Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?.

Kizalendo kabisa na niko upande wa watanzania wenzangu lakini kwa upeo mfinyu kabisa sioni kama tunachetu kwenye mazungumzo hayo.
Wale jamaa kutoa pesa bila kuzibackup na maelezo ya kueleweka ni kinyume kabisa na Sera zao wanazofundishana kila siku '' Barrick code of Conduct and anti-corruption''. Na wanamifano mingi tu ya makampuni makubwa kuliko hata wao ulimwenguni yalivyoingia chaka kwenye sheria yakashtakiwa na Kulipa mabilioni kama sio matrillion ya pesa wakifundishana jinsi ya kukwepa kuingia kwenye makosa ya namna hiyo. Sioni wakifanya kosa la kuwaingiza hasara kiasi hicho. Hata kama ni wizi utakuwa kisheria.
IKIWA KILICHOGUNDULIKA NA TUME YA PROF. MRUMA Hakikuwa Technically Correct tutasubiri sana. Otherwise kwa sababu ni mambo ya siri Tusubiri wahusika wenda wao wanajua kuliko wapiga domo mitandaoni huku.

Maoni.
Mkataba uliyokuwapo ulikuwa unaruhusu kusafirisha makinikia, haikuwa kosa kwao bali la waliopitisha huo mkataba.
Uchunguzi wa akina Prof Mruma ulitakiwa ufanyike pakiwepo wawakilishi wa Barick pamoja na mtu wa tatu ambae ataangalia na kuthibitisha kuwa, ulifanyika kwa kufuata taratibu za kitaalamu. Uchunguzi watz watupu ulikosa nguvu na hata hoja. Huwezi kuishitaki Barick popote kwa matokeo yenu wenyewe ya uchunguzi.
Propesa Kalamagamba mwanasheria nguli alikuwa analijua hilo kama Lissu na wanasheria wengine walivyolifahamu.
Kwa nini "Mzalendo" Propesa na wengine waliyo karibu na Jiwe, waliamua kutoa matumaini hewa kwa watz, ni jambo ambalo linasikitsha.
Kwa mitindo ya aina hii Tz haitokuja kusogea mbele kimaendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa bahati mbaya kwenye suala hili la madini, tumeingia kichwa kichwa katika kila sekta. kuanzia sheria mpya tulizotunga, uzuiaji wa makinikia, uundwaji wa zile kamati mbili, na hatua zilizochukuliwa, na hata katika hayo "mazungumzo" na Barrick. kote huko tumekwenda kichwa kichwa na tumeangukia pua.
Siku ambayo Tundu Lissu alipigwa risasi, asubuhi alikuwa bungeni na alitoa hoja nzito kuonesha jinsi zile sheria zilizopitishwa kuhusu sekta ya rasilimali zetu ikiwemo madini, zilivyokuwa za hovyo.

Tundu Lissu ameshughulika na hawa jamaa wa madini kwa miaka mingi. ni mzoefu sana tu. na katika mengi ambayo amekuwa akitahadharisha miaka yote hii, amekuwa sahihi. cha kushangaza ni kwamba badala ya serikali kumshirikisha, hata kama ni mtu wa upinzani, kama alivyomshirikisha Spika Anne Makinda enzi zile katika uwanja wa sheria, anaonekana ni adui. sasa serikali iko kwenye CUL DE SAC, na hatujui tunatokaje hapo bila kuaibika zaidi.
 
Mkataba uliyokuwapo ulikuwa unaruhusu kusafirisha makinikia, haikuwa kosa kwao bali la waliopitisha huo mkataba.
Uchunguzi wa akina Prof Mruma ulitakiwa ufanyike pakiwepo wawakilishi wa Barick pamoja na mtu wa tatu ambae ataangalia na kuthibitisha kuwa, ulifanyika kwa kufuata taratibu za kitaalamu. Uchunguzi watz watupu ulikosa nguvu na hata hoja. Huwezi kuishitaki Barick popote kwa matokeo yenu wenyewe ya uchunguzi.
Propesa Kalamagamba mwanasheria nguli alikuwa analijua hilo kama Lissu na wanasheria wengine walivyolifahamu.
Kwa nini "Mzalendo" Propesa na wengine waliyo karibu na Jiwe, waliamua kutoa matumaini hewa kwa watz, ni jambo ambalo linasikitsha.
Kwa mitindo ya aina hii Tz haitokuja kusogea mbele kimaendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja wafanye kazi zao, wao ndio wanajua yasirini na wazi . Sisi walalahoi tusubiri matokeo. Yakiwa chanya tunamshukuru Mungu yakiwa hasi tutachukua "lessons learned" hata tusipojifunza kitaifa tunaweza kujifunza ktk level za familia au mtu mmojammoja.
 
