Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
17,135
40,702
Habari ya weekend great thinkers?

Maisha yananipa experience tofauti, Sikuwahi kufikiria kama ningefika third floor bila kuwa na familia wala watoto, kuna muda nahisi kupanic nahofia watoto wasije kuniita bibi badala ya mama, au kukosa kabisa sababu ya umri mkubwa🤔

Enzi hizo nilikua nashangaa mtu hasa mdada unafikaje hadi 30s huna familia, aisee kumbe ni kweli now ni mimi mwenyewe.

Mlioanza familia mkiwa 30s je ni kweli au mnaona dalili za watoto wenu kuwaita bibi au babu? Vipi changamoto za uzazi sababu ya umri mkubwa?😔

Nipo tayari kwa comments zote.

Happy valentine's day in advance 👏🥰
 
Acha uchaguzii saanaaa....chances zinapungua sanaaa.....watu pia wanaisha ...utalea Serengeti boys....tafuta mtu kawaida tuuu malizana pambana watoto....avhana handsome six pack ujinga mwingi theories.....hao huwa hawapo pia wao wanafata simple girls ndio wanaoa...moto na moto huwa haviendiio
 
Habari ya weekend great thinkers?

Maisha yananipa experience tofauti, Sikuwahi kufikiria kama ningefika third floor bila kuwa na familia wala watoto, kuna muda nahisi kupanic nahofia watoto wasije kuniita bibi badala ya mama, au kukosa kabisa sababu ya umri mkubwa🤔

Enzi hizo nilikua nashangaa mtu hasa mdada unafikaje hadi 30s huna familia, aisee kumbe ni kweli now ni mimi mwenyewe.

Mlioanza familia mkiwa 30s je ni kweli au mnaona dalili za watoto wenu kuwaita bibi au babu? Vipi changamoto za uzazi sababu ya umri mkubwa?😔

Nipo tayari kwa comments zote.

Happy valentine's day in advance 👏🥰
Duuh wee muoga wewe...🙌😂

Si bado unachagu chagua.!!

Bado hujasema....
 
Nakuelewa sana.

Maisha hatufanani mazingira.

Wazazi wametuachia vijana jukumu kubwa hili la kutafutana mke na mume kwenye dunia iliyochafuka. Washenzi wengi kuliko wastaarabu. Chuo ni sehemu nzuri sana ya kupata mwenza. Shida ajira siku hizi tunachelewa kuzipata na bila ajira kuoa ngumu maana tunatokea familia maskini. Hivyo spouse wa chuo hamtoboi..

Kuna watu wanakulia mazingira ambayo wanapata spouse kwa jirani zao tu nyumba ya pili

Kuna watu wanapata ajira zinazowafanya wawe wanakutana na watu wengi wapya wanaotafuta wenza kila siku yao ya kazi.

Mwanamke mstaarabu na mwanaume mstaarabu kukutana ni ngumu sana zama hizi kama sio majirani, ama hamjasoma shule ama chuo pamoja.

Nje ya hapo hata mkikutana mnakuwa hamna imani maana hamjuani. Kitu kidogo tu mnaachana
 
Speaking from personal experience..
When approaching 30s kweli pressure ilikua just sana. And I always had a vow kua nkifika 30 I'm gon have a family regardless of my financial status.
By 29, hakuna ramani ilikua inasoma. I told my girlfriend, darling, we need to have a baby,. Akashangaa. Nkamwambia, life ni tight, yes sina life poa sana but sasa hv ndo nina nguvu
Alikataa, baadae around 31 huko akakubali, kimbembe kikaja hakukua na mimba. Tried a whole year b4 bein succesful.
to be honest, with time you get used to it, but mtoto anakupa changamoto ya kupambana zaidi. Every day I wake up at 5 a.m and my little girl anakua macho pia, we have our moments n I leave kwenda kwenye harakati. Its a good feeling wouldn't trade it for nufn.
So financial services, don't sweat it. Cha muhim upate the right person, ul never feel like you are late, it will be a start to the best chapter of your life
 
Kuna kitu nahitaji kuwafunza mabinti ambao hawajafika 30.

Ukipata mpenzi ukamuona ana hofu ya Mungu, maisha yake yapo wazi hasa tabia zake, anakupenda kwa dhati, yupo tayari kukutambulisha kwa ndugu zake na kwa familia yake.

Yamkini asiwe na kipato kikubwa sana ila ana uwezo wa kufanya wote mle na mkalala, ISHI HAPO.

Acha tamaa za kutaka uolewe na mwanaume mwenye pesa, anayefanya kazi TRA, bandari, mfanyabiashara mkubwa, mwenye muonekano fulani n.k mwisho mtakuja kuangukia kwa wanaume za watu au kwa wanaume ambao wataishia kukuchezea. Kumbuka sehemu kubwa ya mwanaume mwenye pesa, ngono anachukulia starehe tu, kwahiyo atakuchukua na kukutumia baada ya kukutamani akijua anapiga na kupita zake.

Binti yangu, huyo mwanaume wa mtu unayemuona ana pesa, hazijaja tu hivi hivi, alianza chini kabisa kama huyo kijana ambae kwa sasa wewe unamdharau.

Kama umewahi kumnyanyasa kijana wa watu kisa masikini, yeye sijui hana umbo zuri n.k moyo wake ukaumia, katafute suluhu naye sababu huenda kuna mambo yako yakafunguka.

Mabinti sio kwamba mnakosa watu wa kuwaoa ila tamaa za maisha zimekuwa zikiwatesa wengi, (kumbuka Hawa alidanganywa kwa kutamani pale bustani ya edeni, mwanamke ukiishinda tamaa una sehemu kubwa sana ya kuishi maisha ya furaha duniani). Mnapenda smartphones, kila wiki msuke, utolewe out n.k mnaishi maisha ya udangaji kisa mna uzuri wa sura au mna matako makubwa, kwa bahati mbaya sana, ukishazoea kudanga, mwanaume yeyote atakujua tu, udangaji ni kama ngozi, HAIJIFICHI na hata ukijitahidi, mtu atasikia tu stori zako.

Sasa hivi kijana wa 30, 31, 32 ambapo kwa sehemu kubwa ndo vijana wengi walau kwa sehemu wanaanza kuona mwanga ktk eneo la uchumi hawezi kuwa na mwanamke wa 30, lazima atafute wa 24, 25 au 26 unless awe mpumbavu.

Girls kuweni makini sana na umri, uliowatupa kisa hawana ela, wakipata ela na wao watakuona wewe sio hadhi yao. Tafuta kijana mwezio mtakaopendana, mtie moyo ktk utafutaji, mpende sana na kumpa heshima hata pale ambapo anapungukiwa, mwanaume huyo hatokusahau.
 
Back
Top Bottom