Je, Ukosefu wa fedha ulishawahi kukudhalilisha? Share experience yako

safi ".... but trust me " ukija kuoa huyo mke wa pili " ndio utakuja kuwa mwanzo wako wakuyumba kimaisha " iwe kiuchumi " au kimahusiano " ya kijamii na ki-familiar "... sikutishi " but utakuja kukumbuka haya maneno Yangu ... mkeo anatokea mkoa gani Aisee namimi unitafutie Mke huko...??
Bora umemwambia mapema....
 
Kapata mke mwema huyo, badala ya kuenjoy amani waliyonayo anataka kualika vita ndani. Uke wenza si jambo rahisi kama wanaume wengi mnavyolichukulia
Naaam mkuu "... tatizo sisi vijana huwaga tunajisahau mnooo " na kuzifikiria nafsi zetu zaidi kuliko za binaadamu wenzetu ".... jambo baya usilopenda kufanyiwa " jitahidi kujizuia na wewe usijekumfanyia mwenzio
 
Mimi Kuna mwanaume nimekaa nae kama wewe hivyo. Nimemvumilia sana zaidi ya miaka Saba. Nikawa namwomba basi nitambulishe Hata kwa kwa wazazi tu. Me ntaridhika.... Me nimekukubali Jinsi ulivyo japo Huna pesa...
Kila siku ananipiga chenga tu.

Nimeamua nijiongeze nimemwacha, sasa analalamika na kunipa laana juuuu. Sasa Nashindwa hata kumwelewa.
Kama mda kanipotezea sana. Sijui anataka nizeeke kwake aje aoe mke mwingine na mimi aniache...


Ila ipo siku atanikumbuka tu.
Sio kwa kumlamba miguu vile japo hata utambulisho wa uongooo tu alishindwaaaa...
Wanaume nyinyi hapana asee.
Ila kwa moyo safi nimemsamehe bureee, Ili baraka zangu zifunguliwe...

Nilimwambia neno moja tu. IPO SIKU NAMI NTAJESHIMIKA,ila sijui ni lini..
Inakera sana
 
Siku hiyo na nauli tu ya kwendea kibaruani ,kurudi Mungu atajua .Gheto nimetoka nimekula mahindi makavu (ili kuleta ladha nimeyakaanga na chumvi).Nimefanya kazi yangu jion nijirudishe kwenye kiota.Nikajaribu kutembea kwa miguu kilometer kadhaa nikaona hali tete,nikaamua liwalo na liwe nikamfata jamaa mmoja ,nikamuimbisha na porojo nyingiii jamaa wacha aanze kupayuka shombo ,nikaona sio case .Nikasali kimoyomoyo Mungu naomba nitakayekutana nae anisadie nauli tu Amina.Nikakutana na dogo anauza matunda mengi yalikuwa ndizi ,nimemuelezea ukweli wangu ,kanipa elfu2 na ndizi.Bahati mbaya sijamuona tena.Umasikini wa kuwaza chakula na nauli nshauvuka .Asante Mungu.
 
safi ".... but trust me " ukija kuoa huyo mke wa pili " ndio utakuja kuwa mwanzo wako wakuyumba kimaisha " iwe kiuchumi " au kimahusiano " ya kijamii na ki-familiar "... sikutishi " but utakuja kukumbuka haya maneno Yangu ... mkeo anatokea mkoa gani Aisee namimi unitafutie Mke huko...??
Bora umwambie
 
Hili tukio ni la juzi kati tu (mpaka sasa sina hela).
Ninataka kuingia na na dem gest mfukoni nina elf 15 tu picha linaanza dem anataka kula nikimuuliza anataka nini akasema chips yai..

Basi hapo hapo guest kuna kisehemu wanauza chips tukaenda kupata chips..
Akaagiza chips na soda na mimi nikaagiza hivyo hivyo.

Baada ya kula nikatoa elf 10 nikarudishiwa elf 4...ikabidi nimuulize jamaa imekuwaje wananipa buku 4 badala ya buku 5... akasema soda ni buku 1...

Hapo mnyawezi plani zangu zikawa zimeyumba maana mfukoni nikabaki na elf 9 wakati kiingilio cha guest ni elf 10..