Mkuu ripoti ya makinikia na Tanzanite ilitaja wanasiasa zaidi ya 20 ambao kwa namna moja ama nyingine wametuhujumu hadi kutufikisha hapa tulipo hasara ya zaidi Trillion 200+ je hatua gani magufuli kachukua dhidi ya hao mafisadi?? Ina maana hao mafisadi wana nguvu kiasi gani hadi waogopeke??
Simply watakwambia yalikuwa maagizo toka JUU, na hao wa juu wanalindwa na Katiba.
Ndio maana TZ haiwezi kuwa na kiongozi smart, cuz unajua una kinga na issue zote zikifika kwa mkuu mstaafu ndio inakuwa "sky is the LIMIT"
 
Ndio nyie mnaotombewa mke alafu unajisifu kwamba umechukua hatua ya kumkanya asirudie tena. ishu hapa si kuchukua hatua tu (god damn it) zinatakiwa hatua zinazotoa suluhisho.... PUMBurAVU wewe..... mtu anakutia kidole cha matako af unamgeukia na kumnyooshea kidole kumwambia aache ujinga...? next time he's gonna put dic in yo as** na huku ukiangalia...... kuchukua hatua ni pale unapomgeukia na kuhakikisha sura imechakaa kwa mkong'oto, hiyo ndo kuchukua hatua, na hatorudia......

Tufike mahali tusifie hatua zenye dhamira ya kweli baada ya kuzitathmini na kuzichambua.... viongozi wote wa sasa ni wapuuzi tu..... hakuna maendeleo watakayoleta zaidi ya kufanya mambo yale yale kwa kuwa kiongozi wao mkuu ni jiwe.
The dic is IN long time, tutulie watule......Japo mi simo ahahaahahaaa
 
Nilimshangaa sana Kabudi aliposema kuwa wao (Barrick) walikuwa 24 lakini sisi tulikuwa 5, na tukafanikiwa.

Ukisikia mwanafunzi mbumbumbu anasema mtihani ulikuwa rahisi sana lakini wenye akili wanasema mtihani ilikuwa mgumu, ujue kuwa yule mwanafunzi mbumbumbu, kuna uwezekano mkubwa, hakuelewa hata kilichoulizwa.

Naikumbuka sehemu ya hotuba ya Rais wa Barrick mwaka 2001:

Barrick has realized overall profit throughout since it was started. While other companies were collapsing, Barrick kept on fluorishing. It is not because of the gold reserves, money or equipment it is possesing but because of the people we have.

In short ni kuwa, hakuna kishika uchumba wala kodi yoyote tutakayolipwa. Madai yetu yalijengwa kwa kutumia taarifa za uwongo. Huwezi kuutegemea uwongo ili kushinda.

It was for political popularity from brain lows. There we have got it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LISSU ALIISHA MALIZA.ALISEMA MTAKUMBUKA MANENO YAKE BAADAE, ALIFIKIA KUENDA MBALI NA KUSEMA MAGUFULI SIO WA KWANZA KUUNDA TUME YA MADINI NA KUTABIRI HATALIPWA CHOCHOTE KUTOKANA NA SHERIA MBOVU ZILIZOPITISHWA KWA HATI YA DHALULA. PIA ALISISITIZA KUWA MAPROFESSOR UCHWARA A.K.A PROFESSORIAL RUBBISH WAMEKOPI HADIDU ZA REJEA ZILEZILE ZA AKINA KIPOKOLA, MASHA, MBOMA NA BOMANI.
NAKUMBUKA PROF. KABUDI WAKATI ANAKABIDHI REPORT YAKE AKAANZA KUSIFIA HUDUMA NZURI YA CHAKULA NA VINYWAJI WALIZOPEWA WAKATI WA UCHUNGUZI WA TUME YAO. YAANI TUNA MAPROF. WAAJABU SANA TZ NA NJAA NDO ZINA WASUMBUA
PERSONALLY NIMEANZA KUMUELEWA NA KUMUAMINI LISSU

