Je, unaamini opposition kuingia Ikulu ndiyo suluhu ya matatizo yetu?

Ni kweli unavyosema bwana Kasheshe
Wapinzani hawana dira. Inaonekana na kueleweka hivyo kutokana na halihalisi ya mazingira wanayoendeshea siasa zao kuanzia gharama za uendeshaji, ushindani uliopo na chama tawala, media coverage, matumizi ya state machineries, falsafa potofu zinazoendeshwa na chama tawala dhidi ya vyama vya upinzani, level ya uelewa ya watu wetu kuhusu mambo ya siasa, matumizi ya jina "WAPINZANI" na maana halisi kwa watu wa kawaida [ambao ndio wengi wa wapiga kura] na mengine mengi.

Ni kweli vilevile kwamba CCM wana dira na ni dira hiyohiyo ndio iliyotufikisha hapa tulipo [kila moja anajua mahali alipo kwa sababu sio wote tupo sehemu moja-kuna walio mbele yetu kwenye hii safari ya maisha bora ndio maana wanatetea dira iliyopo]

Kwa maelezo haya ninashawishika kuamini kuwa opposition wakiingia ikulu tunaweza kuona upande wa pili wa shillingi achilia mbali hujuma za wale watakaokuwawameenguliwa kwenye sistim. Why? Tutakuwa na dira tofauti na hii ya sasa.
 
Last edited:
je unaamini ccm kushikilia madaraka kimizengwe ndiyo suluhisho la matatizo yetu?
 
Upinzani utakapobadilisha sura ya muundo wa vyama vyao na katiba zao amb azo kila kitu ni blue print ya CCM na kuwa na sera, basi labda tunaweza pata tumaini.

Kwa nini Chadema au CUF wasibadilishe mfumo wa muundo wa vyama vyao na kuwa kama Republican na Democrats ambapo ushiriki wa wanachama na wapiga kura wafuasi katika maamuzi ni mkubwa na si ile system ya Politburo ya Halmashauri Kuu, Kamati Kuu na upupu mwingine wa Ki-CCM?

Je kuwa na Halmashauri Kuu na Kamati kuu ni sharti la kusajili chama kwa Tendwa?
 
Upinzani kuingia ikulu si suluhisho la matatizo yetu. Hali kadhalika chama tawala kubakia madarakani si suluhisho la matatizo yetu. Suluhisho ni kuwa na dira sahihi iliyojikita katika matatizo ya msingi tuliyonayo, na kupata watu wenye uwezo, utashi, nia na uzalendo wa kuyasimamia. Watu wa namna hii wanaweza kupatikana katika chama chochote, kama ilivyo kuwa mafisadi wanapatikana katika chama chochote pia. Tuna tatizo la jinsi ya kuwatambua watu wenye sifa hizi na kuunganisha nguvu zao kuzielekeza katika kuijenga nchi.
 
Msimamo wangu ni ule ule

Wapinzani wapewe Ikulu hata ni kwa muda mdogo tu ndio vyama vya siasa vitakua na changamoto yakuwatetea wananchi.

Mkumbuke kwamba sio CCM wote ni mafisadi kwahio wakiingia wapinzani Ikulu ndio CCM itaweza kujisafisha na kuondoa wale wote wachafu/mafisadi ambao walisababisha chama kuangushwa.

Hapo ndipo tutaona viongozi wanaojali wananchi na sio viongozi wanaojali mambo yao.
 
hayo uliyotema hapo ni madini matupu....big up
 
Tatizo sio nani ataingia Ikulu ,maana hata Malaika akifanikiwa kuingia Ikulu basi atatesa tu.
Jambo ambalo litawaweka sawa wanaowania kuongoza serikali ni kuibadili KATIBA ili iendane na wakati,kuna mambo mengi ambayo ufafanuzi wake haupatikani katika KATIBA ya sasa iliyotungwa kwa kura ya ndio hio hio au hapana ila hiyo.

Kwa nini vyama vya upinzani havianzishi katika mahakama zetu kudai Ukarabati wa Katiba na ikibidi itungwe upya.Utawasikia majukwaani wakipiga makelele lakini hatuoni kuanzisha mikakati ya kuwaunganisha wananchi katika kudai KATIBA mpya ,au tuseme wana agenda ya siri.
 
Upinzani utakapobadilisha sura ya muundo wa vyama vyao na katiba zao amb azo kila kitu ni blue print ya CCM na kuwa na sera, basi labda tunaweza pata tumaini.

Kwa nini Chadema au CUF wasibadilishe mfumo wa muundo wa vyama vyao na kuwa kama Republican na Democrats ambapo ushiriki wa wanachama na wapiga kura wafuasi katika maamuzi ni mkubwa na si ile system ya Politburo ya Halmashauri Kuu, Kamati Kuu na upupu mwingine wa Ki-CCM?

Je kuwa na Halmashauri Kuu na Kamati kuu ni sharti la kusajili chama kwa Tendwa?

Rev. Kishoka,
Umeandika kwa kifupi mno lakini ni ujumbe ambao ni mzito sana. Ni kweli kabisa siasa za Tanzania zinahitaji 'overhaul' ili kuonesha tofauti kubwa kati ya Chama tawala na vile ambavyo vitakuwa vinasubiri kuunda serikali. Vyama vya siasa vya Tanzania vinawapa watu wachache (Viongozi wa Vyama) uwezo wa ku-manipulate na kuamua hoja za mustakabali wa nchi hii bila kujali. Vyama vya upinzani ambavyo ndiyo vilitakiwa kuwa chachu ya mabadiliko vyenyewe navyo vimejikuta vikihangaikia kutafuta nyadhifa badala ya kujenga misingi mizuri ya vizazi vijavyo vya nchi yetu.
"Kila mtu anatafuta short cut"
 
Upinzani kuingia ikulu si suluhisho la matatizo yetu. Hali kadhalika chama tawala kubakia madarakani si suluhisho la matatizo yetu. Suluhisho ni kuwa na dira sahihi iliyojikita katika matatizo ya msingi tuliyonayo, na kupata watu wenye uwezo, utashi, nia na uzalendo wa kuyasimamia. Watu wa namna hii wanaweza kupatikana katika chama chochote, kama ilivyo kuwa mafisadi wanapatikana katika chama chochote pia. Tuna tatizo la jinsi ya kuwatambua watu wenye sifa hizi na kuunganisha nguvu zao kuzielekeza katika kuijenga nchi.

Kithuku,
Baada ya kumaliza kusoma posting yako, kwa namna moja au nyingine nimeona mawazo yako kwa kiasi fulani yameshabihiyana na mchango alioutoa Rev Kishoka. Wewe umesisitiza tuwe na dira sahihi na Rev. Kishoka amehoji kwa vyama vya upinzani kwanini visibadilishe mfumo wa muundo ili kuwapa uwezo zaidi wanachama kufanya maamuzi, je unadhani hii inaweza kuwa sehemu ya dira unayoifikiria?
 
Rev. Kishoka na Kithuku,
Mimi huwa si mchoyo wa shukrani hasa pale ninapoona kuwa mtu anastahili.

Nimevutiwa na mwelekeo mlioutoa hapo juu umenipa hata mimi pia fikra nzuri zaidi za kutathmini suluhu ya matatizo yetu.

Ninawapongeza kwa dhati kabisa kwa kunipa fikra nzuri.
 
Tatizo sio nani ataingia Ikulu ,maana hata Malaika akifanikiwa kuingia Ikulu basi atatesa tu.
Jambo ambalo litawaweka sawa wanaowania kuongoza serikali ni kuibadili KATIBA ili iendane na wakati,kuna mambo mengi ambayo ufafanuzi wake haupatikani katika KATIBA ya sasa iliyotungwa kwa kura ya ndio hio hio au hapana ila hiyo.

Kwa nini vyama vya upinzani havianzishi katika mahakama zetu kudai Ukarabati wa Katiba na ikibidi itungwe upya.Utawasikia majukwaani wakipiga makelele lakini hatuoni kuanzisha mikakati ya kuwaunganisha wananchi katika kudai KATIBA mpya ,au tuseme wana agenda ya siri.

Mwiba,
This is a very positive thought. Labda nikichangia hapa na huku nikifanya marejeo ya postings za Rev. Kishoka na Kithuku, ni kwamba vyama vya upinzani ambavyo ndiyo kwa sasa vinajukumu kubwa la kuongoza mabadiliko na hatima ya mustakabali wa kisiasa katika nchi hii, vimekosa mwelekeo wa kuwa dira inayoeleweka kwa huko tunakokwenda. Uendeshaji wa vyama hivi unategemea utashi wa watu wachache kwa yale ambayo wao wanaona yatawapa 'krediti binafsi' ya kisiasa. Endapo kama hivyo vyama vingekuwa vinaendeshwa kwa misingi ya kuwawezesha wanachama wake kuamua nadhani hayo unayoyafikiria au yale ambayo watu wa kawaida ndiyo wanayaona yanahitaji kufanyiwa kazi, basi ingekuwa ni jambo rahisi kabisa kutekelezeka. Kwa mfano suala labda la kudai marekebisho ya katiba kupitia mahakamani ingekuwa si suala la watu wachache waamue - waende au wasiende - lingehusisha wanachama/wapiga kura wengine.
 
Kwa hali ilivyo sasa upinzani hauwezi kuingia Ikulu 2010. Lengo lao kubwa linapaswa kuwa ni kukijeruhi CCM kwa kuwa na wabunge wengi halafu kulinda hivyo viti vya ubunge kwa udi na uvumba. Ni vigumu kuingia Ikulu ukiwa na wabunge 40 wa Upinzani. Kama lengo la kupata wabunge wengi linaweza kufikiwa hata wale wabunge ambao wako CCM kwa sababu ya woga wa kupoteza vyeo au maslahi wanaweza kufikiria kukihama au kuungana na upinzani bungeni kutetea hoja muhimu. Lakini, kwa maoni yangu, siyo vyama vyote vya upinzani ni vya upinzani kweli. Vingine ni CCM B. Kwa hiyo hii miungano au ushirikiano wa vyama vya upinzani unaweza kuwa unaumiza harakati za upinzani.

