Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?.

Nilimshangaa sana Kabudi aliposema kuwa wao (Barrick) walikuwa 24 lakini sisi tulikuwa 5, na tukafanikiwa.

Ukisikia mwanafunzi mbumbumbu anasema mtihani ulikuwa rahisi sana lakini wenye akili wanasema mtihani ilikuwa mgumu, ujue kuwa yule mwanafunzi mbumbumbu, kuna uwezekano mkubwa, hakuelewa hata kilichoulizwa.

Naikumbuka sehemu ya hotuba ya Rais wa Barrick mwaka 2001:

Barrick has realized overall profit throughout since it was started. While other companies were collapsing, Barrick kept on fluorishing. It is not because of the gold reserves, money or equipment it is possesing but because of the people we have.

In short ni kuwa, hakuna kishika uchumba wala kodi yoyote tutakayolipwa. Madai yetu yalijengwa kwa kutumia taarifa za uwongo. Huwezi kuutegemea uwongo ili kushinda.

It was for political popularity from brain lows. There we have got it.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Bams kwa kuliona hilo. Mwalimu Nyerere aliwahi kulidokezea taifa juu ya "negotiating tactics" za Wazungu na alitolea mfano wa Cleopa Msuya alipokuwa akijadiliana na EU akienda Paris, kwamba alikuwa anaingia mkutanoni peke yake wazungu wanakuwa wengi. Hata hivyo Msuya alikuwa mahiri wa kuweza kuhimili mapigo ya wazungu na wakaendelea kushirikiana nasi hata kama hawakubaliani kwa kuwa tulikuwa n.a. "very strong counter arguments".
Wale 15 walivyokuja kila mtu alikuwa na kazi ya kufanya SWOT ANALYSIS ya eneo au mtu mshiriki katika mazungumzo yale na baada ya hapo wanapata ripoti ya awali ambayo itawaelekeza katika kujadiliana na sisi. Ni matumaini yangu vyombo husika waliliona hili na kama mazungumzo yanaendelea basi watilie maanani mambo ambayo walikuwa wakiyasikiliza kwa makini sana. Niishie hapo kwa leo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu si kulipwa TU...Ishu ni kwamba atleast tumeonyesha kuthamini RASILIMALI ZETU....tatzo sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana Tunakaa kusubiri kuona mambo yakiharibika tu tupate sehemu ya kusemea PUMBA zetu LAKINI hatutaki kabsa kupongeza hatua zilizo chukuliwa kuzuia KUIBIWA RASILIMALI ZETU na hawa mabwana wakubwa....Tumpongeze JPM kwenye hili jamani
Hata kama BARRICK anaenda kuuza hisa zake kwa hao WACHINA hii ni kwa sababu tu MIANYA YAO YA KIJINGA KUTUPIGA SISI WATANZANIA IMESHTUKIWA angethubutu vipi kuuza HISA ZAKE kama tusingemshtukia????Hata huyo mchina atakaekuja LAZIMA tuanze nae VIZURI
Aliposhauriwa kuwa na approach nzuri katika hili aliunga mkono wanaomshauri? Hatufurahii kukosa lakini inauma kupoteza muda wetu kufuatilia vitu ambavyo ni wazi tumefanya makosa katika ufuatiliaji na hapo lazima watu wachekane maana hata wao waliwacheka na kuwakejeli walioshauri njia sahihi kutumika.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna msemo wa Kihehe unaosema "gendelage ludodi lukafu luladenyeka" ukiwa na maana kuwa ukiwa juu ya mti ama ukivuka daraja lililojengwa kwa miti jitahidi kukanyaga mti ulio mbichi kwani ukikanyaga mti ulio mkavu unaweza kuvunjika!!

CC: Pascal Mayalla
 
Paskali, hili swali inabidi LIJIBIWE kwa UFASAHA na Ng'walimu wako wa Sheria pale Mlimani. Alishiriki mazungumzo. Kwa sasa ni Bosi wa Wizara moja ambayo mambo yeke uliyasomea pale kwa Mlima..
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa kidogo, kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa. hii ni mada ya swali
Jee Wajua Kuwa Mazungumzo Yetu na Barrick Ni Mazungumzo Tuu? Mwenye Uamuzi wa Mwisho ni Acacia!, Kwa Nini Hakushirikishwa?!. Jee Tutalipwa?.

Kwanza its sad kwa sisi Watanzania kupata update ya hatima ya rasilimali zetu, ni kutoka huko huko kwa hawa mabwana wa rasilimali zetu, au wezi wetu!.

Leo nimepata muda kufuatilia hatima ya mazungumzo kati ya serikali yetu ya Tanzania na Kampuni ya Barrick kuhusu hatma ya makinikia ya Acacia yaliyozuliwa, kupitia taarifa kwenye tovuti ya Barrick, mazungumzo yameelezwa kuwa yanaendele vizuri
Barrick Gold Corporation - Update on Discussions with Government of Tanzania

Acacia nao kwenye tovuti yao nao wameeleza kitu kile kile kilichoelezwa na Barrick
Press Release Item

Jambo la kwanza la maendeleo ya mazungumzo haya, ni mazungumzo yasiyo na time frame, yaani hayana muda maalum wa kumalizika na kufikiwa makubaliano!, mazungumzo ya aina hii ni mazungumzo gani yasiyo na SMART Objectives yanaendelea tuu na yanaweza yakaendelea tuu bila mwisho?!.

Barrick wametoa statement fupi ya page 1 yenye para 3 zenye lines 15 na maneno 146 lakini wakaweka angalizo lenye page 2, para 4 zenye lines 69 na maneno 775!. One has to be good kusoma hiyo statement together with angalizo kuelewa the motive behind.

Tukija kwa Acacia, wao wametoa tuu statement ya Barrick bila kuweka angalizo la pembeni ila wao wameweka msimamo wao wazi kuwa "The Company has been supporting Barrick in its discussions with the GoT, but has not been directly involved in those discussions to date. Any proposal received by the Company in the future that might be agreed in principle between Barrick and the GoT as a result of those discussions will be subject to review by the Independent Committee of the Acacia Board of Directors". Wanaunga mkono mazungumzo hayo lakini wao sio sehemu ya mazungumzo hayo na kwanza hawajahusishwa popote hadi leo, hivyo chochote kitakachofikiwa na mazunguzo hayo kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, ni lazima kiridhiwe na kamati yao maalum!. Hii maana yake maafikiano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali yetu na Barrick sio final and conclusive, mwennye uamuzi wa mwisho ni Acacia!. Kama hali ni hii, kwa nini wanasheria wetu nguli na makini hawakuwahusisha Acacia kwenye mazungumzo haya ambao ndio the determinant ya utekelezaji wa makubaliano yoyote?. Jee mnatambua kuwa chochote ambacho serikali yetu itakubaliana na Barrick, hala Acacia wakakataa kutekeleza, hakuna kitu chochote ambacho tunaweza kuwafanya?.

Wakati mazungumzo yetu na Barrick yako kwenye dilly dallying, wenzetu Barrick wameelekeza macho na masikio yao China!,
"Barrick’s focus on China is real and deliberate.
Barrick’s focus on China is real and deliberate. In 2014, we created the position of President for Barrick China to manage our interests there. In 2015, we sold half of our ownership in the Porgera gold mine in Papua New Guinea and began joint operations with the buyer, Zijin, one of China’s big three gold miners. In 2017, we formed a 50-50 joint venture with Shandong Gold, another one of the big three, at the Veladero mine in Argentina. In addition, two of China’s largest banks—ICBC and China Construction Bank—have joined Barrick’s revolving credit facility, the first time either has forged such a relationship with a Western mining firm".

Hivyo mkisikia Barrick imeuza interest zao za Acacia kwa Wachina, naowaomba msishangae!, naamini wale "jamaa zetu" pia ni mingoni mwa watumishi wazelendo wa Acacia, hivyo wakiona ziara za makundi ya watu kutoka China huku wakiandamana na mabosi wa Barrick, waripoti haraka sana maana usikute ni ngombe wetu wa maziwa yuko mnadani!. Wazungu ambao ni watu wako very much time conscious, ukiona wanazungumza na wewe mazungumzo yasiyoisha bila kuonyesha time concern, kama wewe ni mtu unaejua kutazama mbali, ni lazima uogope!.

Swali la Msingi ni Jee Tutalipwa?.
Kwa mazungumzo ni siri, hakuna ajuaye ni nini kimekubaliwa na nini hakijakubaliwa, my honest opinion ni kuwa hatutalipwa!, hata kile kishika uchumba cha dola milioni 300, I doubt kama tutalipwa, kwa sababu the bone of contention, ni Tanzania kuibiwa kwenye makinikia kwa vile hatujui kilichomo!. Ili tujue kilichomo ni kama tuu tutayachenjua makinikia sisi wenyewe!. Sijawahi kusikia lolote kuhusu uchenjuaji wa makinikia yale, hivyo hata zile fedha za Noah zetu, zijui kama hata robo zitalipwa!.

Lets hope for the best!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
Kuna mtu aliwaita Barrick ni wezi,walipokuja Tanzania kuzungumza akawaita kuwa ni wanaume haswaa,wakajifungia ndani mmoja tukiambiwa mwanaume haswaa, mwingine hatukuambiwa ni nani haswaa!!

Matarajio ni mimba tu na kichefu chef!!
Ha ha ha
Watu mna mneno balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu si kulipwa TU...Ishu ni kwamba atleast tumeonyesha kuthamini RASILIMALI ZETU....tatzo sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana Tunakaa kusubiri kuona mambo yakiharibika tu tupate sehemu ya kusemea PUMBA zetu LAKINI hatutaki kabsa kupongeza hatua zilizo chukuliwa kuzuia KUIBIWA RASILIMALI ZETU na hawa mabwana wakubwa....Tumpongeze JPM kwenye hili jamani
Hata kama BARRICK anaenda kuuza hisa zake kwa hao WACHINA hii ni kwa sababu tu MIANYA YAO YA KIJINGA KUTUPIGA SISI WATANZANIA IMESHTUKIWA angethubutu vipi kuuza HISA ZAKE kama tusingemshtukia????Hata huyo mchina atakaekuja LAZIMA tuanze nae VIZURI
Bado upo kwenye kupiga makofi ata kama siyo. Kuwa
umesahau kuwa wabnuge wa upinzani waliposema sheria ni mbovu walizomewa na wakafukuzwa bungeni na ccm wakapitisha sheria ambazo leo mnaziona ni mbovu JPM akiwa mmoja wao
 
Ishu si kulipwa TU...Ishu ni kwamba atleast tumeonyesha kuthamini RASILIMALI ZETU....tatzo sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana Tunakaa kusubiri kuona mambo yakiharibika tu tupate sehemu ya kusemea PUMBA zetu LAKINI hatutaki kabsa kupongeza hatua zilizo chukuliwa kuzuia KUIBIWA RASILIMALI ZETU na hawa mabwana wakubwa....Tumpongeze JPM kwenye hili jamani
Hata kama BARRICK anaenda kuuza hisa zake kwa hao WACHINA hii ni kwa sababu tu MIANYA YAO YA KIJINGA KUTUPIGA SISI WATANZANIA IMESHTUKIWA angethubutu vipi kuuza HISA ZAKE kama tusingemshtukia????Hata huyo mchina atakaekuja LAZIMA tuanze nae VIZURI
We unaaandika tu, hujui madhara ya hizo ishu kwa taarifa yako akiuziwa mchina watanzania wajiandae kupoteza kazi migodi itajaa wachina hadi wapiga deki na wapishi watatoka China.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom