Je, umeshawahi kutoa rushwa kwakuwa hakuna uwajibishwaji wa watoa na wapokea Rushwa?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
Rushwa, iwe ya kiwango kidogo au kikubwa, inakatiza na kuzuia utawala wa sheria kutekelezwa ipasavyo. Ni kikwazo kikubwa katika utawala bora kwani huathiri sekta ya umma na binafsi na kusababisha watu kushindwa kufikia maendeleo stahiki na huduma bora za kijamii.

Vitendo vya Rushwa vina athari kubwa kwa jamii kwakuwa huwaacha watu katika utawala wa viongozi wasioaminika, na hivyo kujikuta wakikabiliwa na unyonyaji, ufisadi na huduma zisizo bora.

Kitendo cha kutumia fursa ya ofisi au mamlaka fulani kwa manufaa binafsi bila kuzingatia athari zinazoweza kusababishwa, si jambo la kufumbiwa macho.

Watumishi wa umma wanapotumia vibaya uaminifu uliowekwa kwao ni jambo linaloweza kuwahimiza wengine ndani ya mfumo kufuata njia ya ufisadi na/au kuwavunja moyo wa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu.

Ni vyema wale wanaotumia fursa za mamlaka fulani kwa manufaa binafsi wawajibishwe ili raia nao waache kutoa na kupokea rushwa kwa mazoea ya kutokuwepo hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yao.

Vita dhidi ya ufisadi ni ya kila raia. Kila hatua ni muhimu, haijalishi ni ndogo kiasi gani, inaweza kuwa hatua ya kwanza kuelekea maendeleo yenye tija.
 
Back
Top Bottom