Wakuu,
Nilisema nitakuwa naandika taratibu juu ya yale niliyoyaona kwenye safari yangu ya TZ siku za karibuni.
Kule Kyela niliambiwa na kugundua kwamba ni tatizo, mkakati wa kutumia wanachama wa vyama vya upinzani kwenye kura za maoni za CCM hapo mwakani.
Ni kwamba kuna wagombea wa CCM wanaoungwa mkono na wanachama wa upinzani kwasababu zozote zile, wanagawa kadi kwa hao wanachama wa upinzani ili wawasaidie kwenye kura za maoni 2010.
Hii ni kama ile ya kule USA ambapo Republicans walikuwa pale mwanzoni wanampigia kura Obama kwa makusudi ili mama Clinton asichaguliwe.
Sijui CCM watafanya nini kuondoa hili tatizo; ila kwa mawazo yangu nimeona kama litakuwa tatizo kwenye baadhi ya majimbo.
Kwa Kyela imeamuliwa kwamba katibu kata atahakiki kila kadi ya mwanachama ndipo watapatikana wanachama hai. Lakini je katibu kata akiwa na mapenzi na mgombea anayeungwa mkono na mwanachama Mamluki, kweli ataweza kusema wewe huna sifa? Pili watajuaje kwamba huyo bado ana mapenzi na upinzani na wala sio CCM?
Kwa wale mnaotaka kugombea, anzeni kutafuta jawabu la tatizo hili. huenda jimbo kama Ubungo ambalo lina wapinzani wengi, wakaamua kumuunga mkono mtu dhaifu ili iwe rahisi kwa wao kumshinda kwenye uchaguzi mkuu.
Je CCM wafanye nini kuepuka tatizo hili?