Je ulipokuwa mdogo ulitamani kufanya kazi gani ukubwani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,833
Mimi niliharibiwa sana na kitabu cha PANGA LA SHABA na mwanae UFUDU.
Nikatamani na mimi nikiwa mkubwa niwe mganga wa jadi ili nikamate wanawake wazuri na nipate mahela.
Ila nilikuwa naogopa sana kula panya na nyama za watu.
kila kilichoa andikwa kwenye kile kitabu nilikuwa naona ni ukweli mtupu.

544874_300611983358085_100002278567469_648884_1043957698_n.jpg


Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila mwenye umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma mwenye umri wa miaka 20 (mwanaume) ambao walitambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha,walikamatwa jana majira ya saa 12 asubuhi katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.
 
Bujibuji kusema ukweli namshukuru Mungu kwani tangu kinda nilikuwa natamani sana kuwa Balozi wa Kiswahili ktk Shule za Msingi na Sekondari.
Nashukuru Mungu kazi niliyoiotea,imetimia.
 
Last edited by a moderator:
pasi na shaka nilitamani sana kupiga soka kama Lunyamila,lakini shule ikapeperusha ndoto zote hata danadana 10 sifikishi
 
Bujibuji kusema ukweli namshukuru Mungu kwani tangu kinda nilikuwa natamani sana kuwa Balozi wa Kiswahili ktk Shule za Msingi na Sekondari.
Nashukuru Mungu kazi niliyoiotea,imetimia.

kumbe.!! hongera yako banah..
mi nlitamani kuwa mfalme, sa sijui niahirishe au niendlee kustrugle maybe siku mambo yatajipa
 
Last edited by a moderator:
kumbe.!! hongera yako banah..
mi nlitamani kuwa mfalme, sa sijui niahirishe au niendlee kustrugle maybe siku mambo yatajipa

Wewe mtoto Junior. Cux,
mambo yatajipa lini?
Ila cwez jua mana kila sehemu kuna mfalme wake,
Mambo yetu yale,Jikoni,Vibarazani,Uani n.k,
Jitahd sehem mojawapo utapata Award.
 
Last edited by a moderator:
Tobaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa......

Marinda ya sketi au????

BT ! Mbona umenimaka, hadi nimekua mpole ?
Kioja ki-wapi ?
Nani asoyajua marinda hapa jamani ?
Kwani we wayajua marinda ya aina ngapi ?
Hadi uulize ni ya Sketi au ?
Hembu nitajie aina uzijuazo, then ndo namie nikujibu!
 
nilikuwa napiga ball kinoma kila mtu alijua ntakwea pipa lkn baba alipenda nipige kitabu zaidi na nilimtii mzazi wangu.
 
nilitamani kuwa dakitari lakn nilipoteza matumaini f6 baada ya kudanganywa na washikaji na kukimbilia uhasibu! ningefanyaje maoparasheni hapo muhimbili!
 
Nilitamani kuwa Mkurugenzi wa fedha na utawala wa BOT nisimamie ujenzi wa majengo pacha!
 
Pilot, nilikuwa naona wana raha sana.

Ndo maana hadi leo nafurahi kukaa kimya tu nikitazama mawingu.
Huwa naona movies nyingi sana kwenye mawingu meupe.
 
nilitamani niwe rubani na nikaenda kusoma PGM A-level, ila ukosefu wa chuo cha kufundishia urubani hapa nchi ya makenge(Tanzania) ndio ulunionza.
 
pasi na shaka nilitamani sana kupiga soka kama Lunyamila,lakini shule ikapeperusha ndoto zote hata danadana 10 sifikishi

Comment yako imeniuma sana watu8, hata mimi nilitamani niwe mwanasoka, inspiration kubwa ilikuwa timu yangu ya kitaa, Texas Dume, ila ndo ivo, ukiamua kusoma hakuna soka.
Ila angalau huwa nacheza mazoezi na maveterani pale uwanja wa shule.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom