Je, unaamini opposition kuingia Ikulu ndiyo suluhu ya matatizo yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unaamini opposition kuingia Ikulu ndiyo suluhu ya matatizo yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundamilia07, Sep 2, 2008.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wengi wetu tumeshuhudia katika chaguzi kuu za mwaka 1995 hadi 2005 vyama vya upinzani viliwekeza nguvu kubwa ya kuingia Ikulu kwa maana resouces nyingi zilitumika katika kutafuta kiti cha urais huku viti vya ubunge vikiachwa vitafutwe bila ya kuwekeza vya kutosha. Aidha, miaka 10 baadae baada ya uchaguzi wa kwanza uliohusisha vyama vingi, vyama vya siasa vya upinzani bado havijaelekeza nguvu zao nyingi za kuimarisha shughuli zao za kisiasa katika ngazi za chini kwa maana kuwa na matawi ambayo ndiyo majukwaa ya kukusanya wananchi na kusambaza shughuli zake.

  Je, bado tunaamini kuwa kwa wapinzani kuipata Ikulu ndiyo suluhisho la matatizo yetu?
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nikijibu kama Darwin.

  Wapinzani wakiingia Ikulu inategemea nani umemuweka Ikulu, sio kuangalia tu mtu kwamba ni mpinzani wa CCM basi tumuweke Ikulu, lazima tujue anachotaka kufanya akiwa Ikulu nasio kusema tu CCM wanafanya vibaya.

  Kwa upande wangu kama wapinzani wataingia Ikulu hata miaka mitano tu na CCM wakawa wapinzani ndio tutayajua hasa matunda ya vyama vingi.

  Kwanini?

  Wapinzani watajitahidi kwa uwezo wao kuwaridhisha wananchi ili waendelelee kuwa chama tawala.

  CCM kwa wakati huo kama wapinzani ndio watakaotoa changamoto sana kuhusu taifa letu.
  Wanajua pesa zinapatikana wapi na zitatumika vipi kuwanufaisha wananchi na kwahio wapinzani hawataweza kuwadanganya wananchi.

  Wapinzani nao kwa wakati huo kama chama tawala watajitahidi kuwatendea mema wananchi ili usukani usiende tena na mwingine.

  Yaani hao wapinzani wapewe hata miaka mitatu tu, hapo ndio tutayaona manufaa ya vyama vingi.

  Lakini kama toka mfumo huu wa vyama vingi uanze aliyekua ni huyo huyo wa mwanzo basi Tanzania haitafika kokote japokua ni nchi yenye utajiri.

  Ukimkabidhi mtu madaraka kwenye nyumba yako, na keshokutwa unata sukari akakunyima na akakuambia hana sukari, basi utamuambia unaniongopea kwasababu iko sehemu fulani, hii ilikua nyumba yangu na najua sukari ilipo, na kama haipo basi inapatikana sehemu fulani.
  Hii ndio itakavyofanya CCM ikiwa mpinzani.
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Kwanini umetaja hilo moja tu la "kuipata Ikulu"?  .
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Lazydog,
  Ahsante kwa mchango wako.
  Kama ambavyo nimeelezea kwa ufupi hapo juu ni kuwa nguvu nyingi zimekuwa zikielekezwa kukipata kiti cha urais katika chaguzi zote zilizopita. Kwahiyo nikaona nianzie hapo, lakini pia nilijaribu kugusia kwanini nguvu zisiwekwe kwenye ubunge ambapo ndiyo kwenye uwakilishi mkubwa wa wananchi?
  Hata hivyo uko huru kujadili vile ambavyo unadhani ni sahihi kwa mujibu wa mawazo yako.
   
 5. C

  Chief JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Na wewe in mmojawapo ambaye unajiuliza au?
   
 6. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii baraza iko wazi, karibu uchangie ukiwa huru.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ukweli ni Kwamba Wapinzani hawana dira hata kuliko CCM! difficult to pronounce but that is the facts
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Naam wenye dira ni chama cha mafisadi tu ambacho kimejaa wahuni, mafisadi, na walioweka maslahi yao binafsi na ya chama chao mbele kuliko yale ya Tanzania kwa kusaini mikataba ambayo haina maslahi yoyote kwa Watanzania, kukupua mabilioni ya pesa za walipa kodi na kuziweka kwenye bank accounts zao nchi za nje. Ukiwauliza wamefanya nini ambacho Watanzania wanaweza kujivunia, wanang'aa macho. Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu! :(
   
 9. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ahsante Bubu ataka kusema,
  Pamoja na maelezo yako mazuri, mimi ninafikiri ni vyema sasa tukatafuta mustakabali wa nchi yetu kwa kuchangia ni nini tunakiona juu ya mambo ya kitaifa. Sasa tunakwenda kwenye uchaguzi wa Tarime, baada ya miaka miwili na nusu duru la uchaguzi Mkuu litakuwa limerudi tena, how ready are we gonna be? Opposition waendelee kukitafuta kiti cha urais kwa udi na uvumba? au wajikite kutafuta wabunge wengi zaidi wa opposition?
   
 10. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Na wapinzani waunganishe nguvu kwanza, tatizo wengi wao wanatamaa ya madaraka. Wakigombana wako ikulu itakuwaje usalama wa taifa?
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tanzania hakuna wapinzani kuna waganga njaa tu....
   
