Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Kuna watu wanazibeza takwimu zinazotolewa mitandaoni. Takwimu ambazo nyingi kila mara zinaonyesha kuwa Tundu Lissu anamshinda Magufuli.
Binafsi ninaweza kusema kuwa hizi takwimu (polls) zinaweza kuwa credible (zenye kuaminika) zaidi nyakati hizi za sasa kuliko baadhi ya watu wanavyodhani na nitaelezea sababu za kitakwimu
Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo
1. Aina ya Sampuli (Sampuli nasibu/random sampling)
2. Uwepo wa Taarifa unaoshabihiana na takwimu hizi (Triangulation of information)
3. Jumuia ambayo takwimu hizi zinatoka(credible population from which the sample is drawn
1. Aina ya Sampuli
Tumeona kuwa takwimu zinazochukuliwa ni kutoka kwa mtu yeyote anayeamua kwa utashi wake bila kulazimishwa na yeyote na hakuna wa kumzuia yeyote kupiga kura yake katika mtandao husika. Hii tayari inaonyesha kuwa kuna "nasibu" au randomness, kwa sababu hujui mtu atakayefuata atampigia nani, Kwa kigezo hiki tayari Takwimu za mitandaoni zinapata credibility
2. Uwepo wa Takwimu zinazoshabihiana na Taarifa hizi (Triangulation)
Mwaka 2017 Taasisi ya TWAWEZA ilionyesha kuwa umaarufu wa Magufuli umeshuka kutoka asilimia zaidi ya 90 mwaka 2016 hadi asilimia 55 mwaka huo.
Pili kwa mujibu wa Taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe humu JF kuwa TISS imefanya utafiti mwaka 2018 na kuonyesha kuwa Uchaguzi ukifanyika mwaka huo basi Magufuli anashindwa.
Tatu kukosekana kwa takwimu yoyote ya mtandaoni iliyo wazi inayoonyesha Magufuli kumshinda Lissu, Isipokuwa ni Lissu tu ndo anaonekana kumshinda Magufuli hivi.
Kwa majumuisho ya sources hizi hii inaonyesha kuwa huenda ni kweli Lissu anakubalika kuliko Magufuli
3. Jumuia ya mtandaoni inaakisi Jumuia ya wapiga kura nchini (credible population)
Kwa mujibu wa NEC waliojiandikisha kupiga kura nchini ni milioni 29 na kwa mujibu wa TCRA zaidi ya Watanzania milioni 23 wana access ya mtandao (internet), Hii maana yake ni kuwa sampuli ya takwimu za mtandao inatoka kwenye population halisi ya wapiga kura nchini.
Kwa hiyo kutokana na vigezo hivyo vitatu huenda takwimu zinazotolewa mitandaoni, ambazo kila mara zinaonyesha Tundu Lissu anakubalika zaidi ya Magufuli zina ukweli ndani yake.
Lissu alikuwa sahihi kusema kuwa waachie CCM na ma TV yao na Magazeti yao ila washughulikiwe kwenye mitandao ikiwemo Whatsapp, huenda alijua ukweli huu kuwa Jamii ya Watanzania kwa sasa ni Jamii ya kidijitali zaidi (digital society)
Na huenda ndiyo maana serikali ya CCM imeanza kusumbuasumbua vijana wa mitandaoni wanaorusha maudhui ya Lissu. Hata hivyo wameshachelewa. Wananchi wanajua wapi pa kupata taarifa za Lissu wakizitaka, napo ni mtandaoni!
Hitimisho:
Huu uchaguzi siyo mwepesi kwa CCM hata kidogo, labda walete magumashi yao
Hapa chini ni Taarifa ya Shirika la habari la Reuters, ya mwaka 2018 wakiinukuu TCRA kuhusu kiwango cha watumia internet na wenye kutumia smartphones kuaccess mtandao