Kwa unyenyekevu mkubwa hebu naomba ufafanue tuweze kujifunza🙏
Katika kila tendo /maisha ya mwanadamu kuna roho inayomwongoza kufanya jambo fulani yamkini ni roho chafu ambayo husimamia matendo machafu kama wizi, zinaa,ulevi ama husuda na Roho safi ambayo husimamiwa na Roho Mtakatifu mwenyewe.
Bila Shaka umeshawahi kutaka kufanya jambo ama kusikia mtu alifanya/kughairisha jambo na mabaya yakatokea:
Mfano: Unaweza ukawa unataka kusafiri unakuta kuna sauti/fikra inakuzuia na ukitii kuna matokeo utaona, ama ukifanya kuna matokeo utaona mara nyingi matokeo hasi.
Sasa basi, hakuna tendo linafanyika mwilini bila kuwa na roho.
Kama ilivyo utajiri, umasikini, uzinzi, ulevi, wizi nk zote hizo ni roho, hizo ndizo zinaamua mtu aweje na zinatoka ndani ya mtu.
Na roho hizi huenda kizazi hata kizazi; Tuchukue mfano mdogo wa Baba yetu wa Imani Ibrahimu alikuwa na roho ya utasa, alimzaa Isaka kupitia kwa Sara katika hali ya uzee kadhalika Isaka nae baada ya kumuoa Rebeka akawa hapati watoto, ikabidi aingie magotini.
Mwanzo 25:21
“Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mkewe, maana alikuwa tasa; Bwana akamkubali, Rebeka akapata mimba.”
Mtoto wa Isaka ambaye ni Yakobo aliyezaliwa pacha na Essau nae alikutana na utasa kupitia kwa mkewe Rahel ambae alimlilia mmewe kwamba nipe mtoto la sivyo nitakufa mimi.
Mwanzo 30: 1
Mwanzo 29:31
“Bwana akaona Lea amechukiwa, akamfungua tumbo lake; lakini Raheli alikuwa tasa.”
Huo ni mfano mmoja tu, ila katika familia zetu kuna roho zinazofuatilia familia ama koo, Mfano roho za magonjwa, mauti ya aina fulani kama ajali, kutoolewa, kuzalia nyumbani nk (hawa wanakuwa wamepandiwa rohonya aibu)
kujidhuru, nk.
Kikitokea watu ndo hukumbuka aaah na babu yake alikufa kwa mtindo huu ila kwakua hawana maarifa wanapuuza hadi lije litokee tena.
Hili somo ni refu sana, bahati mbaya sijajiandaa kulifundisha naomba niishie hapa, nimechukua hatua sababu umeniomba.
Naamini kuna mwanga fulani umepatikana.
Maana kuna namna ya kujitenga nazo nalo ni somo refu tu.