Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Inarudi palepale kuwa kama Magufuli asingetokea mwaka 2015 kama Rais, tusingekuwa hapa tulipofika. Tuko hapa ni kwa sababu ya Magufuli.

Angalia miaka 10 ya BWM na JK hakukuwa na ushenzi huu. Lakini Magufuli akaanza kuvunja katiba na kukandamiza demokrasia, mkamchekea ndipo baada ya kufa na Samia kuja, naye anajaribu kuacha ambalo halimsaidii na kuchukua linalomsaidia
Nakubaliana nawe mia kwa mia. Huyu jamaa alitengezea majitu kama Samuya, Bashiti, Bashungwa, Kabundi, Mkumbo madelu na majambazi mengine mengi. Alianzisha utawala wa kifalme na kifala uliojaa ukatili, ushamba, na upofu hadi tunajikuta hapa tulipo. Heri aliondoka mapema. Hata kama alijenga vitu, alibomoa utu na uwajibikaji na kuumba umungumtu.
 
Maridhiano yapi?

Ya kuua watu na kuwahonga wasimkosoe?

Kwahiyo hapa umekubali Samia na Magufuli wote playbook yao ni moja?

Kwanini unajifunga goli kirahisi hivi.
Ngamia anachinjwa kwa upande alioelekea, siyo lazima umelekeze kibra. Ukitaka kumuelekeza kibra humchinji.

Walivyokuja Tundu na Heche ndivyo walivyokabiliwa
 
Sasa Rais alitengeneza mazingira ya maridhiano na tukaona waliokimbia nchi wakati wa Magufuli wakirudi nchini.

Lakini wakaanza dharau nankuponda kwa kejeli hao hao aliowarudisha kutoka Belgium na Canada. Ndiyo naye kaonyesha kuwa ameshika mpini. Hata mimi ujinga wa Tundu nisingeuvumilia
Magufuli VS Samia = wote ni wakatili.

Magufuli vs Samia= wote wameua. Ila Samia ameua zaidi.

Magufuli vs Samia= magufuli ni Bora kwenye utendaji kuliko Samia.

Magufuli vs Samia= magufuli ni Bora kwenye kufanya vitu vitokee kulinganisha na Samia.

Magufuli vs Samia= Rushwa na ufisadi umekuwa mkubwa zaidi kwa Samia kulinganisha na mtangulizi wake magufuli.

Sasa mkuu,

Mimi na wewe Huwa tunatofautiana hapa tu;

Kwa nini Huwa unachora mstari linapokuja swala la Samia,wakati kwa mambo ya hovyo ambayo unamponda magufuli kwa nguvu zako zote humu ndani,huyo Samia ni kama anafanya mara mbili yake na Yale yaliyo mazuri ya magufuli huyu Samia anastruggle kufikia ile level ya Magufuli?

Double standards?
 
Hayo ni maoni yako tu na hivyo vipimo ulivyoweka vya viwango vya rushwa ni arbitrary.

Bottomline ni kwamba aliyevuruga misingi ya demokrasia, utawala bora na kuanzisha utekaji na mauaji ni Magufuli
 
Hayo ni maoni yako tu na hivyo vipimo ulivyoweka vya viwango vya rushwa ni arbitrary.

Bottomline bi kwamba aliyevuruga misingi ya demokrasia, utawala bora na kuanzisha utekaji na mauaji ni Magufuli
Wewe vyeti feki una matatizo yako naona,sasa kama Magu alianzisha hayo mambo ya utekaji na mauaji, sasa iweje huyo mtakatifu Samia nae akubali kuyaendeleza?
 
View attachment 1734652
Picha: Hayati Rais Magufuli enzi uhai wake

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti (Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss, kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo.

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje, kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu, S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Haijawahi kutokea Rais bora kama huyu Tanzania na Afrika nzima na hatatokea kwa miaka mingine 50 hivi
 
Wewe vyeti feki una matatizo yako naona,sasa kama Magu alianzisha hayo mambo ya utekaji na mauaji, sasa iweje huyo mtakatifu Samia nae akubali kuyaendeleza?
Vyeti FEKI siyo issue ya kunifanya nisiseme ninachoami japo mimi siyo cheti feki. Kwa taarifa yako Magufuli pia alikuwa na PhD Feki
 
Hayo ni maoni yako tu na hivyo vipimo ulivyoweka vya viwango vya rushwa ni arbitrary.

Bottomline bi kwamba aliyevuruga misingi ya demokrasia, utawala bora na kuanzisha utekaji na mauaji ni Magufuli
Wala bado haujanijibu swali langu.

Nimekuekea maelezo ya magufuli vs Samia katika context yako ya ""CHUKI DHIDI YA UTAWALA".

Mwishoni Nimekuuliza;

Kama viwango vya chuki dhidi ya magufuli viko juu,katika context hiyo hiyo Samia 'anafit in' Tena viatu vile vile vya magufuli,Samia unayemtetea anavivaa na naweza kusema vinambana ana mguu mkubwa.

Sasa basi... Kwanini chuki yako imeegemea upande mmoja na siyo kwa wote wawili?

Nini kinakufanya umchukie magufuli na umependeza Samia?

Kama magufuli aliua,Samia ameua zaidi kuliko Marais wote hapa nchini,why unamchukia magufuli kwa kuua na kumtetea Samia kwa mauaji yaleyale,Tena yeye zaidi?

Kama kuteka,Samia pia ameteka sana na anazidi kuteka maana muda anao zaidi,why unamchukia magufuli kwa utekaji na kumtetea Samia kwa swala hilohilo?

Na kukujibu kwenye kichaka chako unachojifichia cha "kwa sababu magufuli ni mwasisi wa kuua na kuteka" hiyo siyo kweli kabisa na nakujibu kaka ifuatavyo;

Mauaji na utekaji vilikuwepo katika awamu zote,ila nakubali ukiniambia kuwa takika regime ya magufuli,graph 📉 ilipanda.. ila habari mbaya zaidi ni kuwa utawala wa huyu unayemtetea graph ipo juu si tu kuliko Magufuli,bali pia kuliko Rais yoyote aliyewahi kuongoza hapa nchini. Kwa hiyo hapa tunakubaliana kuwa magufuli anatetewa katika hili kwa sababu huyo samia aliyempokea kijiti amepuyanga mara elfu ya huyo magufuli unayemchukia. Ameua zaidi na ameteka zaidi na muda anao wa kuendelea kuvunja rekodi zake mwenyewe...Samia muuaji,Samia mtekaji,Samia mfiraji.

Ndiyo nikakuuliza...double standards? Kwa nini unamchukia mmoja na kumpenda mmoja? Kwa nini usiwachukie wote au kuwapenda wote.

Au una lingine la sirini limejificha kwa magufuli ambalo hutaki kul!sema hapa?
 
Wala bado haujanijibu swali langu.

Nimekuekea maelezo ya magufuli vs Samia katika context yako ya ""CHUKI DHIDI YA UTAWALA".

Mwishoni Nimekuuliza;

Kama viwango vya chuki dhidi ya magufuli viko juu,katika context hiyo hiyo Samia 'anafit in' Tena viatu vile vile vya magufuli,Samia unayemtetea anavivaa na naweza kusema vinambana ana mguu mkubwa.

Sasa basi... Kwanini chuki yako imeegemea upande mmoja na siyo kwa wote wawili?

Nini kinakufanya umchukie magufuli na umependeza Samia?

Kama magufuli aliua,Samia ameua zaidi kuliko Marais wote hapa nchini,why unamchukia magufuli kwa kuua na kumtetea Samia kwa mauaji yaleyale,Tena yeye zaidi?

Kama kuteka,Samia pia ameteka sana na anazidi kuteka maana muda anao zaidi,why unamchukia magufuli kwa utekaji na kumtetea Samia kwa swala hilohilo?

Na kukujibu kwenye kichaka chako unachojifichia cha "kwa sababu magufuli ni mwasisi wa kuua na kuteka" hiyo siyo kweli kabisa na nakujibu kaka ifuatavyo;

Mauaji na utekaji vilikuwepo katika awamu zote,ila nakubali ukiniambia kuwa takika regime ya magufuli,graph 📉 ilipanda.. ila habari mbaya zaidi ni kuwa utawala wa huyu unayemtetea graph ipo juu si tu kuliko Magufuli,bali pia kuliko Rais yoyote aliyewahi kuongoza hapa nchini. Kwa hiyo hapa tunakubaliana kuwa magufuli anatetewa katika hili kwa sababu huyu aloyemshikia kijiti amepuyanga mara elfu ya huyo unayemchukia. Ameua zaidi na ameteka zaidi na muda anao wa kuendelea kuvunja rekodi zake mwenyewe...Samia muuaji,Samia mtekaji,Samia mfiraji.

Ndiyo nikakuuliza...double standards? Kwa nini unamchukia mmoja na kumpenda mmoja? Kwa nini usiwachukie wote au kuwapenda wote.

Au una lingine la sirini limejificha kwa magufuli ambalo hutaki kul!sema hapa?
Siwezi kumchukia Samia kwa vile yeye amerithi mfumo mbovu ulioasisiwa na Magufuli. Alifanya yake yakutosha mengi tu kupunguza lakini aka face resistance kutoka ndani ya chama chake na upinzani pia.
 
Siwezi kumchukia Samia kwa vile yeye amerithi mfumo mbovu ulioasisiwa na Magufuli. Alifanya yake yakutosha mengi tu kupunguza lakini aka face resistance kutoka ndani ya chama chake na upinzani pia.
"Siwezi kumchukia mtoto mwizi kwa sababu yeye amerithi wizi kutoka kwa baba yake aliyeasisi."

Mkuu,tatizo lako ni kubwa sana. Kubwa kuliko nilivyodhani.
 
1:Magufuli mvunjifu wa kanuni, sheria na taratibu katika nchi. Hususan Demokrasia l, ubabe usio na tija katika uongozi na kutoa lugha chafu zisizo na staha.
2: muasisi wa uchawa, Kuchagua watu wenye uwezo mdogo katika utumishi Ili wam please yeye.
3: Kutumia nguvu kubwa kununua wapinzani na kurudia uchaguzi, chini ya kibaraka wake Polepole.
4: muasisi wa kuvuruga uchaguzi, Kufanya uchaguzi usionekane na maana.
5: Ubadhirifu uliokithiri, Prof. Assad aliibua kashfa ya ubadhiri wa 1.5 trillions matokeo yake akatumbuliwa.

Wa TZ tumetawaliwa na unafiki, lakini ukweli ni kwamba hizi changamoto nyingi tulizonazo katika awamu muasisi wake ni JPM.
 
Back
Top Bottom