Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:
- Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
- Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
- Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
- Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
- Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
- Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?
Jamani wana JF swali hili ni gumu sana siyo kukimbilia kulijibu kwa vile tu tunawachukia hawa jamaa...
Siku zote katika nchi yeyote polisi ni kielelezo cha ustaarabu wa wananchi na pia uadilifu wa viongozi wa nchi
Katika kujibu hapo juu chunguza kipengele kimoja kimoja
1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold...mtakumbuka kuwa mambo hayo yote yapo juu ya uwezo
wa Jeshi hilo kutokana na mfumo uliopo, EPA - Rais aliwasamehe warudishe fedha, Dowans/Richmond baraza la mawaziri lilianguka, Kagoda imejaa siasa nyingi, Meremeta na Tangold Mh. Pinda aliapa hawezi kuzitaja,
2.Vitendo vya kishirikina alivyofanya yule mmoja kati ya wale mapacha inajulikana hata gamba limewashinda kumvua
3.Kuangamiza viongozi mashuhuri kuna siasa nyingi hapo!!
4.Kipengele No.4 USHAHIDI UNAHITAJIKA ZAIDI(
kila anayetuhumu analo jukumu la kuthibitisha)
5. Tatizo la kutoa siri ni kubwa sana hapa TZ, siku hizi siri nyigi zinavuja serikalini ndiyo maana hata habari za EPA
na nyiginezo ziliibuka hadharani( hili ni tatizo la maadili japo wakati mwingine limesaidia kufichua maovu) ila halipo kwa polisi peke yao, madaktari nao wamekuwa wakitoa siri za wagonjwa ndiyo maana watu wanaogopa kupima ngoma jirani
na wanapoishi...katika CCM, CDM,CUF zipo siri zinavuja huko kenye vyama Polisi hawapo...hili ni tatizo kubwa la kijamii linaakisi tabia zetu Watanzania kwa Ujumla. HATA HIVYO POLISI HAWANA BUDI KUONDOKANA NA LAWAMA HII WANATIA AIBU...JIREKEBISHENI HARAKA...MAKAMANDA ACHENI KUAJIRI WATOTO WENU HAWANA MAADILI
6. Hapa lipo tatizo la mafunzo wanayopata, somo la haki za binadamu liingizwe kwenye mitaala yao, aidha nafasi ya IGP iwe inathibitishwa na Bunge na aongezewe security of tenure ili asipokee maelekezo toka kwa wanasiasa bali afuate sheria bila kujali nani kakosea hata kama ni walipo madarakani washuhulikiwe kikamilifu kama wengine...