Je unataka kujua siku ya kifo chako?

Je unataka kujua siku ya kifo chako?

mnaonekana ni waoga sana wa kujua siku zenu za kufa. msiogope ni kitu cha kawaida sana... mnachotakiwa kufanya andikeni kama nilivyoelezea hapo juu ili niweze kuwaambia.
Wewe tapeli la kawaida!
Wana JF muwe macho inaelekea huyu jamaa anayo access kwenye data bank fulani na anatafuta password kuaccess siri zenu au account zenu.
Ukitoa tu information hiyo katazame akaunti yako kama huja pigwa!!!
 
Wewe tapeli la kawaida!
Wana JF muwe macho inaelekea huyu jamaa anayo access kwenye data bank fulani na anatafuta password kuaccess siri zenu au account zenu.
Ukitoa tu information hiyo katazame akaunti yako kama huja pigwa!!!

ha ha ha!! we mkuu umeenda mbali sana! hujajua dhamira yangu bado kwa hiyo usinihukumu!!!
 
wakuu, kama kweli unataka kufahamu siku ya kifo chako yani tarehe, mwezi na mwaka. unachotakiwa kufanya ni kutaja majina yako yote matatu pamoja na tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa then mimi nitakwambia siku yako ya kufa.

mfano: michael james kintonto. 23/05/1982

NOTE: kama hutaki hujalazimishwa waache wale wanaotaka kujua siku zao za kufa wasaidiwe.

Asanteni

Kumbe kumwambia mtu siku atakayo kufa ni kumsaidia!?
Ngoja wenye hofu na mashaka waje
 
W.p.slaa
13.05.1935
Dah, ma nyinyiemu mpo desparate balaa! Yaani hadi unatamani kujua tarehe ya kufa jamaa? Aisee nimeamini siku hizi hamlali usingizi kwa sababu ya kuwa hai huyu jamaa! Poleni make jamaa alianza na Mungu na atamalizia na Mungu!
 
Jina:Bunge.Baba:LA.Babu:katiba.mm naitwa BUNGE LA KATIBA.Haya mkuu nitabirie
 
naambiwa hakuna mtu mwenye jina kama hili. jaribu kuwa mkweli mkuu.

Kweli JF kuna watu na vitu vya ajabu! Haya mnaoyafta wake/waume mnaona hii kitu? Wewe sina uhakika Kama ni bin Adam au bin.....duh! Inatishaaaa!
 
Hakuna sayansi iliyofanikiwa kufahamu kiumbe cha Mungu anakufa lini...usilete uzushi hapa.
 
Nenda face book huko hamna haja ya watu kutaja majina yao na miaka kwani kila kitu kipo katika profile zao. Huko watabirie siku zao za kufa ikiwa wanataka au hawataki.
Unaona je ukiomba kazi pale Muhimbili ili kila mgonjwa anapoletwa uweze kutoa siku yake ya kufa kuepoka kupoteza pesa na resources nyingine kwa mgonjwa aliyefikia ukingoni?
Kama attorney Isp. General amekutuma Jf kifichua maruhani mwambie umebugi men,.
.
 
mpaka sasa hakuna hata mtu ambaye amefanya kama niliyoagiza hapo juu!! hii inaonesha kuwa hakuna mtu ambaye yupo tayari kujua siku yake ya kufa( siku ambayo mtu atakutana na Mungu).

licha ya kuwa kila mtu anafahamu kuwa maisha ni mafupi na ipo siku ambayo atakufa(utakutana na Mungu wako)lakini binadamu hatuachi yale ambayo tumekatazwa katika vitabu vyetu ambavyo tunaamini( kwa wale wenye kuamini). kila siku watu wanazini, wanaiba, wanadhulumu, wanaroga, wanaua na mambo mengine mabaya. wakuu hizi pumzi tunazozivuta zisitudanganye tukawa wenye kujisahau hapa ulimwenguni! Mungu yupo na ipo siku utakutana nae. Tujitahidi kuishi kama tulivyoagizwa kwenye vitabu vyetu tunavyoviamini.

Kwa ufupi hakuna mtu ambaye anaweza kujua siku yake ya kufa na ndio maana tunatakiwa kila wakati tujiandae kwa hilo kwa kufanya yake ambayo ni mema.

Mbarikiwe na jumapili njema wote.
 
Back
Top Bottom