 12. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Mimi ningepanda sana WaTanzania tukawa na fikra huru(yaani tuweze kuwa na fikra isiyoshinikizwa na jambo lolote nje ya fikra yenyewe), hilo litatuwezesha kuweza kufanya maamuzi ya busara(sina maana kuchagua upinzani ndio maamuzi ya busara maana kuna wengi humu hupenda kujaza maneno yao kwenye vinywa vya wenzao) katika kila jambo, likiwa ni uchaguzi ama utetezi wa haki binafsi na haki za kijamii na Taifa kwa ujumla wake.
  Pia tutambue kuwa UKIRITIMBA ni mfumo m-baya sana, ambao humpa nguvu aliyenacho na kumdidimiza asonacho. tujenge mazingira ambayo hakuna chama wala jamii wala kikundi cha watu watakao jiona wao ndio Tanzania na bila wao basi ni vurugu na upotevu wa amani. ni hulka ya binaadamu kujiskia pale anapokuwa na nguvu kupindukia na kuwaona wale waliomwezesha kuwa na nguvu hizo si chochote si lolote.
  tujihadhari na ukiritimba wa ccm ama chama kinginecho chochote.
   
 13. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli punda kunatakiwa kazi kubwa.

  Kwanza ni muhimu sasa ikafanyika kazi kuweka bayana ni nini tunakitaka kama taifa. Hii ndiyo iwe dira yetu ya taifa.

  Matatizo ya kuwa na chama kinatawala kinavyotaka na hakuna namna wanavyodhibitika inawezeshwa sana na kukosekana kwa dira mahsusi ya taifa. Hii ndiyo sababu hata vyama vya upinzani vinapata shida kuibana CCM. Hakuna ubishi kuwa Upinzani unatakiwa kuingia ikulu. Lakini kabla ya kuwapeleka ikulu tuwawekee majukumu ambayo watayatekeleza huko ikulu.

  Masatu anasema kuwa Tanzania hakuna wapinzani, kuna waganga njaa tu. Yeye mwenyewe kwenye status yake amejiaidentify kuwa he is fast asleep; Now that he is fast asleep how could he know as to whether there are oppositions or not?
  Keep on sleeping brother
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapana umekosea status yangu ni Im falling asleep this by miles is different from being "fast asleep"
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ni nani kati ya wapinzani na CCM ambao wan dhamira ya kuwa Ikulu?
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba CCM tayari wapo Ikulu - hili halina ubishi

  Wapinzania wamejaribu bila ya mafanikio kwenda Ikulu tangu 1995 - 2005 - hili pia halina ubishi.

  Ni kweli kuwa CCM ina wabunge wengi kuliko wale wanaotoka upande wa upinzani - Hii ni kweli

  Lakini hata hivyo vyama vya upinzani vilijaribu kupata wabunge kutoka kwenye majimbo mbalimbali - hili halina ubishi pia.

  Je, opposition waendelee kukisaka kiti cha Urais at any cost while wakiacha nafasi za ubunge zikiendelea kuzolewa kwa wingi na CCM?
   
 17. D

  Darwin JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama huyaoni yanayofanywa na wapinzani hasa kwa wakati huu. nina wasiwasi na wewe.

  Unamjua mganga njaa?

  Yeye anaangalia akipata mlo tu basi analala kama sign yako inavyosema.

  Hio Ikulu ni kama mwanamke ambaye amefikia umri wa kuchumbiwa au mwanamke ambaye keshaolewa tayari.

  Yule mhongaji mzuri, mvuto, au mwenye maneno mazuri ndio baba mwenye nyumba.

  Kama wapinzani wanamtaka huyo mwanamke [Ikulu] wataganga njaa kweli?
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tazama katiba za vyama vyote vya siasa nchini, CCM pekee ambayo moja ya madhumuni yake ni kukamata mamlaka ya dola. Hakuna dhumuni hili kwenye katiba za vyama vingine. Mpaka hapa bado unaamini kuwa primal objective ya vyama vya upinzani ni kwendq Ikulu?
   
 19. D

  Darwin JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni swali gani hili?

  CCM au wapinzani wote wana dhamira yakuwa Ikulu

  Swali lako linachekesha

  CCM ni chama tawala na kamwe hutawasikia wakiwaambia wapinzani muwe Ikulu

  Kama post yangu ya hapo juu, kila mmoja anajitahidi kuonyesha uzuri wake ili awe Ikulu.

  CCM wanataka waendelee kuwa ikulu kwasababu dhamira yao ilishatimia tayari.
  Wapinzani wana dhamira yakuwa Ikulu kwasababu bado hawajawahi kufika Ikulu.

  Kumbuka pia kwamba CCM wakiwa wapinzani watakua pia na dhamira ya kuwa Ikulu
   
 20. Lady Capricorn

  Lady Capricorn Member

  #20
  Sep 2, 2008
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapinzani wamefanya kazi kubwa bungeni awamu ya nne, wakiongeza viti bungeni labda huko mbele ya safari wanaweza wakapata majority halafu watafute urais. lakini hali ilivyo sasa, haitapendeza hata kidogo tukipata rais mpinzani kama bado ccm ina majority bungeni. Tanzania ingekuwaje leo kama augustine mrema angeshinda uchaguzi wa 1995? Hata ukimpa mpinzani maaraufu na anaependwa na wananchi wengi, utendaji ni tofauti sana na bla bla za kupinga chama tawala, na atashindwa kuturidhisha kama anavyoshindwa rais wetu wa sasa hivi. tunamatumaini ya juu sana.

  pia sidhani kama vyama vyetu vya upinzani vimekomaa vya kutosha kuendesha nchi kama executive. vyama havilingani kabisa katika sera zao wala uwezo wa kisiasa, tusiwaweke kundi moja. vipo vyama ambavyo vitakufa tu, na vingine vitaendelea kukuwa na kupata ushindi. ni juu yetu wananchi kupiga kura kwa umakini. punda milia, nadhani hiyo strategy unayoigusia ya kulenga viti vya bunge badala ya ikulu is a sound one.
   
Loading...