Je, ulishawahi kuletewa pigo sizo na kinyozi, weka mkasa wako

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Nakumbuka nywele zilikuwa nyingi sana hadi ikawa kero, nilipopata muda jioni ikabidi niende mtaani kunyoa,

Kinyozi alikuwa kavaa kiheshima na yeye kanyoa kiheshima nywele zake, hakuuliza ninyoe vipi ila kwa muonekano wake nikajua ataninyoa kawaida, ila kulikuwa hakuna kioo.

Eeeh, kamaliza ndo kanipa kiooo nijicheki, Yesu Maria na Yosefu!! yani kichwa kimegeuka kuwa kama kitunguu, kaninyoa kiduku kile cha vibaka !! na hapo ikumbukwe nina mke, watoto, ninafanya kazi serikalini,

yani tulizinguana sana sio kidogo, ilibaki kidogo nimpige ngumi ya uso maana nilikasirika sana.

ilibidi tu nisepe hapo nikavaa kofia mpaka nlipofika kwa vinyozi wanaojielewa nikapigwa upara maana style aliyoninyoa yule bwanza huku pembeni alipiga upara kabisa juu akaziacha.

Kuanzia siku hio kila nikienda kwa kinyozi lazima niwaambie wanyoe vipi
 
Pole Sana mkuu,Mimi toka nianze kunyoa huwa nanyoa kawaida tu Wala sio mtindo,ndio maana huwa wananinyoa vizuri.
 
1. Hukumpa maelekezo vizuri,
2. Aliona nywele zilizoota ni matokeo ya kiduku cha mwanzo
3. Aliona kichwa kimekaa ki kiduku kiduku akatimiza maandishi.
4. Aliangalia muonekano ulioenda nao, akajua ni wale wale,
5. Alipenda tuu akuone umenyoa kiduku,
6. Alikosea kukunyoa pembeni, akaona kuliko para bora kiduku,
 
Kuna jamaa alienda kunyoa akiwa na mtoto walipo fika saluni akaanza kunyolewa jamaa alipomaliza akamwambia kinyozi endelea kumnyoa mtoto anaenda dukani mara moja narudi. Jamaa akasepa bila hata kulipa kwa kuwa alimuacha dogo pale, kinyozi alipo maliza kumnyoa dogo walimsubiri jamaa sana lakini hakurudi, kinyozi akamuuliza dogo vipi mbona baba yako harudi? Dogo akamjibu yule sio baba yangu wala simjui alinikuta tuu akaniambia twende tukanyoe bure.

Wewe kama kinyozi ungefanyaje.
 
Kuna jamaa alienda kunyoa akiwa na mtoto walipo fika saluni akaanza kunyoa jamaa alipomaliza akamwambia kinyozi endelea kumnyoa mtoto anaenda dukani mara moja narudi. Jamaa akasepa bila hata kulipa kwa kuwa alimuacha dogo pale, kinyozi alipo maliza kumnyoa dogo walimsubiri jamaa sana lakini hakurudi, kinyozi akamuuliza dogo vipi mbona baba yako harudi? Dogo akamjibu yule sio baba yangu wala simjui alinikuta tuu akaniambia twende tukanyoe bure.

Wewe kama kinyozi ungefanyaje.
Kinyozi anasamehee amna namna apa anajifunza siku nyingine pesa mbele alafu huduma inafata
 
Hii chai hii. Inawezekana vipi saluni kusiwe na kioo. Kinyozi gani uende kunyoa mara ya kwanza asiulize unanyoaje?
 
Kuna jamaa alienda kunyoa akiwa na mtoto walipo fika saluni akaanza kunyolewa jamaa alipomaliza akamwambia kinyozi endelea kumnyoa mtoto anaenda dukani mara moja narudi. Jamaa akasepa bila hata kulipa kwa kuwa alimuacha dogo pale, kinyozi alipo maliza kumnyoa dogo walimsubiri jamaa sana lakini hakurudi, kinyozi akamuuliza dogo vipi mbona baba yako harudi? Dogo akamjibu yule sio baba yangu wala simjui alinikuta tuu akaniambia twende tukanyoe bure.

Wewe kama kinyozi ungefanyaje.
Asee Bongo watu wanaishi kiujanjaujanja sana 😂😂😂
 
mimi nakereka saluni unakuta kuna washkaji wengine wamekaa sio vinyozi wala nini,wanapiga story na kinyozi mpaka ufanisi wake unakuwa mdogo,halafu wanakuangalia usoni kila hatua unayopitia,kama wanakariri sura yako.
 
Back
Top Bottom