Buhaya Empire
Senior Member
- Aug 3, 2016
- 116
- 299
Moja kati ya mambo ambayo yatakuchanganya sana akili yako ni kudhani kwamba unaweza kumbadilisha mtu fulani tabia ili awe kama unavotaka wewe.
Nikupe taarifa tu rafiki kwamba jambo hilo linauwezekano mdogo unaokaribiana na kushindikana.
Na ikiwa utachagua kuamini kwamba haiwezekani kumbadilisha mtu tabia ili kuwa kama unavotaka wewe, niseme tu kwamba utakuwa umefanya uchaguzi wa busara sana.
Kuna watu wamekuwa wakijidanganya kwamba watawabadilisha marafiki, ndugu, au mpenzi eti ili wawe kama yeye binafsi anavotaka, rafiki unapoteza muda.
Watu wengi wamejikuta katika nyakati ngumu, kwa vipindi tofauti, na wengine hata sasa ninavyoandika hapa wanajitoa uhai kwa sababu tu waliamini kwamba wamewabadilisha watu wao wanaowapenda sana na kufikiri kwamba wataishi maisha ya raha mustarehe ndani ya dunia waliojitengenezea, Hilo ni jambo la kuchekesha na kusikitisha kwa wakati mmoja.
Kwa uzoefu wangu, na juhudi katika kujifunza kwa umakini juu ya tabia za watu wanaonizunguka, marafiki, wapenzi, na kusoma, nimebaini jambo moja zuri kuhusu mabadiliko ya mtu ya tabia.
Jambo la awali kabla ya kufikiri mara mbili unapaswa pasina shaka kujua kwamba mabadiliko ya mtu mwingine yanatoka ndani yake yeye mwenyewe. Na mtu anabadilika baada ya kukubali yeye pekeake bila shuruti kwamba inampasa kubadilika.
Lakini mpaka mtu kufikia kutaka kubadilika. Je kiu hii ya mabadiliko inaanzaje?
Nikutanabaishe tu kwamba si kwa viboko wala maneno makali. Imethibitika kwamba kwa njia hizo haiwezekani kumbadilisha mtu mzima ili kuwa bora bali kuwa mbaya zaidi.
Kuamini kwamba unaweza kuwabadilisha watu wengine ni mawazo ya gizani na ya kishetani, nilichogundua katika maandiko pia ni kwamba Mfalme wa Nuru (YHWH) hakuwahi kuthubutu kuwabadilisha watu akili zao ili wamtumikie yeye bali aliwataka wabadilike wao wenyewe ili wamgeukie.
Jambo la busara sana linaloweza si tu kukupa furaha bali pia kukufanya uishi vizuri na kuvumiliana na watu ni kujua kwamba msaada pekee unaoweza kuwapa watu katika eneo hili ni KUCHOCHEA au KUANZISHA kiu ya mabadiliko yao binafsi na baada ya hapo ukae pembeni, mabadiliko yao kamili ni jukumu lao na si lako
Moja kati ya vichocheo ambavyo dunia inavitumia sana kuanzisha kiu ya mabadiliko ndani ya watu ni KUWAVUTIA watu katika mambo fulani, kuonesha upande mmoja wa faida za mambo fulani, na kuwa wema sana kwa watu katika mambo fulani.
Jukumu la kuamua kubadilika linabaki kuwa lako, na katika hilo hakuna wa kumlaumu.
Ni ukweli kwamba mtu anauwezekano mkubwa wa kubadilika na kuwa bora zaidi au mbaya zaidi kwa sababu ya watu waliomzunguka, ni sahihi kabisa. Lakini unahitaji fikra safi kugundua kwamba mabadiliko ya mtu huyu yanatokana na yeye binafsi kuvutiwa na tabia za waliomzungua na kuchagua yeye binafsi kubadilika
Katika hilo asitokee yeyote na kusema kambadilisha mtu huyo, HAPANA, mabadiliko kamili ni hatua ya mwisho anayoipiga mtu binafsi.
Leo hii tuna mapadre, wachungaji na masheikh wengi wa hovyo ambao watu wanawaamini na kudhani eti vitabu vimewaweka katika njia nyoofu, lakini kwa isivyo bahati vitabu havijafanikiwa kuwabadili kwakuwa wao binafsi bado hawapo tayari kubadilika
Ishi humo.