Man watu werevu tulimuelewa TL huwa hakurupuki wala kuropoka, he does his home work thoroughly, he is a policy wonk and a work holic! Na zaidi ya hapo yule ni "Nabii"; (binadamu wa kawaida how do you survive an assasins bullet tena 30+?!)
Japo wakati utaongea, lakini pia Nji hii itamkumbuka TL both akiwa hai na akishatangulia mbele ya haki! Get well soon TL
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kidogo, kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa. hii ni mada ya swali
Jee Wajua Kuwa Mazungumzo Yetu na Barrick Ni Mazungumzo Tuu? Mwenye Uamuzi wa Mwisho ni Acacia!, Kwa Nini Hakushirikishwa?!. Jee Tutalipwa?.

Kwanza its sad kwa sisi Watanzania kupata update ya hatima ya rasilimali zetu, ni kutoka huko huko kwa hawa mabwana wa rasilimali zetu, au wezi wetu!.

Leo nimepata muda kufuatilia hatima ya mazungumzo kati ya serikali yetu ya Tanzania na Kampuni ya Barrick kuhusu hatma ya makinikia ya Acacia yaliyozuliwa, kupitia taarifa kwenye tovuti ya Barrick, mazungumzo yameelezwa kuwa yanaendele vizuri
Barrick Gold Corporation - Update on Discussions with Government of Tanzania

Acacia nao kwenye tovuti yao nao wameeleza kitu kile kile kilichoelezwa na Barrick
Press Release Item

Jambo la kwanza la maendeleo ya mazungumzo haya, ni mazungumzo yasiyo na time frame, yaani hayana muda maalum wa kumalizika na kufikiwa makubaliano!, mazungumzo ya aina hii ni mazungumzo gani yasiyo na SMART Objectives yanaendelea tuu na yanaweza yakaendelea tuu bila mwisho?!.

Barrick wametoa statement fupi ya page 1 yenye para 3 zenye lines 15 na maneno 146 lakini wakaweka angalizo lenye page 2, para 4 zenye lines 69 na maneno 775!. One has to be good kusoma hiyo statement together with angalizo kuelewa the motive behind.

Tukija kwa Acacia, wao wametoa tuu statement ya Barrick bila kuweka angalizo la pembeni ila wao wameweka msimamo wao wazi kuwa "The Company has been supporting Barrick in its discussions with the GoT, but has not been directly involved in those discussions to date. Any proposal received by the Company in the future that might be agreed in principle between Barrick and the GoT as a result of those discussions will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors". Wanaunga mkono mazungumzo hayo lakini wao sio sehemu ya mazungumzo hayo na kwanza hawajahusishwa popote hadi leo, hivyo chochote kitakachofikiwa na mazunguzo hayo kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, ni lazima kiridhiwe na kamati yao maalum!. Hii maana yake maafikiano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali yetu na Barrick sio final and conclusive, mwennye uamuzi wa mwisho ni Acacia!. Kama hali ni hii, kwa nini wanasheria wetu nguli na makini hawakuwahusisha Acacia kwenye mazungumzo haya ambao ndio the determinant ya utekelezaji wa makubaliano yoyote?. Jee mnatambua kuwa chochote ambacho serikali yetu itakubaliana na Barrick, hala Acacia wakakataa kutekeleza, hakuna kitu chochote ambacho tunaweza kuwafanya?.

