Je, wajua haya kuhusu Ukraine?

Je, wajua haya kuhusu Ukraine?

kyaibumba kwani na Sisi kupotea ' Kusikojulikana ' kwa ile 1.5 Trillion Tsh siyo Maendeleo? Una uhakika waliozichukua au waliogawana hawajazifanyia hayo Maendeleo?
hizo pesa zimeenda kufichwa benki za ulaya, huko ndio zinafanyiwa maendeleo na hizohizo ndio wanatujopesha kwa riba juu.
 
Maendeleo unayozungumza hapa na haya mapicha picha mbona ni vitu viwili tofaut,naona na picha za mabasi ,mabasi hata sisi tunayo naona madaraja hata hapa kwetu lipo la kigamboni, tena zuri tu
 
Sasa kama wasomi wakubwa wanajenga miundombinu kwenye mkondo wa maji bila kutumia reasoning unategemea Vijana wahitimu wapate wapi akili ya hata kukata nguzo na kuzipanga juu kama daraja ili wakati wa msimu wa MAJI mengi wasiliwe na mamba.
Inasikitisha kwa kweli
Yaani kila kitu ni dili
Unajiuliza inakuwaje kila wakati nguzo zinaanguka kwenye mbuga hivi hawana akili ya kutatua tatizo dogo hivyo, lakini ni tamaa zao tu

Uzalendo my black hairy #$$
 
Sijui sisi tuna matatizo gani.
Wakati South Africa serikali ikiongozwa na makaburu, SA ilikuwa na uchumi imara inachuana na nchi za Ulaya ikiwa na viwanda kede kede na miundombinu ikiboreshwa.
Ingekuwa kaburu bado kashika serikali nina amini SA ingekuwa mbali sana kimiundombinu na uchumi mkubwa sana.
Now Nigeria ina uchumi mkubwa kulijo SA na SA uchumi wake unashuka day after day.
Sijui kwanini uongozi wa watu weusi unashindwa atleast Botswana wamejaribu na wanaweza taratibu.
Waarabu nao wameweza tumia rasilimali yao vizuri nchi kama qatar, Kuwait, UAE, Brunei ni nchi zenye miundombinu na uchumu imara huku zikiwa top ten ya nchi zenye high level ya purchasing power.
Wakoloni weusi hawawezi leta maendeleo wamejaa ubinafsi, pia wana chuki sana na matajiri, wana roho za kimasikini sana,wanaamini ukitaka kuwatawala watu wafanye wawe masikini
 
Hivyo vinchi vina mabadiliko gani kabla ya huo uhuru na sasa? Vilishaneemeshwa na kuwezeshwa na iliyokuwa shirikisho la Urusi, hawajajenga lolote jipya.
Unaweza kutueleza kwa undani ni kivipi wapo juu nje ya Urusi?
 
Ukimtukana mwanao au mtoto kila siku kuwa ni mjinga hawezi kitu na kila anachojaribu unakiponda na kumdhalilisha
Haya ndio matokeo yake
Waafrika tumeathirika kisaikologia ingawa sio wote.
Imefika mahali hata kufanya jambo tunashindwa.
Vijana waliohitimu wapo lakini huwezi kuona wametengeneza hata daraja fupi sehemu ambayo kina mama wanaliwa na mamba kila kukicha
Tunaweza ila akili haikubali
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nakumark, siku nikipata balance nitakununulia vocha
 
Unaweza kutueleza kwa undani ni kivipi wapo juu nje ya Urusi?
Mimi sio mwanzisha uzi na sikubaliani na dhana kuwa mara baada ya kuwa nje ya shirikisho basi wameendelea sana kulinganisha na miaka 50+ ya Tz.
 
Hili neno ,,kupata Uhuru” naona labda huwa hamlielewi na mnalitumia vibaya, kwa mfano Wazungu wa AK leo wana movement ya kujitenga na AK na wanataka nchi yao eneo la Western Cape ( Cape Town) liwe nchi yao, tuseme wafanikiwe na wajitenge mwaka huu 2018, watasema wamepata Uhuru mwaka 2018 na watakuwa wanasherehekea Uhuru wao kila mwaka, sasa utasema Western Cape imepata Uhuru mwaka 1 tu lkn imeendelea klk TZ?

Lei hii Capetown imeshaendelea kama Mji wowote tu wa first world!
Bado si kisingizio cha umasikini wa taifa lako
 
Kwao uhuru wa bendera ulitanguliwa na uhuru wa fikira. Kwetu sisi ilikuwa kinyume na hata sasa fikra zetu hazijawa huru na ndo maana hatujui tuendako, na hilo linatufanya kutumia njia yoyote, ko' kila ajae anakuja na njia yake.
Ndo maana kinywa kinasema viwanda akili inawaza ndege.
Hhaaaaaa, dah bonge la tafakuli…. Mkuu, Ongezea hii, wabunge na serikali wanaimba kila kuchwao kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Watanzania ajabu ni kuwa kilimo hakionekani kuendelezwa kivitendo ila vinywani tu.
 
Cha ajabu hapa kipi sasa? Nchi zilikua tayari na maendeleo zikiwa ndani ya Soviet ambayo ilikua na uchumi mkubwa wa pili duniani baada ya USA.. 1992 ndo zimejiondoa umoja wa Soviet ila haimanishi hizo nchi ndo zimeanzishwa mwaka huo zilikuwepo kabla..
Hata leo jimbo la California lina uchumi mkubwa kuliko Canada, Wingereza, Italia, Brazil na nyingine zote isipokua China, Japan na Ujeruman tu so leo California ikipata Uhuru kutoka USA haitashangaza kua nchi hii mpya inazizidi uchumi nchi kongwe na kubwa za G8 na G20
Acheni visingizio, kama wangelala wangerudi nyuma, mbona ninyi mmeachiwa vitu vingi hata Ikulu lakini mnapiga marktime?
 
Kwao uhuru wa bendera ulitanguliwa na uhuru wa fikira. Kwetu sisi ilikuwa kinyume na hata sasa fikra zetu hazijawa huru na ndo maana hatujui tuendako, na hilo linatufanya kutumia njia yoyote, ko' kila ajae anakuja na njia yake.
Ndo maana kinywa kinasema viwanda akili inawaza ndege.
Post of the year!

Platinum!!

Bingo!!!!
 
Kwa sababu South Africa na Kenya hakuna CCM... right?
Sababu kubwa nayoijua ni kwamba wale wakoloni walikaa sana maeneo haya kiasi kwamba walifikiria kwamba wangedumu katika maeneo hayo ikapelekea kuweka investments nyingi kama viwanda, infrastructures, social services za kutosha ..
Ila vile vile kama Kenya zilikuwepo plantations na sababu nyinginezo
Btw hata huko penye kuna maendeleo kuna CCM zao
 
Sababu kubwa nayoijua ni kwamba wale wakoloni walikaa sana maeneo haya kiasi kwamba walifikiria kwamba wangedumu katika maeneo hayo ikapelekea kuweka investments nyingi kama viwanda, infrastructures, social services za kutosha ..
Ila vile vile kama Kenya zilikuwepo plantations na sababu nyinginezo
Btw hata huko penye kuna maendeleo kuna CCM zao
Ila Kenya ilipata uhuru 1962 na sisi 1961. Tafauti ya mwaka mmoja tu lakini wametucha mbali..
 
Sijaona maendeleo yeyote waliotuzidi kwenye hizo picha, labda ulete data za GDP
 
Hhaaaaaa, dah bonge la tafakuli…. Mkuu, Ongezea hii, wabunge na serikali wanaimba kila kuchwao kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Watanzania ajabu ni kuwa kilimo hakionekani kuendelezwa kivitendo ila vinywani tu.
Unataka viwanda bila kuboresha mazingira ya mkulima na kilimo kwa ujumla ili kupata malighafi.
Safari yetu ni ndefu mno.
 
Back
Top Bottom