Je, unaamini opposition kuingia Ikulu ndiyo suluhu ya matatizo yetu?

Kama huyaoni yanayofanywa na wapinzani hasa kwa wakati huu. nina wasiwasi na wewe.

Unamjua mganga njaa?

Yeye anaangalia akipata mlo tu basi analala kama sign yako inavyosema.

Hio Ikulu ni kama mwanamke ambaye amefikia umri wa kuchumbiwa au mwanamke ambaye keshaolewa tayari.

Yule mhongaji mzuri, mvuto, au mwenye maneno mazuri ndio baba mwenye nyumba.

Kama wapinzani wanamtaka huyo mwanamke [Ikulu] wataganga njaa kweli?

Yaani Ikulu unaifananisa na kuhonga wanawake? kazi kweli kweli...

Haya niambie hayo waliyoyafanya wapinzani zaidi ya kuombea ruzuku kila uchao...
 
Tazama katiba za vyama vyote vya siasa nchini, CCM pekee ambayo moja ya madhumuni yake ni kukamata mamlaka ya dola. Hakuna dhumuni hili kwenye katiba za vyama vingine. Mpaka hapa bado unaamini kuwa primal objective ya vyama vya upinzani ni kwendq Ikulu?

Mpita Njia,
Sawasawa nimekuelewa,
Je unadhani kugombea kwao kwenda Ikulu katika chaguzi zilizopita ilikuwa ni makosa kwao kufanya hivyo? Kwa sababu hapa tumekuwa tukishuhudia resources nyingi zikielekezwa kukisaka kiti hicho?
 
Mpita Njia,
Sawasawa nimekuelewa,
Je unadhani kugombea kwao kwenda Ikulu katika chaguzi zilizopita ilikuwa ni makosa kwao kufanya hivyo? Kwa sababu hapa tumekuwa tukishuhudia resources nyingi zikielekezwa kukisaka kiti hicho?

Dhamira ya cvhama inaonyeshwa kwenye katiba yake. Dhamira hiyo inaweza kuonekana kwenye 'kuwekeza', (kama ulivyosema resources) nyingi kwenye eneo fulani (wewe unasema kwenda ikulu).
Kwa kwua sina hakika na kiasi cha resources ambazo vyama vilitumia katika 'uwelezaji' wao kuitafuta ikulu vs kutafuta viti vya Bunge, inaniwea vigumu kuwashutumu kuwa waliwekeza zaidi kwenye kuingia ikulu kuliko kutafita viti vya bunge.
Kama una data za 'uwekezaji' huo wa resources zao, nadhani turtakuwa na bases nzuri ya kuargue kuhusu wapinzani kuwekeza zaidi kwenye kuwania ikulu kuliko viti vya bunge
 
Yaani Ikulu unaifananisa na kuhonga wanawake? kazi kweli kweli...

Haya niambie hayo waliyoyafanya wapinzani zaidi ya kuombea ruzuku kila uchao...

Ndio maana nikakuambia mwanzo kwamba kama huyaoni wanayofanya wapinzani [HASA KWA SASA/ KIPINDI HIKI TUNACHOONGEA] basi una matatizo

Halafu bila kujua kwamba ruzuku zinatoka kwenye jasho la kila mtanzania.
Ruzuku ni haki zao kwani ni wawakilishi wa wananchi na wanawatetea sio Bungeni tu bali kitaifa. Taifa lina wana CCM na wapinzani [malizia la saba upate japo kuelewa].

Hivi wewe umesomea wapi?

Mbunge akitetea jimbo fulani hasemi kwamba haya ninayotaka yafanyike yafanyike kwa watu wa CCM tu au wapinzani, yanafanyika kwa wananchi wote walipa kodi wakiwa CCM na wapinzani upo hapo?

Kwahio kama hayo huyaoni basi nina wasiwasi na elimu yako.

Nakupa homework kidogo, Mtanzania ni CCM na wapinzani
Walipa kodi sio CCM tu bali wapinzani,na
na wale ambao hako upande wowote

Wanapewa ruzuku kwa kuwatetea watanzania
wote
Keshokutwa nitakufundisha zaidi kuhusu utaifa
 
Ahsante Bubu ataka kusema,
Pamoja na maelezo yako mazuri, mimi ninafikiri ni vyema sasa tukatafuta mustakabali wa nchi yetu kwa kuchangia ni nini tunakiona juu ya mambo ya kitaifa. Sasa tunakwenda kwenye uchaguzi wa Tarime, baada ya miaka miwili na nusu duru la uchaguzi Mkuu litakuwa limerudi tena, how ready are we gonna be? Opposition waendelee kukitafuta kiti cha urais kwa udi na uvumba? au wajikite kutafuta wabunge wengi zaidi wa opposition?

Mimi kwa maoni yangu upinzani inabidi uungane ili kuongeza nguvu zao na kutuonyesha Watanzania kwamba wanaweza kabisa kuuweka ubinafsi pembeni kwa maslahi ya Taifa. Wakishafanya hili wajitangaze mijini na vijijini na wanaweza kabisa kuchukua Ikulu na Bunge maana CCM haistahili kabisa kuendelea kuwepo madarakani hata kwa siku moja achilia mbali miaka mingine mitano.
 
Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba sisi kama wananchi tuwe na mapango wa panga pangua. hapa namaanisha kwamba pamoja na itikadi zetu za kisiasa chama chochote tunachokipa madaraka kipimo chake ni miaka mitano tukiona wafanya vizuri tukisaport kwa miaka mingine la sivyo tunaweka pembeni tunaangalia kingine hii itaondoa ukiritimba wa ccm wa kujitapa kuwa hakuna mwenye uwezo wa kukiondoa madarakani. Hivi vyama hasa ccm lazima vitambue kuwa wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho. Leo hii Kanu iko wapi?? si walikuwa na majigambo kama ccm, hata kama itakuja kufanikiwa kurudi madarakani lakini washajua kuwa wananchi wakiamua wanaweza.
 
Kwa mtazamo wangu, msemo kwamba "Upinzani kuingia Ikulu ndio suluhu ya matatizo yetu" una utata kidogo. Kama wapinzani wakifanikiwa kuingia Ikulu then wakapata popularity na kuanza kuweka itikadi za "Chama ama forum Chetu/yetu" ama "Chama ama forum (k)ina wenyewe" na kuendesha mambo kivyaovyao bila ya kusikiliza stakeholders (wananchi) wanasema nini mimi nafikiri itakuwa ndio tiketi ya wao kubwagwa 5 years later.

Let's learn from blunders zinazofanywa na Serikali iliyomo madarakani sasa hivi kwamba haisikilizi malalamiko ya Raia pamoja na raia kupiga kelele nyiiiingi kuhusu ufisadi, kiwira nk...., na sisi tutumie reference hiyo kujirekebisha kuanzia humu humu JF.
 


SULUHISHO LA MATATIZO YETU NI....

elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu-elimu
 
Asalamu alaykum.

Mimi nadhani wapinzani wafanye yote mawili kukitafuta kiti cha urais na pia nafasi za wabunge na wawakilishi kwa upande wa zanzibar.

jambo la kuungana kwa vyama nalo ni tatizo jengine kwa sababu uzoefu unaonesha kuwa vyama vya upinzani hapa nchini wanashindwa kuafikiana katika kuungana lakini jengine ambalo kubwa ni kuwa ni katiba yetu tulionayo haijurusu suala hilo. kwa hivyo kwanza katiba ifanyiwe marekebisho then kuwepo na huo umoja.
 
Binafsi kama ingewezekana tulitakiwa tufanye kama Kenya tu... Vyama vya Upinzani viungane kumwondoa CCM Ikulu kwanza...Hata kama wanatofautiana ktk sera na ilani zao kama walivyokuwa Kibaki na Raila.. Kisha baada ya kumwondoa CCM ikulu ndipo wanaweza kuzishughulikia tofauti zao wakati CCM imepoteza kabisa sauti kama ilivyo KANU..
Tukitegemea mageuzi ya Wabunge tu jamani tujifunze kutoka Kenya yenyewe wakati waliposhinda Ubunge lakini Kibaki akawatoa je..
Pili Mugabe pia ni mfano mzuri wa kuacha kiti cha Ikulu kupigania majimbo. Lakini hadi sasa hivi inaonyesha wazi Upinzani hawawezi kula sahani moja hata kama wote wana njaa kali...
Kifupi CCM na Kikwete wanachukua tena ushindi tena wa Kimbunga na hakuna wa kuwazuia..
Bila kumwondoa CCM Ikulu hakuna lolote linalowezekana kwa sababu Bunge letu tumeliona likifanya kazi pale tu rais alipokubali wazungumzie.. Bunge halina nguvu zaidi ya Ikulu na kama tunavyojua JK anaweza kabisa kuvunja Bunge wakati wowote, na Bunge haliwezi kumsimamisha yeye, Ni politics za Afrika na nchi zote maskini..

Nitaendelea kupinga mabaya yanayoletwa na uongozi huu lakini sidhani kama kuna mapinduzi yoyote ktk Uongozi wa nchi yetu hasa pale tunaposhindwa kuelewa kwamba vyama vya Upinzani vikiwa vimegawanyika ni rahisi sana kwa CCM kuelekeza mapambano yake kwa chama kimoja na kikukidhoofisha..Chama ambacho kitaonekana kuwa tishio watawekewa vikwazo na kuburuzwa bila CCM kuonekana wanavunja sheria za uchaguzi kitaifa na Kimataifa..Ni chama kimoja tu chenye viongozi na wanachama wakorofi!... mbona vyama vingine havisumbuliwi?... hilo ndio litakuwa jibu lao kwa kila hoja itakayokuwa raised. Lakini kama watakuwa wameungana na CCM ikajaribu kuweka mbinu zake basi hicho chama kinaweza kujitoa ktk Uchaguzi na likawa pengo kubwa ktk demokrasia..
Tatizo jingine ni hao vibaraka waliopandikizwa na CCM ndani ya vyama vya Upinzani ambao kila kukicha ni wao wanaotumiwa kuzua FITNA baina ya viongozi na wanachama...Wangwe ni mfano mmoja mdogo sana na bado tutakuja yaona mengi hasa uchaguzi ukikaribia...
 
Suruhisho la matatizo yetu litakuja pale sisiemu iking'oka madarakani na viongozi walafi kama akina kingunge, RA,EL, wakienda zao.
 
Pundamilia07,

Mkuu sijui kama nimempata vizuri Invincible lakini mimi binafsi nina definition yangu kuhusiana na usemi wake na mara nyingi nimeuzungumzia isipokuwa kwa mafumbo na pengine naweza kusema kiswahili kigumu hasa napotumia mfano wa Pilau la maulidi..

Leo nitaiweka sawa, nimekuwa nikitumia neno hilo kwa sababu sisi wote tumepitia maisha hayo na rahisi kwetu kutazama tofauti zilizopo kati ya wale wanaochukuliwa kama Ulamaa (wasomi) na sisi wengine maamuma ambao huwa tunapangwa ktk janvi bila idadi tukisubiri hilo Pilau -Yaani pato la serikali..

Sasa kwa kuelewa kwangu matatizo yote tuliyokuwa nayo na hapa tulipofikia yamesababishwa na sio tu viongozi wabaya isipokuwa mila na desturi zetu za kutunikia watu wadhifa na uheshimiwa bila kuchunguza zaidi elimu za hao watu ama kama kweli wanastahili nafasi hizo...

Tazama katika Pilau la Maulidi kuna kundi la watu huandaliwa ama kutengwa kama waheshimiwa - Masheikh, Mapadre, Viongozi, Ulamaa, Waheshimiwa na kadhalika hali hakuna mtu yeyote anayefahamu elimu ya watu hao kupewa heshima ile isipokuwa tunachofahamu ni title ama sifa ililotangulia jina lake hivyo kumwezesha kukaa msitari wa mbele..

Na kwa sababu hawa watu wanafahamu ujuha wetu kuwatukuza bila kutazama kwa kina uwezo wao ktk sifa hizo ama wameweza kufanikisha kitu gani hawa jamaa wamekuwa mstari wa mbele kuvuna zaidi wakivaa majoho ili siku ya kula hilo Pilau wawe janvi kubwa wakiongoza jamii zetu ktk fani ambazo hawana ujuzi zaidi ya sifa wanazopewa na wananchi wenyewe....
Na ukitazama kwa makini wengine hata kuongoza dua yenyewe hawawezi isipokuwa waitikiaji wenye madaha na sauti kubwa utafikiri Mungu alisubiri tu sauti zao ili dua hiyo ipokelewe...Na ajabu ni kwamba hata ktk sala hawa watu ama kundi hili hujipeleka msitari wa mbele na wakakubalika lakini sio mlalahoi ambaye hafahamiki, hakupeba title fulani mbele ya jina lake..Huyu atapigwa jicho la kuuliza wewe vipi?..jicho la kind like.. "Do You belong here?"

Sijui kama uko nami hadi hapo...

Kwa hiyo kama tupo pamoja utakubaliana nami kuwa watu hawa ambao tumekuwa tukiwatukuza ktk jamii zetu wameweza kujenga heshima ambayo haiwezi kuvunjika kirahisi pamoja na kwamba hakuna kati yetu anayeweza kusema mapungufu ya watu hao ktk elimu, utendaji kazi, uheshimiwa ama uongozi wa ngazi waliyokuwa nayo na kama ikitokea mtu kukosoa hawa watu basi wewe ni mfitini..Hawa ndio the CHOSEN ONE... tunawaheshimu na kuwatukuza bila shuku ya aina yoyote kwa sababu NDIVYO TULIVYO!

Sasa basi ukirudi ktk Siasa na Utumishi wa Umma utakuta hali ni ile ile kwamba kuna watu wameweza kuchuma Uheshimiwa kwa njia kama hizo.. hawa watu toka tupate Uhuru aidha kwa kupitia Mwalimu waliweza kujenga majina yao na kupata heshima ambazo haziwezi kupimwa na katika kutumia nafasi hizo wameweza kufaidika zaidi ktk Pilau la Maulidi...
Ni hawa ambao wanapambwa kila siku hali hawana ujuzi wowote zaidi ya majina yao ambayo wameyajenga wakati wa mwalimu kwa sababu hapakuwepo na wasomi isipokuwa umaarufu ndio ilikuwa CV ya kutosha..

Tumeendelea na mfumo huo hadi leo hii kiasi kwamba leo hii tuna Ma - Dr na Phds kibao bandia ambao kama kawaida wamekaa janvi kubwa, hatuna fikra za ku challenge uwezo wao ktk utendaji kazi ama elimu zao. Leo hii ukitazama ngazi za CCM utaona watu yenye kila sifa na title zilizotangulia majina yao na aghalab mtu ku question uwezo wake mbali na kujiuliza kama hizo sifa alizokuwa nazo zinampa vipi nafasi na uwezo wa kukaa meza kubwa.. Tumefikia hata kiwango cha kuamini kwamba mtu fulani maadam ana elimu kubwa Phd na kuzungumza kiingereza cha England au US basi ni lazima atakuwa kiongozi mzuri na amesoma sana.. imani ile ile tunayoipata sisi misikitini kuamini mtu akiweza kuongea kiarabu basi bila shaka kasoma sana Kuran na lazima awe Sheikh mzuri.

Hapo ndipo CCM ilipotufunga magoli na kama kawaida wanatuweka janvini kila siku kwa promises ambazo pamoja na ulaghai wao tunaamini kabisa kwamba kesho itakuwa bora zaidi kwetu hali wao bado wamekaa meza kubwa ya waheshimiwa...
To my experience sijawahi kuona wala kusikia ugawaji mzuri wa Pilau ktk janvi la walalahoi zaidi ya kushuhudia watu wakishindana mikwapuo ya chakula cha siku moja...
Kila sifa utakayoiona kwa viongozi wetu ni sifa ya siku moja tena basi haina comparative relation kati yake na idadi ya walengwa na ndio maana unaona watu wakigawiwa T Shrt, fulana ama mtu anafunga bar na kutoa round za safari....

Sasa basi tunaweza kusema haya yote yanatokana na watu kutokuwa na ELIMU, lakini mimi baada ya kulitazama swala hili kwa undani zaidi naanza kuamini kwamba mbali na ELIMU kuna vipengele vinayhotufunga tambala la uso wananchi...
1. NJAA
2. IMANI
Ni vigumu sana kwa vyama vya Upinzani, wasomi na wote wenye kufikiria kwamba ELIMU inaweza kuwaondoa watu Ujinga tulikuwa nao kwa sababu hizi factors mbili ni Ufa mkubwa sana ktk kueneza ELIMU yenyewe..Mtu mwenye NJAA na aliyejengwa IMANI ya kuabudu CCM..
Ni rahisi sana kuwaongoza kondoo WALIOPOTEA (Kwa elimu na kuwajenga imani mpya) lakini sii rahisi hata kidogo na pengine vigumu zaidi kuongoza kundi la kondoo wenye NJAA..

CCM wanajua kuwa wananchi wana NJAA na wanaendelea kutuweka na Nnjaa hiyo makusudi ili siku ya siku itakapo fika wataliweka sinia la Pilau ktk janvi letu... Kutokana na njaa kali hapo elimu yote wote itawekwa pembeni na utaona mikonoz juu ya sinia..

Kifupi, no matter what! wananchi wana njaa kali na hata siku moja msitegemee judgement yao ama wao kuwa mstari wa mbele kupiga kura against CCM hali wananchi matumbo yao wazi..Fikra za wao kufikiria kesho, kesho kutwa ama kizazi kijacho ni kiini macho kwa mtu mwenye njaa.

Kama Julius Kaizar, mabadiliko ni kuondoa Utawala uliokaa meza kubwa..
 
Naam wenye dira ni chama cha mafisadi tu ambacho kimejaa wahuni, mafisadi, na walioweka maslahi yao binafsi na ya chama chao mbele kuliko yale ya Tanzania kwa kusaini mikataba ambayo haina maslahi yoyote kwa Watanzania, kukupua mabilioni ya pesa za walipa kodi na kuziweka kwenye bank accounts zao nchi za nje. Ukiwauliza wamefanya nini ambacho Watanzania wanaweza kujivunia, wanang'aa macho. Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu! :(

Na ulichoandika ndio sera za upinzani.

So you are justifying that Upinzani hauna vision! Chama Kikubwa kama CCM lazima kuwe na walafi, kwa taarifa yako CCM ni reflection ya Watanzania kwa kuwa population kubwa iko nao.

Kuwatukana CCM ni kuwatukana Watanzania...

Mfano kuitukana DP; umetukana Mch. Mtikila na washirika wake wachache, kuitukana NCCR-Mageuzi umemtukana Mbatia na Group lake....

Kuitukana CHADEMA umetukana probably more than 5Mil. people in Tanzania, CUF the same...

Prolating the figure ukiitukana CCM umetukana wale watu waliowapa kura by 80%.
 
Binafsi kama ingewezekana tulitakiwa tufanye kama Kenya tu... Vyama vya Upinzani viungane kumwondoa CCM Ikulu kwanza...Hata kama wanatofautiana ktk sera na ilani zao kama walivyokuwa Kibaki na Raila.. Kisha baada ya kumwondoa CCM ikulu ndipo wanaweza kuzishughulikia tofauti zao wakati CCM imepoteza kabisa sauti kama ilivyo KANU..
Tukitegemea mageuzi ya Wabunge tu jamani tujifunze kutoka Kenya yenyewe wakati waliposhinda Ubunge lakini Kibaki akawatoa je..
Pili Mugabe pia ni mfano mzuri wa kuacha kiti cha Ikulu kupigania majimbo. Lakini hadi sasa hivi inaonyesha wazi Upinzani hawawezi kula sahani moja hata kama wote wana njaa kali...
Kifupi CCM na Kikwete wanachukua tena ushindi tena wa Kimbunga na hakuna wa kuwazuia..
Bila kumwondoa CCM Ikulu hakuna lolote linalowezekana kwa sababu Bunge letu tumeliona likifanya kazi pale tu rais alipokubali wazungumzie.. Bunge halina nguvu zaidi ya Ikulu na kama tunavyojua JK anaweza kabisa kuvunja Bunge wakati wowote, na Bunge haliwezi kumsimamisha yeye, Ni politics za Afrika na nchi zote maskini..


Probability kwamba yaliyotokea Kenya (in red above) yanaweza kujirudia hapa kwetu ni ndogo mno. Na ikitokea, tutakuwa tumepiga hatua kubwa mbele.

Nadhani mabadiliko ya haraka ndiyo yatatuharibia kabisa, hasa ukizingatia hali yetu ya kisiasa ilivyo.
Vyama vya upinzani vionyeshe ukomavu kwa kushirikiana kizalendo, mfano kuachiana majimbo.

Pundit aliwahi kusema,
...It all depend on how you look at it, kama unataka kumuondoa leo leo, sio mimi tu hata CHADEMA na civil society ya Tanzania - if we have one- are too late.

My approach embraces gradual change in the absence of rapid revolutions.

By exposing him, I am not putting up with him, to the contrary I am puting him out there for the world to see how much of a fraud he is.

SOURCE: Bush na Kikwete; Hizi ndio sababu za kupayuka kwetu?


.
 
ndio njia pekee lakini sioni mwanga ndani ya upinzania pia... nani anaweza kuwa rais kuotka upinzania? but we need changes. imewezekana kenya na tz tufanye hivyo ili CCM itie adabu
 
Back
Top Bottom