Je, unakijua kikosi cha KM?

Je, unakijua kikosi cha KM?

Haiwezekani mkuu kama mods wameibania basi iache tu iende zake na nadhani huu utakua ndio mwisho wangu wa kupost hizi inteligence posts naona mods wanapenda sana tujazane chitchat na jukwaa la siasa

Inasikitisha sana.Wanataka tujazane MMU
 
Sasa kwanini wanalipwa mshara mdogo kwa kazi ngumu wanayofanya????


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Mtu mmoja ambaye hatakin jina lake lioneshwe JF kwa kuwa sio msemaji rasmi wa suala hili ananinongoneza hapa kwamba hawa jamaa and company kwa maana ya wenzao wengine walio kwenye service wanalipwa ujira mdogo kwa maana waliingia hapo baada ya kila kitu mtaani kuwa hakiwafai kutokana na ufaulu usioridhisha wa kidato cha nne na darasa la saba miaka yao waliyomaliza!
 
maishapopote Nadhani inategemea na mfungwa. Inamaana hata mfungwa wa EPA nae anakula kichapo?
Asante kwa somo zuri
 
Last edited by a moderator:
nadhani mwaka 2005 kunaeneo dar wananchi walikuwa kwenye mgogoro na magereza wakatumwa hawa wajomba,nenda kawaulize ile shuruba FFU hakamati hapo
Ahaaaa, nadhani ni ile ambayo waandishi wa habari wakaenda na camera zao; nao wakala kichapo wakabaki kulialia magazetini mwezi mzima! Jamaa jibu lao lilikuwa short and clear; Waandishi walivunja sheria kwenda eneo la gereza!!!
 
Uwepo wa kikosi hicho ni wa kupoteza nguvu kazi na fedha za mafunzo maana tokea nipate akili sijawahi kusikia kuna gereza wafungwa wameaasi..Mambo hayo yapo sana South na Latin America
Ukiona nyumba yako haishambuliwi, jua mlinzi wako ni timamu sana hata maadaui hukaa mbali ( ingawa si walinzi wote)

Sasa mfute kazi ukiona anakula bure, utagundua kitu
 
Mara nyingi wanakuwaga vijana wa jkt,wakitoka kozi ya jkt kama service mana(sm) ambao wanakuwa kitengo cha combati karate(wanajiita karateka) ,wanapelekwa moja kwa moja vikosi na kambi za mafunzo maalumu ya magereza,
Si kweli.

KM ni kozi ya ujuzi zilivyo kozi nyingine katika vyombo vya usalama na ulinzi.

Baada ya vijana kupiga kozi basic ya magereza, ndipo kuna ambao huendelea na mafunzo ya ziada.
 
Si kweli.

KM ni kozi ya ujuzi zilivyo kozi nyingine katika vyombo vya usalama na ulinzi.

Baada ya vijana kupiga kozi basic ya magereza, ndipo kuna ambao huendelea na mafunzo ya ziada.
Mkuu sio kweli kivipi sasa'mbona unaniunga mkono,

Mara nyingi mnapo ripoti katika vikosi vya mafunzo ya magereza huwa kuna waliopitia usaili wa mtaani na walio pitia usaili wa jkt,sasa makamanda wanapokuwa wanafanya selection ya watu maalumu kwaajili ya kuwa km's ndipo uzingatia wale waliopitia jkt na uwapa platoon yao wakisha maliza mafunzo ya awali, kwaajili ya kuendelea na mafunzo ya ziada.

Ni kama ilivo kwa kikosi maalumu cha police field force (Ffu)mafunzo ya awali mtafanya wote lakini kuna wataobaki na kuendelea na mafunzo ya ziada na kigezo kikubwa huwa ni jkt na mara chache sana uchukua hata wasiopitia jkt
 
Back
Top Bottom