Wakati mazungumzo yetu na Barrick yako kwenye dilly dallying, wenzetu Barrick wameelekeza macho na masikio yao China!,
"Barrick’s focus on China is real and deliberate.
Barrick’s focus on China is real and deliberate. In 2014, we created the position of President for Barrick China to manage our interests there. In 2015, we sold half of our ownership in the Porgera gold mine in Papua New Guinea and began joint operations with the buyer, Zijin, one of China’s big three gold miners. In 2017, we formed a 50-50 joint venture with Shandong Gold, another one of the big three, at the Veladero mine in Argentina. In addition, two of China’s largest banks—ICBC and China Construction Bank—have joined Barrick’s revolving credit facility, the first time either has forged such a relationship with a Western mining firm".

Hivyo mkisikia Barrick imeuza interest zao za Acacia kwa Wachina, naowaomba msishangae!, naamini wale "jamaa zetu" pia ni mingoni mwa watumishi wazelendo wa Acacia, hivyo wakiona ziara za makundi ya watu kutoka China huku wakiandamana na mabosi wa Barrick, waripoti haraka sana maana usikute ni ngombe wetu wa maziwa yuko mnadani!. Wazungu ambao ni watu wako very much time conscious, ukiona wanazungumza na wewe mazungumzo yasiyoisha bila kuonyesha time concern, kama wewe ni mtu unaejua kutazama mbali, ni lazima uogope!.

Swali la Msingi ni Jee Tutalipwa?.
Kwa mazungumzo ni siri, hakuna ajuaye ni nini kimekubaliwa na nini hakijakubaliwa, my honest opinion ni kuwa hatutalipwa!, hata kile kishika uchumba cha dola milioni 300, I doubt kama tutalipwa, kwa sababu the bone of contention, ni Tanzania kuibiwa kwenye makinikia kwa vile hatujui kilichomo!. Ili tujue kilichomo ni kama tuu tutayachenjua makinikia sisi wenyewe!. Sijawahi kusikia lolote kuhusu uchenjuaji wa makinikia yale, hivyo hata zile fedha za Noah zetu, zijui kama hata robo zitalipwa!.

Lets hope for the best!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
Kuna mtu kashalipwa 'watch out' Hakuna mazungumzo business as usual!!
 
Ishu si kulipwa TU...Ishu ni kwamba atleast tumeonyesha kuthamini RASILIMALI ZETU....tatzo sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana Tunakaa kusubiri kuona mambo yakiharibika tu tupate sehemu ya kusemea PUMBA zetu LAKINI hatutaki kabsa kupongeza hatua zilizo chukuliwa kuzuia KUIBIWA RASILIMALI ZETU na hawa mabwana wakubwa....Tumpongeze JPM kwenye hili jamani
Hata kama BARRICK anaenda kuuza hisa zake kwa hao WACHINA hii ni kwa sababu tu MIANYA YAO YA KIJINGA KUTUPIGA SISI WATANZANIA IMESHTUKIWA angethubutu vipi kuuza HISA ZAKE kama tusingemshtukia????Hata huyo mchina atakaekuja LAZIMA tuanze nae VIZURI
KIBST pamoja na maongezi mazuri yakupendeza umesahau kitu kizuri haukutaka kukisema..Hatujawahi kuibiwa hata na MTU mmoja kupitia uwekezaji..TUMEJIIBIA wenyewe kupitia MIKATABA ya uwekezaji. Haya yakifanyika serikali hii ilikuwepo. Uthubutu wa Mwenyekiti wetu ni pale alipobadili sheria kujaribu kuzuia..Nawasilisha
 
Mara nyingi ukweli huwa haujifichi, na ukweli hukuweka Huru.
Report hazikufanyika huru kisayansi bali kisiasa. Namna ya uwasilishaji tuu kwa muelewa wa mambo ulileta ukakasi, matangazo yalivyokuwa nayo pia ilileta ukakasi, na report ya pili Mwenyekiti wake alikuwa anatetemeka na hajiamini means kuna yaliyotamkwa si sahihi.
Mzalendo yeyote hatapenda kuonea Kama asivyopenda kuonewa. Je, Kama maprof Wetu waliyoyaona ni kweli kwanini wasitafute Mchunguzi huru wote Serikali, Barick na Accacia wampe namna ya kuchukua sampuli na namna ya kupima majibu yatolewe ili ijulikane na kukubalika kwa wote, hapo watakosa cha kusingizia then serikali inataifisha kila Kituo chao.
 
Back
Top Bottom