Lembeli: Watanzania waache tabia ya kumsifia mtu akishafariki dunia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,828
Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli amewaasa Watanzania kuacha tabia ya kumsifia mtu baada ya kufariki dunia wakati akiwa hai husemwa kwa ubaya.

Lembeli amesema tabia hiyo inazidi kuchonganisha Taifa.

Akimzungumzia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema kuna kipindi watu walimsema sana huku akikiri hata yeye amewahi kumsema lakini baadaye walipokutana upinzani akagundua alikuwa mtu mwenye moyo safi, anayependa watu na asiyependa umasikini.

Lembeli amesema ndiyo maana umati mkubwa umejitokeza leo kumuaga kwa kuwa wanampenda na walikuwa wanamkubali.
 
Ni kweli walimsema sana. Ila mtu akishafariki mambo yake yote yanabakia kati yake na Mungu wake au cho chote anachokiamini. Ndiyo maana ni bora kusema mema yake tu na kuyaacha mabaya yake yote kati yake na Mungu wake 🙏🏿

IMG-20240212-WA0137.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom