Je, unajua namna Sekta Binafsi zinavyoshiriki katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
JF Voice based SEKTA BINAFSI TABIA NCHI.jpg
JamiiForums wakishirikiana na Taasisi ya Wajibu wataangazia dhana nzima ya Mabadiliko ya Tabianchi, Athari zake pamoja na jitihada Mbalimbali zinazofanywa na Sekta Binafsi katika kukabiliana na Changamoto hii.

Karibu ujiunge na ushiriki nasi kwenye Mjadala huu utakaofanyika siku ya Alhamisi ya Septemba 21, 2023, kupitia 'X Spaces' ya JamiiForums

Kujiunga na mjadla huu gusa hapa

Pia, unaweza kuandika maoni yako kwenye uzi huu, yatasomwa siku ya mjadala.

=====

Umuhimu wa kila mtu kushiriki katika mchakato wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Edward Leonard Ishengoma-Mkurugenzi wa utafiti na utafiti Energy Cards akishiriki katika mjadala huu amesema ni muhimu kila mmoja kushiriki katika kutafuta suluhisho kwenye mabadiliko ya tabia nchi kwasababu jambo hili linamgusa kila mmoja, na ikiwa kila mtu hatahusika kwenye juhudi hizo kutakuwa na madhara makubwa.

Amesema pia ni muhimu kwa Sekta Binafsi pia ni katika mchakato wa kutafuta utatuzi katika mabadiliko ya tabia nchi sababu serikali haiwezi kufaya kila kitu wenyewe.

Msaada wanaohitaji vijana kwenye kubaliana na mabadiliko ya tabia nchi

Doreen Ngemera, Mwanaharakati wa Mazingira amesema vijana wanahitaji msaada wa fedha pamoja na elimu katika mapambano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, akisema kuwa vijana wako tayari kushiriki katika miradi mbalimbali ya mazingira na kutoa ubunifu wao katika kukabiliana na tabia nchi lakini rasilimali fedha inawaangusha.


Nafasi ya Afrika katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
Justine Godson, Mkurudenzi Mtendaji wa African Youth Transformation amesema chi nyingi Afrika zina uwezo mdogo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia kuna changamoto ya kukubaliana katika kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kati ya nchi za Afrika na nchi zilizoendelea. Jstine ameshauri nchi husika iwe inatenga bajeti kwenye juhudi hizi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

GERVAS SULLE: MATAIFA YA MAGHARIBI HAYAKUBALI KUCHANGIA FEDHA KUKABILI ATHARI ZA MAZINGIRA

Mdau huyo wa Mazingira amesema Licha ya Mabadiliko ya Tabianchi kuwa ni suala la kimataifa lakini, bado kuna mataifa yamekuwa nyuma katika kusaidia uwezeshaji wa kupambana na changamoto zinazojitokeza na hivyo, kuna viwango vya kuanza kushughulikia kwa ngazi ya Taifa

Ameonya kuwa endapo Mataifa ya Magharibi hayatakubali kuchangia kwa kiwango kikubwa cha Fedha au kushiriki kupambana na mabadiliko itakuwa ni wimbo tu ambao utaimbwa bila kuwa na matokeo yoyote.

Akiongezea mchango wake kuhusu changamoti hizo, Mdau wa Mazingira, Justine Mponda amesema katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, taasisi za Serikali zinapaswa kuliweka jambo hilo katika bajeti zake

Kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Justine Godsone amesema mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari zake isionekane kama ni janga la nchi fulani pekee na kwamba haliwahusu watu wengine, nchi zihusike kwenye kukabiliana na athari zinazoletwa na mabadiliko hayo kwa pamoja wakati suluhisho linatafutwa.

Mchangiaji Bilali Kileo kwa upande wake amesema Tanzania ianze kutumia magari ya umeme na gesi asilia, ambayo yatapunguza uchafuzi wa mazingira, lakini pia Serikali ihakikishe elimu inatolewa kwa watu wote kuhusu mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari zake.
 
Back
Top Bottom