RUGE OPINION
 
Wakuu,

Kwanza naomba niseme kwamba, niliamua kuachana na siasa kwa muda hapa jamvini baada ya kukerwa na ile hotuba ya rais bungeni. Hotuba ile niliichukulia kama janga la kitaifa, hivo niliamua kuomboleza kisiasa kwa kipindi chote kilichopita baada ya hotuba!

Katika kuchangia thread hii napenda niseme kwamba, vyama vya upinzani bado vina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa 2010 kama tu vitafanya mambo yafuatayo:

1. Watengeneze mazingira yatakayowawezesha kuungana kwa dhati kabla ya 2010 na kisha wasimamishe mgombea mmoja wa serikali za mitaa, udiwani na ubunge ambaye anakubalika kwa watu wengi wa mtaa, kata na jimbo husika, na kisha vyama vyao vyote kwa pamoja vimuunge mkono!

2. Wasimamishe mgombea mmoja wa urais na aungwe kwa dhati na vyama vyao vyote.

3. Nawashauri wamchague bwana Hamadi Rashidi (CUF) agombee kiti cha urais, na Dr. Slaa (CHADEMA) awe Mgombea mwenza.

Wakifuata huu ushauri wangu, amini usiamini, wapinzani watashinda kwenye uchaguzio mkuu wa 2010!

Mungu vibariki vyama vya upinzani viweze kuungana kwa dhati ili watz wapate ukombozi wa kweli!

Mungu wabariki bwana Hamadi Rashidi (CUF) na Dr. Slaa (CHADEMA)!
 
Last edited:
Ukweli ni Kwamba Wapinzani hawana dira hata kuliko CCM! difficult to pronounce but that is the facts

Wapinzani ni vilaza lakini ninyi CCM vilaza zaidi. Labda apatikane mgombea mpya toka upinzani lakini hawa waliopo wananuka uchovu, hawataki kuamini hilo basi warudishe majina yao 2010 au 2015 waone wataambulia nini. Wang'atuke na kuwaachia mikoba watanzania wengine, kwani wao wanaweza wenzao wanashindwa wana nini? Embu huko, lakini CCM vilaza sana tu, pole Bwana kasheshe, habari ndo hiyo.

pamoja na upimbi wangu bado natambua kuwa CCM itamalizwa na wana CCM wenyewe, haswa vilaza wazuri kama Makamba, mkumbatieni na kuna cku mtayavuna mabua.
 
Mungu vibariki vyama vya upinzani viweze kuungana kwa dhati ili watz wapate ukombozi wa kweli!

Mungu wabariki bwana Hamadi Rashidi (CUF) na Dr. Slaa (CHADEMA)!

Msee, umesema kweli hapo. Lakini Mbowe, Mrema, Lipumba na ving'ang'anizi wengine waachie ngazi, Dr.Slaa akigombea walahi nitapiga kura. Kuna vichwa vizuri lakini vinabaniwa banaaa! Mrema kuachia cjui kama ni rahic hivyo, labda atokewe na Bwana Yesu na amwambie huwezi kuupata urais mangi
 
Wapinzani hawatakiwa kukaa kuwasubiri CCM, CCM wana resources zote wanazohitaji na ikifika kipindi cha uchaguzi watawapiga bao haraka haraka. upinzani wanatakiwa kuwa na strategy za long terms na short terms na mara baada ya uchaguzi wanatakiwa wawe wakiendelea na long terms kama vile kuhamasisha na kuongeza wanachama, na pia kujitangaza kisera katika maeneo ambayo hawajakubaliwa kuliko kusubiri hadi uchaguzi ndio waanze kupanga na ku-excute strategies zao.
 
ndio njia pekee lakini sioni mwanga ndani ya upinzania pia... nani anaweza kuwa rais kuotka upinzania? but we need changes. imewezekana kenya na tz tufanye hivyo ili CCM itie adabu

Mkuu Ochu,

Kama nilivosema kwenye post yangu iliyotangulia, Hamadi Rashidi anaweza kuwa rais na Dr. Slaa anaweza kuwa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania!
 
Je, bado tunaamini kuwa kwa wapinzani kuipata Ikulu ndiyo suluhisho la matatizo yetu?

...suluhisho la matatizo yetu ni jinsi wenyewe watanzania tunavyoyatafsiri matatizo yetu, na uwezo wetu wa kufikiria, na kuchanganua njia mbalimbali ambazo zikitumika, zitatatua matatizo yetu kwa manufaa ya wote kuanzia kizazi hiki na kuendelea.

Kinyume na hapo tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu!
 
Back
Top Bottom