Ikabidi niingie hivyo hivyo tu lakini akilini niko napanga mbinu zangu za kivita za kuingia gest kwa elf 9..

pale kaunta nikawaambia wanionyeshe chumba kwanza ndio nilipe waliponinyesha chumba nikamwambia yule dem aingie kwanza room mimi nikamalizie malipo counter fastaa. Dem kaingia chumbani mimi na muhudumu tukarudi kaunta kumaliza malipo tulipofika nikatoa buku 9 niliyokuwa nayo ...muhudumu akagoma..nimembembeleza hadi kidogo nipige magoti hadi akakubali..

Nikarudi room nikamkuta yule dem yupo katulia tu ile nataka kuanza mambo yangu ya kuvunja ile amri pendwa no 6. Manzi anaanza kugoma goma..nikajua hii ni danganya toto tu ...
Lakini huwezi amini hadi naondoka mule mzigo SIKUPATA anasema alikua yuko MP...

Mfukoni nilikua sina hata 100 ya nauli na hapo yule dem ananiomba nauli..

Nilimchenjia fastaa nikamwambia kama vipi tuachane tu (hapo ilikua ni defence mechanism maana sina hela ya nauli aliyoniomba) nikaondoka kwa hasira.

Balaa likaanza la kurudi gheto kwa miguu nimetembea kuanzia saa 11 jioni hadi saa 3 usiku ndo nafika home nimechoka nakuta home maji hakuna nikalala njaa (nilishindia chips ile niliokula mchana)



MJINI USIOMBE UKAWA HUNA PESA UTAPATA TABU
Hii kweli mbwa kala mbwa :):)
 
Mimi Kuna mwanaume nimekaa nae kama wewe hivyo. Nimemvumilia sana zaidi ya miaka Saba. Nikawa namwomba basi nitambulishe Hata kwa kwa wazazi tu. Me ntaridhika.... Me nimekukubali Jinsi ulivyo japo Huna pesa...
Kila siku ananipiga chenga tu.

Nimeamua nijiongeze nimemwacha, sasa analalamika na kunipa laana juuuu. Sasa Nashindwa hata kumwelewa.
Kama mda kanipotezea sana. Sijui anataka nizeeke kwake aje aoe mke mwingine na mimi aniache...


Ila ipo siku atanikumbuka tu.
Sio kwa kumlamba miguu vile japo hata utambulisho wa uongooo tu alishindwaaaa...
Wanaume nyinyi hapana asee.
Ila kwa moyo safi nimemsamehe bureee, Ili baraka zangu zifunguliwe...

Nilimwambia neno moja tu. IPO SIKU NAMI NTAJESHIMIKA,ila sijui ni lini..
Mkuu

Bado eneo lako lipo wazi au limeshapata mwekezaji ?
 
Niliwahi muacha mtu sababu hakua na pesa ingawa alikua na mapenzi ya kweli..sitasahau nilivyomjibu ovyo pande za mwenge kwa wauza chips....alafu sikujali hata hadi rafiki zangu walijisikia vibaya...ulikua ujinga wa pesa
Vipi huku Omba mrudiane
 
Hahaha sasa Mazingaumbwe ukose ww ...mwalimu akupige ..ila shule za msingi zilikua na uonevu sana
Yaani kosa langu lilikuwa kuingia kwenye mazingaombwe kwa kupitia dirishani kiwizi kwa sababu sikuwa na hela ya kulipa kiingilio mlangoni. Kwa kiswahili cha miaka hiyo nilizamia.
 
mi bado sijapata pesa nzuri ila nashukuru maisha yangu wamekuwa ya kawaida sana sijawah pata adha ya kudharaulika

ila kuna dogo mmoja nakaa nae jirani, umri namzidi alikuwa ananisimanga kukaa na wazazi umri ukiwa umeenda. huyu bwana nikimuona huwa nacheka maana yeye karudisha mpira kwa kipa mimi najitegemea
 
Siwezi kusahau siku niliyozabwa kofi la nguvu sana sikioni na mwalimu mkuu wa shule yangu ya msingi mbele ya wanafunzi wote hadi nikaanguka chini huku nikihisi sikio kuziba. Hii ilinitokea nikiwa darasa la nne baada ya kuwa nimekosa hela ya kiingilio cha kuangalia mazingaombwe na mimi nikawa nimerukia dirishani ila bahati mbaya yule mwalimu akawa ameniona. Nilikuwa mdogo lakini hilo tukio lilinifedhehesha muda wote hadi nilipohama shule hiyo nikiwa darasa la sita ndipo nikapata nafuu.
Ahahaaahaaahaaa hii ikua fundsho kwa wengne wenye tabia ya kupga chabo
 
Back
Top Bottom