Je, ulishawahi kuletewa pigo sizo na wageni wako? Weka mkasa wako, yangu hii hapa

Kuna shemeji zangu nimewaunganisha kazi sehemu wao wakirudi toka job wanasalimia na kukaa nje eti ndani joto msomi ukiiva wanakula na kusepa hata kijiko hawakoshi alafu ni swala tano. Juzi kati nimenunua pork wakafika wakakuta anakaangwa wakasema nyama gani mbona inanukia vyema nikawatajia wakasepa hadi leo, raha ya kula ni kuosha vyombo ishu ilipelekwa kwa dada yao mtu akiumwa anataka umpeleke hosp na kumlipia tiba, maji ya kunywa safi dumu Tsh.2,000/- hawanunui wakikuta kwangu wanabeba nikabadili kitasa nimeoa dada yao siyo ukoovy mjini bajeti
Sasa wataoshaje vyombo wakati dada yao yupo?
 
Nilipata ugeni wa single mother alikuja na mwanae getto asubuhi kaamka anafanya usafi kumbe alimuacha mwanae kitandani bila nguo nashituka naona dogo anakunya na kukojoa juu ya godoro nilitaman nishushe vitasa kwa dogo bahati mama ake akaingia toka siku hiyo lile godoro sijawahi kulitumia tena .shikamoo mlioko kwenye ndoa na mna watoto
 
Ilikuwa jumamosi majira ya mchana nimetulia zangu nikaanza kutafuta majina ya kufuta kwenye simu yangu.

Katika kupekua majina nikakuta jina moja jamaa hatujaongea miaka kadhaa nikampigia nijue kama ipo hewani au nifute. Turns out nae kumbe yuko mkoa niliopo kipindi hicho.

Nikamwambia aje ninapoishi tupige story.

Siku ya kwanza akaja tukapiga story jioni akaniambia yuko broke nikamtoa nauli na hela ya akiba siku mbili tatu.

Mara ya pili kaja tukapiga story na misele kadhaa, akalala kesho yake akasepa.

Mara ya tatu akahamia kabisa ile kimya kimya siku zinaenda hana mpango wa kusepa, sikuona tatizo sababu najua nini maana ya kukosa au mambo kwenda vibaya.

Shida ilianza jamaa akawa hataki kufanya chochote yeye akae tu, kila kitu nifanye mimi, ukimwambia jamaa ananuna balaa siku nzima hakusemeshi na hakujibu.

Unaenda mishe, unarudi unafikia kuanza kupika na jamaa kalala tu ukimuamsha anajifanya kasinzia ila ukiivisha anaamka.

Ikatokea nimefungua biashara mkoa mwingine inabidi niende halafu dogo aje kusimamia hii ya huu mkoa niliokuwa naishi.

Basi nikahamia mkoa huu mpya yeye bado yupo geto, madogo wakaja akawa anakaa nao. Wiki haijaisha wanalalamika jamaa analeta kisirani mbaya, hataki kufanya kazi yoyote ila muda wa mpira anaomba hela akaangalie mechi

Nikamwambia njoo huku nilipo mimi, nakupangia chumba miezi 3 baada ya hapo utakomaa kiume, nakupa na godoro wewe tafuta akiba tu ya kuanzia uje.. Jamaa ananipiga chenga mara sijapata hela, mara nataka kurudi mkoa ila haondoki wala nini.

Siku dogo akamuomba akae dukani kidogo ili akafunge mzigo, bahati mbaya akachelewa kidogo, aisee jamaa akakasirika balaa amecheleweshwa mechi kakosa kipindi cha kwanza, na bado hela ya mpira akaomba.

Dogo akamwambia hela sikupi, kila siku unaomba hela ila hutaki kufanya chochote na bado unaleta visirani kila muda umenuna hatuna hata amani.

Jamaa akakasirika, akasepa bila kuaga na akatublock wote kuanzia mimi hadi madogo.

Kaja kunitafuta baada ya miezi kama sita au saba hivi, namuuliza uko wapi anasema nilirudi home kwa wazazi.
Kwa wazazi? Najua maisha magumu ila kwa wazazi? 30 yrs unarudi kwa wazazi?

Nikajisemea tu hili litakuwa ndio lile sikio la kufa ambalo wahenga walilisema.

Ulikuwa na moyo aisee kumvumilia siku zote hizo
 
Dah hatari sana hii. Hebu malizia mkuu, ilikuwaje alirudi au?
Hakurudi tena mkuu,
,ilikuwa ndy ticket ya kutokomea kusikojulikana.

Maana alipokuja kwngu hakuja na chochote zaidi ya kifuko cha Marlboro,
Ambacho kulikuwa na nguo mbili tatu tu.

Kwa kifupi mwamba alinijia Kwa mission maalum.

Ilipita miaka tukajaonana tena ila nilishapotezea Jambo lile.
 
Ilikuwa xmas tukaalikwa na familia nyingine kwa ajiri tusheherekee wote sasa wakati wa chakula nilitoa boko nilipakua msosi mwingi sana hadi nikashindwa kumaliza daa nliona aibu sana
 
Back
Top Bottom