwamba uchawi huvaliwa kama nguo?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,605
696,697
Unaweza kushangaa na hata kujiuliza kwamba mtu mchawi anawezaje kupigwa kujeruhiwa na hata kuuliwa na watu wa kawaida kabisa wasio wachawi
Kuna baadhi ya mambo ni lazima uvae vazi maalum yani kama watu wa maabara kwenye kemikali Kali, wazima moto, waendao anga za mbali nknk... Yaani hawa ni baadhi wafanyao shughuli ambazo vazi rasmi ni lazima kwenye uchawi na ushirikina nako ni hivyo hivyo
Kwa wale waliowahi kufika kwa waganga wa kienyeji wanalifahamu hili vema, unapoenda kwake, kama hayuko kikazi atakuchukua mpaka chumba maalum, kule atavaa mavazi maalum ndio aingie kazini
Mavazi yale avaayo ndio NGUVU na utii na ukuu wa NGUVU za giza, ndio kibali na kitambulisho cha kuweza kufanya atakayokufanya
Kwahiyo hata wale wanga na wachawi wanaosafiri usiku wana mavazi na vitendea kazi maalum kwa kazi hiyo.... Nje ya hapo ni wachumba tu.. Na ndio maana huweza kudhuriwa ama kudhurika kwa urahisi kabisa,! Ndio maana nao huugua magonjwa mengine ya kawaida kabisa ya kutibiwa hospitali za kisasa, ndio maana nao hufa vifo vya kawaida kabisa
Mchawi mshirikina ama mganga hawezi kuzivaa hizo NGUVU muda wote, ni nzito na zenye mambo ya kutisha sana, wachawi na waganga wa kweli anapokuwa amevaa NGUVU husika huona mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida na mengi yanatisha mno...... Mwili huu wa nyama hauwezi kuhimili kubeba nguvu za giza kwa muda mrefu.... Ikitokea hivyo mtu hachukui round anakufa
Wanaokufa wengi kishirikina, wakati mwingine sio kwamba kafanyiwa chochote kibaya, bali ni kubebeshwa tu zigo zito la hizo NGUVU kwa muda mrefu na hatimaye mwili kuchoka na kushindwa kuhimili uzito na kufa kifo cha kawaida kabisa
09a23ddd838cf6b93f7bd711df71600c.jpg
 
Mlipe tu hakuna namna, hiyo ni dhulmati
Nje ya maada hii. Kuna Mzee mmoja mtaani kwangu ni rafiki yangu anapenda sana kuniomba hela zamani nilikuwa nampa sana Baadae nkaambiwa ni bonge la chuma ulete mtaa mzima unamjua. Sasa siku kila akiniomba nashindwa kumpa au nampa mtu mwingine ampe. Ni nilikua nimemzoesha ila ki ukweli ni mzee mmoja yuko poa sana na tunaheshimiana nae. Nini nifanye asiweze kuchuma kwangu na kupeleka kwake?
 
Nje ya maada hii. Kuna Mzee mmoja mtaani kwangu ni rafiki yangu anapenda sana kuniomba hela zamani nilikuwa nampa sana Baadae nkaambiwa ni bonge la chuma ulete mtaa mzima unamjua. Sasa siku kila akiniomba nashindwa kumpa au nampa mtu mwingine ampe. Ni nilikua nimemzoesha ila ki ukweli ni mzee mmoja yuko poa sana na tunaheshimiana nae. Nini nifanye asiweze kuchuma kwangu na kupeleka kwake?
Saa nyingine ni maneno ya watu ila kama unahofia ukimpa mpe noti lakini uliyokata kipande kidogo
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom