LazyDog
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 2,473
- 189
Wapinzani wamejaa maboriti tele. Wakutusaidia ni God tu.
Mungu akitupa huo msaada tutaweza kuutambua?
Mwaka 2005 alitupatia kiongozi kilaza ili kutupunguzia ugumu wa kufichua maovu serikalini.
Je, sababu tunazo za kushinikiza yale tunayotaka yafanyike? Katiba yetu kwa mfano, inakidhi hali ya sasa?
Kila mmoja wetu atumie nafasi aliyo nayo walau tuweze kuwa na idadi kubwa ya wabunge wa vyama mbadala 2010; labda kama hatujaona kazi wanayofanya.
Ni makosa kuketi chini tumekunja mikono kifuani tukisubiri wapinzani wafanye hiki au kile. Mwananchi anayeitakia mema familia na uzao wake ndiye mwenye jukumu. Wapinzani wasikilize kutoka kwetu na sio kinyume chake.
Kwa maoni yangu, msaada tushapewa - swali ni je, tunajua tunachotaka?
Rejea hoja ya Pundamilia07.
...Nasi tumkubali Jakaya Mrisho Kikwete kwa mapungufu yake yote, ukimya, uzembe, uvivu, uzubaaji, kutokuchangamka, kutokuwajibika na dhana kuwa analinda wale wahujumu. Mapungufu yake, ndiyo ngao na silaha yetu tuliyopewa na Mungu dhidi ya wale wenye kutaka kutufanyia dhuluma na kutuumiza.
....Kila jamii ina njia yake ambayo Mungu kawatengenezea. Njia yetu ya Ukombozi ni wakati huu wa ndugu yetu Muungwana akiwa Raisi!
Tutumie fursa hii ku....
KASOME: Thank God for Giving Us Kikwete!
.