Je, unakijua kikosi cha KM?

Je, unakijua kikosi cha KM?

Uwepo wa kikosi hicho ni wa kupoteza nguvu kazi na fedha za mafunzo maana tokea nipate akili sijawahi kusikia kuna gereza wafungwa wameaasi..Mambo hayo yapo sana South na Latin America
kwa hiyo ulitaka wakisha asi ndo kikosi kama hicho ndo kiundwe?
 
Hao hawana KM. Yaani eti Juzi kuna kibaka katoroka gerezani na helicopter Ufaransa....! Ndiyo maana Trump anawatishia tishia Europe, wepesi sana.
hahaha ile michezo tu ...Yule aliyetoroka itakuwa ametoroshwa na wakubwa ""..
 
ili wawe na hasira zaidi pale wanapokutana na binadamu .. ni kama mbwa ambaye amekula kidogo si sana.. anakuwa mkali na hasira ukichanganya na njaa.... basi ni kama wamevuta bhangi tu.
Sasa kwanini wanalipwa mshara mdogo kwa kazi ngumu wanayofanya????


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
ili wawe na hasira zaidi pale wanapokutana na binadamu .. ni kama mbwa ambaye amekula kidogo si sana.. anakuwa mkali na hasira ukichanganya na njaa.... basi ni kama wamevuta bhangi tu.
We kichwa yako si nzuri bana mdogo...
 
View attachment 142139

Wadau kuna vikosi vingi hapa nchini vya usalama wa wananchi,viongozi na Taifa ambavyo havijulikani kabisa kwa wananchi,sasa nimeamua kwa mtiririko kama wa series nitakua nakuja na kikosi kimoja kimoja kwa nia ya kuwafahamisha ili wakati mwingine tuwe na uelewa kidogo kuhusu usalama wetu,viongozi wetu,na nchi yetu kwa ujumla...na leo nawaletea kikosi cha KM maana yake Kikosi maalumu cha jeshi la magereza....

Kikosi cha KM kama ilivyoainishwa ni kikosi cha jeshi la magereza ambacho hutumika kutuliza fujo na kazi maalumu za jeshi la megereza kwenye magereza zote hapa nchini,Kikosi hichi kinaundwa na vijana shupavu wenye urefu usiopungua futi sita na lazima uwe na miraba minne,mavazi yao yanajumuisha ngao,nguo ngumu kwa ajili ya kujikinga na mabuti magumu sana yenye chuma kwa mbele.

utendaji wa KM ni wa ajabu sana,kwa mfano ikajulikana na mkuu wa gereza kuwa kuna watu wanataka kuanzisha fujo ya jumla gerezani? hii huwa inajumuisha wafungwa wengi sana,au kuna wafungwa wanapanga kutoroka kwa kutumia nguvu mkuu wa gereza hatawaambia kitu lakini siku hiyo mtakapofunguliwa milango ya sero zenu ili muende kazini hapo ndo ghafla mtakutana na KM mbele yenu,kwa idadi ya kutosha na hamtaona askari hata mmoja wa magereza mliemzoea,halafu wao watawatangazia kua mvue nguo zote na wao huanza kichapo cha kufa mtu bila kuwaambia sababu,mtapigwa kinyama sana hadi mtalainika tu halafu ndio wanaweza kuanza kuwahoji mkiwa hoi kabisa.

KM wanaogopeka kwasababu ni wakatili sana,utendaji wao ni wa kikatili zaidi ya field force,wao hawaogopi kitu maana kule gerezani haki ni ndogo mno,KM wengi wanavuta bhangi na wanalipwa mshara kidogo sana,na mara nyingi hawana kazi yoyote,ni hao tu wafungwa wakorofi wanaowaogopa tu! na nia hao tu ambao wana uwezo wa kutuliza ghasia kubwa kabisa gerezani.

sio kila gereza lina KM,mara nyingi vikosi vyao vipo sehemu zenye magereza makubwa tu lkn hupelekwa kwenye magereza madogo kama kukiwa na matatizo kama niliyoyasema hapo juu,kitu kimoja ambacho ukimuuliza mfungwa yeyote kuhusu KM atakujibu ni kwamba hao ni wanyama na sio binadamu,na wanawaogopa sana.

ukiwa mfungwa mkorofi,utapangiwa kwenda kufanya kazi katika kikosi cha KM kwa maana kambini kwao,maana wana kambi tofauti,hilo tu ni adhabu tosha kwa mfungwa na niamini hakuna mfungwa anaetaka mazoea na KM kwa namna ya aina yoyote ile.KM ni hatari kwa mfungwa kuliko mfungwa mwenzake hatari......

kama kuna maswali au una unachotaka kuongezea unaweza,na kesho kama sitabanwa nitawaletea habari kuhusu kikosi cha upelelezi cha jeshi( military inteligency agency) ambacho kipo Lugalo

Shukrani!
Kuhusu lugalo huo ni uongo mkuu
 
Uwepo wa kikosi hicho ni wa kupoteza nguvu kazi na fedha za mafunzo maana tokea nipate akili sijawahi kusikia kuna gereza wafungwa wameaasi..Mambo hayo yapo sana South na Latin America
Endelea kusubiri media zitangaze kuwa Gereza fulani kuna covert operations za wafungwa, Hio Huwa Hazitangazwi KM waki suspect tu unusual activities basi hutimba na Kisago huanza
 
hahahaha,Mkuu Mimi si mtu wa siasa na sitarajii kuwa mwanasiasa,maana kuwa mwanasiasa ni hatari kuliko jasusi,ukiwa jasusi ukikosea adhabu yake unapewa wewe mwenyewe,lakini ukiwa mwanasiasa ukikosea wanachi wote nchi nzima wanaadhibiwa,adhabu kali
Kweli tupu. Nimeamini kuwa unafaa kuwa kama kifaa hiki
IMG_20180714_194957.jpg
 
Endelea kusubiri media zitangaze kuwa Gereza fulani kuna covert operations za wafungwa, Hio Huwa Hazitangazwi KM waki suspect tu unusual activities basi hutimba na Kisago huanza
ubabaishaji tu nawajua KM kuliko unavyofikiria hivi mfungwa ambae hana silaha wala pa kujificha anahitaji nguvu kubwa wanayopoteza wale jamaa..wangine hadi wanakufa au kupata ulemavu kwenye mafunzo..ni ukosefu wa akili tu
 
ubabaishaji tu nawajua KM kuliko unavyofikiria hivi mfungwa ambae hana silaha wala pa kujificha anahitaji nguvu kubwa wanayopoteza wale jamaa..wangine hadi wanakufa au kupata ulemavu kwenye mafunzo..ni ukosefu wa akili tu
Mkuu ukitaka kuwajua tembelea Ukonga au chokoza vya watu ukishindwa sana kamuulize Scorpion
 
Back
Top Bottom