Je, ulishawahi kuletewa pigo sizo na wageni wako? Weka mkasa wako, yangu hii hapa

Siku 2 zilizopita nilikuwa mgeni kwa mtu,siku ya kuondoka ahsubuhi sana niliingia chooni nikashusha mbolea mle.Nilipofika ubungo ndio nakumbuka sikuflash choo.Mpaka nimefika nilipokuwa naenda sijaona meseji ya mwenyeji wangu kuniuliza iwapo nimefika salama au lah na si kawaida yake nahisi kuna tatizo sehemu.
She.nz kabisa ww dah!!
imebidi nicheke bila kupenda...
 
Kwetu sisi na kama utamaduni wa Ki-Afrika(Tanzania) familia nyingi ni extended hivyo kwa upande wa familia yetu nikiwa mdogo watu wengi mashangazi,wajomba, baba wadogo,wakubwa, watoto zao n.k walipita nyumbani kwetu kwa shughuli tofauti, tofauti.

Sasa wengine wamesomeshwa na Baba, wametafutiwa ajira/vibarua pia, chakula kwetu ni first priority(Rorya) kwahiyo watu tunakula na kushiba hadi leo, Tabia hizo nimeona nyingi yaani kabla na baada ya mafanikio ya hao watu.

Kwa ufupi ni kwamba mazingira yanabadilisha watu, hasa mtu akishafika dar(mfano) na kuishi muda mrefu mfumo wa maisha ubadilika kwa kiasi fulani, unakuta mtu umepokelewa dar watu wanakulukula vibites huko kwahiyo wakirudi nyumbani hawana hamu ya kula hata kidogo, sasa kwa mwenzangu alozoea kutokuvunga kwenye msosi wewe unapika robo mchele afu njemba ni ya kanda ya ziwa huko si atakufanyia maajabu ya dunia(yaani kupiga hotpot yote na bado ana njaa pia)

Kwa kifupi nimeona watu wa tabia zote nzuri na mbaya sababu ilifika hatua mtu anarudi kijijini mwenyewe kwa aibu, sababu ameonywa muda mrefu au anaishia selo kwa kutozingatia ushauri husika, Hivyo maisha ni hayahaya ya kitanzania, tusaidiane,turekebishane na la kuzingatia ni kwamba kwenye maamuzi tufikiri kwanza ingekuwa mimi nafanya au nafanyiwa hivi je matokeo yatakuweje?

Wengine mwache uchoyo.
 
Pindi tupo home kifamilia tunaishi kwa uncle,siku hiyo uncle alikuja na rafiki yake ambae alikuwa mpole Sana umri wake ni wa Kati tuu,Ile time ya msosi si ndio mgeni akasogezewa pot la ubwabwa aanze kujipakulia,eehee bwana alichotufanyia ....!!..uncle alitamani kumwambia " na wenzio bado hatujapakua"....alijaza plate karibia robo tatu ya pot.....Kama ndio alikuwa anakula kwa Mara ya mwisho..
Nilim'mind Sana ukizingatia siku hiyo asbh nikugonga chai andazi 2 nikiwa na matumaini ya mchana ki"cover... Yaani alikichafua siku hiyo huyo mgeni.. bakuri la mboga mchuzi alijichotea Kama ye ndio alipika,hakuongea neno lolote nilikuja kumsikia akiaga....hakuna aliyemuitikia......kwa masela zaidi ya mke wa uncle....
Kama robo tatu ya chakula chote kwenye hotpot imetosha kwenye sahani moja, basi tatizo sio mgeni. Tatizo ni budget yenu!
 
Nina kesi wadogo zangu wako kusini huko wakapigiwa simu na mdogo wangu mwingine Yuko dar kwamba Kuna mgeni tena mkaka(wao ni wasichana) hana pa kufikia wampokee anakuja kuanza kazi kweli akapokelewa huu mwezi wa pili hana hata dalili za kuondoka.Kibaya zaidi ana amri "harakisheni chakula nawahi kazini" hivi napanga Safari niende nikamfukuze wao wameshindwa
Atakuwa ameanza kuwachakata
 
Sasa Mimi ndo mgeni niliyeenda kwa Shangazi yangu mkoa Fulani miaka ya nyuma wakati naenda kuanza form one nikafikia kwake.

Mda wote wa safari sikula chochote nikijua niendako ntakuta chakula niliishia kula vibites na vinywaji .Nilifika mida ya saa kumi na moja nikaoga nikakaa sebuleni nkisubiri kama kuna chochote kitu ilipofika mida ya saa mbili kasoro wakati nimekaa na aunt tunapiga story mtoto wake akaleta hotpot la chapati chai karanga na ndizi nne make mle ndani walikua watatu na Mimi wanne.

Ndo Shangazi akasema "endelea tu mwanaume "wengine wote walikua wadada bas bwana mwanaume bila kujua kwamba huo ndo mlo wa usiku na ndo chapati za watu wote mzee baba nikala chapati 5 kati ya 8 ndizi 3 kati ya nne na karanga karibia zote nikisubiri mlo wa usiku.

Kumbe nilowatia hasara picha nilianza kulisoma alivyokuja cousin alilopoka akauliza kama wengine washakula kumbe mzee nshawapiga 5-1 asee iyo siku sitaisahau kwanza aibu njaa ilianza kuniuma kabla hata sijaenda kulala make apo kati kulikua na kipindi cha maombi mazito kusifu na kuabudu usipime.
😂😂😂😂
 
Kuna chalii yangu tulisoma nae chuo, siku moja akaomba kufikia gheto kwangu maana alikuwa mkoa tofauti na alikuwa amekuja kufuatilia mishe za ajira. Gheto langu ni chumba kimoja tu na sebule na choo/bafu ndani, sasa kimbembe Kesho yake asubuhi aliamka mapema kabla yangu akaingia kuoga, dah mwamba katoka bafuni namcheki ametengua taulo langu anajifuta fresh tu mpaka matakoni, bafuni katumia mswaki wangu na ninao mmoja tu huo huo, mlango wa bafuni hafungi then kashusha mzigo huko harufu inarudi room yote yaani ni kama mtu ambaye hana ustaarabu kabisa, Malapa ya bafuni anazunguka nayo mpaka sebuleni na yana maji maji aiseeee!!!! Nikashindwa vumilia nikamchana live kuwa asepe siku hiyo demu wangu anakuja kulala baadaye usiku! Kama ana akili alielewa


Hadi mswaki wako akatumia huyo jamaa ni wawapi mbona anatisha😀😀
 
Walikuja wageni kwangu nikawachinjia kuku kumbe bwana ni Waislam (nilikuwa na najua ila sikutilia manani ishu ya kuchinja) alooo si wakanizilia makuku yote mawili mimi na familia yangu wakaamua kula mchicha nikajifanya sielewi tulikula kuku wenyewe wakala michicha, yaani mi ninunue kuku wawili then nielekezwe nani wa kuwachinja utafikili wakichinja Waislam wataongezeka mapaja na hipsi.
Kikawaida waislamu wameruhusiwa kula chakula chochote kitakachoandaliwa na ahlul kitab(wakristo ni ahlul kitab) ispokuwa tu kisiwe katika vile walivyokatazwa mfano nguruwe.
Hao walizingua pakubwa mnoon,unaachaje kuku kwa mfano?
 
Kuna kipindii home alikuja binamu alikuwa anasumbuliwa na tumbo sasa akawa ana enda pale kcmc miaka hiyoo kwenda kuchomelewa...
(Mionzi)

Sasa kila akija nilikuwa siruhusiwi kulala kitanda kimoja na yeye mimi walikuwa wananitandikia chinii..

Sasa alikuwa anamtindo ana amkaa usiku ananichapa kuwa nikakojoee au ananichap niende ku mwagilia vitu mapema na hapo ni usiku kama saa 10.

Nika mwambia mama ila alipuuzia na kusema ndo unatakiwa uamke mapema nikaona hii kesii...

Sasa kama asipo nipiga usiku kwenda kukojoa basii ata nipiga kwenda ku mwagilia mfano akaniamsha nika mwbia kuwa sina mkojoo utasikia jiandaee uka mwagiliee bustanii (mchicha tuta kama 14,ma papaii, migomba, mauwaa, chainise .nk)

Ikafikia kipindi ikawa kero mpaka naota usiku kuwa napigwa. Nikaona isiwe kesiii nika chukua hatua moja tamu sana.

Nikatandika shuka kwenye uvungu anao lala so ikifika usiku saa 6 naingia nalala kwenye uvungu mwisho akiamka anakuta hamna mtu anajua dogo sasa kashazoea kumbe niko uvinguni nimelala..

Sasa wakati wa kuamkaa huwa nipo karibu na mlango so akienda chooni/nje mimi na nyata natoka naenda chumba cha maza kumsalimia natoka nje kufungulia mbuzii..

Niliishi hivyo mpaka jamaa akasepa. Ila walikiwa wanaulizaa mbona una amka mapema na mashamba makavuu nikawa najitetea tu nilienda kukimbia mpaka uwanjanii..

Sent using mt4 app
 
Back
Top Bottom