Kisoda2
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 2,475
- 745
Mkuu Pascal Mayalla karibu tena na hongera kwa kutukumbusha machungu.
Kwa wafuatiliaji wa taarifa za nchi za wenzetu watakubaliana na mimi kwamba kuna vyombo vya habari ambavyo kazi zao ni pamoja na kureport progress za maagizo na ahadi za viongozi wa serikali.
Sisi hapa kwetu hatuna hii kitu, waandishi wakishakaa press mkuu yeyote akatoa agizo, hawarudi tena kuandika/kutangaza juu ya utekelezaji wa agizo lile, wala hawatoi mrejesho wa kipi au hatua zipi kiongozi amechukua kwa agizo lake kutotekelezwa, na hii imesababisha kila kiongozi anatoa tamko tu.
Tuna watu kama kina Makonda (RC); show rooms Kigamboni, Kukagua Guests saa za kazi, shisha, madawa, ombaomba Dar, walotelekeza watoto, kupima tezi dume, kukusanya vijana wasio na ajira etc
Kigwangala; Umiliki Loliondo, Ardhi Monduli, MRI Mbeya (akiwa naibu Afya), majangiri, etc
Kangi; Huyu sitaandika chochote.
Jafo, kuna waziri wa kufufua Viwanda, na wengine wote, tulitakiwa tuwe na chombo cha kufuatilia maagizo yao na wapi iliishia au inaendeleaje.
Kazi unayoifanya Pasco ilitakiwa ifanywe na vyombo vikubwa vya habari, na ingesaidia sana kuzuia matamko ya kimuhemko kwa sababu mtoaji angekaa akiwaza siku ya kujibu progress ataumbuka.
Na kwa style hii ndipo tunapopigwa ngwala na watawala wetu!! Halafu tunabaki kulia lia.