Je, waijua Historia ya Gwiji wa Soka Ronaldinho Gaucho?

Allein mushi

Member
Dec 14, 2017
9
11
Gaucho.gif

Mwaka 1983 Brazil waliingia katika msiba mzito kisoka pale walipompoteza gwiji wao Manuel Francisco dos Santos almaarufu kwa jina la Garincha. Garincha ni moja ya kizazi cha dhahabu cha soka la Brazil kilichoibuka mwishoni mwa miaka ya 1950s akiingoza vyema nchi hiyo kunyakua ubingwa wa dunia mwaka 1962 nchini Chile pasipo uwepo wa Pele aliyeumia hatua za makundi.

Hakika ulikuwa msiba mzito kutokana na kumbukumbu yake kisoka, uwezo uwanjani, ucheshi wake na uzalendo kwa taifa lake lakini Mungu bado aliendelea kusimama kisoka na taifa hilo ambalo kwa hakika mchezo huu pendwa zaidi duniani una kitanda chake pale.

Wakati wakiwa msibani; familia moja ya maisha ya wastani ya bi Dona Miguellina na bwana Joeao Moreira walikuwa katika malezi ya mtoto wa miaka mitatu aliyezaliwa March 21, 1980. Huyu si mwingine bali ni Ronaldo de Assis Moreira au wengi wanamjua kwa jina la Ronaldinho Gaucho.

Wachambuzi wengi wa soka na wadau mbalimbali wa soka waliobahatika kumuona Garincha au kutazama video zake, wanamfananisha sana Gaucho na Garincha katika aina zao za uchezaji na hivyo kukiri Mungu kumrudisha Garincha katika umbo jingine.

Gaucho aliyezaliwa katika jiji la Porto Alegre jiji la kumi kwa ukubwa nchini Brazil, anahesabika mmoja wa wachezaji wa kibrazil aliyeutambulisha vyema mpira wa Brazil Ulaya, Samba.

Maisha ya soka ya gwiji huyu yanaanzia katika klabu ya Gremio nchini Brazil aliyopata kuichezea mechi 52 na kufunga magoli 21. Hii ni moja ya klabu kongwe nchini Brazil na tajiri zaidi kwa ukanda wote wa Latin America iliyoanzishwa mwaka 1903 na wafanyabiashara wa kiingereza. Ni klabu ambayo ndio iliyomlea na kumkuza kisoka Gaucho kabla ya kutimkia Ulaya. Klabu ya mtaani kwao katika jiji la Pelegre.

Ronaldinho alijiunga rasmi na klabu hiyo mwaka 1998 baada ya kudumu hapo kwa miaka kadhaa katika shule ya kukuzia vipaji na mwaka 2001 aliingia kandarasi ya miaka mitatu na Paris Saint Germane (PSG) jijini Paris nchini Ufaransa.
Uwezo mkubwa kisoka alianza kuonesha akiwa na timu ya soka ya vijana ya Brazil chini ya miaka 17 iliyoshiriki Olympic nchini Misri na kuibuka mabingwa pia kujumuishwa katika kikosi cha timu mwaka 199, ndio muda uliomfanya wababe wengi wa soka Ulaya kumtolea macho lakini walikuwa PSG walioweza kuwashawishi Gremio kuwauzia ' lulu ' hiyo.

Gaucho ana mengi ya kukubwa kisoka kama ilivyo kwa wakali wengi wa Brazil hususani kwa wapenzi wa FC Barcelona, klabu ambayo aliichezea kwa muda mrefu kabla ya mwanga wake kisoka kuzimika ghafla nakutoka kwenye njia ya wachezaji tegemeo huku dunia ikijiuliza kulikoni?

Akiwa Barcelona aliyojiunga nayo mwaka 2003 na kuichezea kwa miaka mitano mpaka mwaka 2008, aliweza kuichezea mechi 145 na kufunga magoli 70!. Klabu iliyomwezesha kushinda tuzo zifuatazo:

La Liga: 2004–05, 2005–06
Supercopa de España: 2005, 2006
UEFA Champions League: 2005–06

Gaucho msimu wa pili tu akiwa na FC Barcelona aliweza kuwafunga mara mbili mfululizo Real Madrid katika mechi yao maarufu ya El classico. Alikuwa mfungaji pekee wa mechi zote mbili kitu ambacho kilimfanya kupokea heshima ya pekee kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid inayojulikana kama ' Standing Ovation ' . Ni kitendo cha mashabiki wa timu pinzani kusimama majukwaani na kumpigia makofi mchezaji wa timu pinzani aliyeweza kuwafunga mara mbili mfululizo . Kabla ya Gaucho , Diego Maradona alifanya hivyo pia mwaka 1983!

Tuzo binafsi za gwiji huyu ni hizi hapa:
FIFA Confederations Cup Golden Ball: 1999
FIFA Confederations Cup Golden Shoe: 1999
Bola de Prata: 2000, 2011, 2012
FIFA World Cup All-Star Team: 2002
Onze de Bronze: 2002, 2004
Ligue 1 Goal of The Year: 2003
La Liga Best Foreign Player: 2003–04, 2005–06
Trofeo EFE: 2003–04
FIFA World Player of the Year: 2004, 2005
UEFA Team of the Year: 2004, 2005, 2006
World Soccer Magazine World Player of The Year: 2004, 2005
UEFA Club Forward of the Year: 2004–05
FIFA Confederations Cup Bronze Ball: 2005
Ballon d'Or: 2005
Onze d'Or: 2005
FIFPro World Player of the Year: 2005, 2006
FIFPro World XI: 2005, 2006, 2007
UEFA Club Footballer of the Year: 2005–06
La Liga top assist provider: 2005–06
UEFA Champions League top assist provider: 2005–06
FIFA Club World Cup Bronze Ball: 2006
Onze d'Argent: 2006
FIFA World Player of the Year Bronze award: 2006
Golden Foot: 2009
Serie A top assist provider: 2009–10
Campeonato Brasileiro Série A Team of the Year: 2011, 2012
Campeonato Brasileiro Série A Best Fan's Player: 2012
Campeonato Brasileiro Série A top assist provider: 2012
Bola de Ouro: 2012
Copa Libertadores top assist provider: 2012, 2013
South American Footballer of the Year: 2013
FIFA Club World Cup Golden Ball: 2013
UEFA Ultimate Team of the Year
Brazilian Football Museum Hall of Fame
A.C. Milan Hall of Fame

Licha ya mafanikio makubwa aliyoyapata gwiji huyu kisoka ambaye kwa sasa ni mwimba muziki , mcheza filamu na balozi wa kudumu wa Barcelona, wengi wanamuona kama aliondoka ghafla kwenye kiwango chake cha soka tofauti na wenzake waliomtangulia jinsi walivyostaafu. Hakuachana na soka katika ile heshima aliyoijenga kama ilivyokuwa kwa Ronaldo de Lima , Zizzou na wengineo . Ni kama mpira ulimkataa mwishoni.
*********************************************
Garincha na Gaucho nje ya uwanja maisha yako kama yalifanana tu, isipokua Garincha yeye alizidisha ulevi wa kupindukia na kupenda wanawake, stori ya kuhuzunisha ni pale alipopata ajali kwa kuendesha gari kwa mwendokasi huku akiwa amelewa, ajali iliyosababisha kifo cha mama mkwe wake, lakini pamoja na yote hayo Wabrazil walimhusudu sana na ndo maana kwenye kaburi lake yaliandikwa maneno, "Hapa amelala mtu ambaye alikua furaha ya wengi"
 
Acha Plagiarism, kama ndo unaanza kuandika hizi makala jaribu kuwa wewe kwanza hata kama utakosea baadae utakuwa bora tu.
Asilimia kubwa umecopy toka katika makala ya Edo Kumwembe, wewe ulichoongeza kidogo ni hizo takwimu tu. Hii haitokujenga na haitokukuza kwenye safari yako ya uandishi.
 
Acha Plagiarism, kama ndo unaanza kuandika hizi makala jaribu kuwa wewe kwanza hata kama utakosea baadae utakuwa bora tu.
Asilimia kubwa umecopy toka katika makala ya Edo Kumwembe, wewe ulichoongeza kidogo ni hizo takwimu tu. Hii haitokujenga na haitokukuza kwenye safari yako ya uandishi.

Utajisikiaje ukigundua ya kuwa mwandishi huyu ndiye Edo Kumwembe.?
 
Kuna watu wana vihele hele ndugu!! Hata kama ameicopy sehemu si mbaya kutushirikisha na sisi,hatuna muda wa kumfatilia huyo eddo kumwembe.
Huyo kajitambulisha kama mwandishi kule kwenye jukwaa la utambulisho, kama mwandishi sitoacha afanye kitu ambacho hata akiwa shule alikatazwa 'Plagiarism'. Nitamkumbusha akirudia tena, hii ni kwajili yake na uhai wa tasnia.

Kwenu kwenye tasnia nyingine labda kucopy si mbaya, lakini huku alikojipambanua ni dhambi sharti kukemewa. Vinginevyo acknowledge kazi ya mwenzake huo ndo uungwana na utaratibu.
 
Garincha alikuwa kama Hana akili timamu..
Wameshinda kombe la dunia ..wenzie wanafurahia yeye kanuna anajua kuna mechi ya marudiano ..hajui michuano imeisha na Brazil bingwa..


Ronaldinho hapendi mazoezi..mpira kama starehe kwake..na mizaha mingi sana..
Kuna kipindi alikuwa na kitambi Barcelona..

Hana discipline ya European players..
Wachezaji wote wa Brazil wako hivyo..
Starehe hadi wanaenda mazoezini wamelewa..
Kipaji chake ni zaidi ya Cristiano Ronaldo..lakini Cristiano kawazidi discipline
 
Siku nilipo angalia huyu mtu ndiyo siku nilianza kuupenda mpira na timu yangu ilawa barcelona , lakini akiwepo gaucho.. asipo cheza nazima tv..

Milimpenda kwa jinsi alivyo kua anafurahia soka na akiwa uwanjani saa zote anataka kufanya vitu vipya kwa ajili ya kuwafuragisha mashabiki.


Sitasahau goli alilo wafunga chelsea kwa kuwaduwaza.
 
Back
Top Bottom