Je, Ukosefu wa fedha ulishawahi kukudhalilisha? Share experience yako

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Maisha ya sasa ni maisha yanayobadilika kwa kasi sana.Pesa imekua suluisho na kipaumbele kikubwa katika maisha yetu ya kila siku.
Ukija kwenye mapenzi ndio kabisaa hakuna Binti anaweza kukuelewa kwa lolote bila kuwa na Pesa mfukoni.

Naelewa ukiwa kama Mwanaume umeshapitia mazingira fulani ya kudhalilishwa na mwanamke wake kisa pesa ,either kukataliwa,kusalitiwa au kukanwa mbele ya watu kabisa,inaweza ikawa si mapenzi tu ila kwa namna moja pesa inaweza ikawa imeshawahi kukuletea aibu fulani katika mazingira fulani.
Share nasi ni kwa namna gani fedha imewahi kukuletea fedhea .

Vile vile kwa Wanawake mnaweze kushare nasi namna mvilivyowakana na kuwasaliti watu wenu wasio na pesa au walioshiwa gafla , au ni kwa namna gani fedha ilikufanya utoe utu wako kwa ajili ya kupata kitu kama kazi ,nafasi kazini,cheo na mambo kadha wa kadha.

Experience make a person better.

#share .
 
Mmmmhh!! Nimekumbuka mbali sana kipindi hiko na kademu kangu baada ya kumaliza chuo yeye alipata kazi kwanza mimi nikawa bado, dah ama kweli kufika kazini huko akaanza dharau kweli kweli na mimi matusi mpaka mengine nilikua siyajui natukanwa kisa sina kazi lakini Mungu si athumani nikapata kasehemu nikajibanza huku yule dada kazini kwake kukiwa kumedorora (kampuni ilifilisika) basi mpaka sasa ananitafuta huku nafsi inamsuta mimi sina kinyongo nae ila kwa sasa acha mama abadili vitenge kwanza na mwenye masikio na asikie
 
Hii inaitwa what goess arounds comes around.
 
Siwezi kusahau siku niliyozabwa kofi la nguvu sana sikioni na mwalimu mkuu wa shule yangu ya msingi mbele ya wanafunzi wote hadi nikaanguka chini huku nikihisi sikio kuziba. Hii ilinitokea nikiwa darasa la nne baada ya kuwa nimekosa hela ya kiingilio cha kuangalia mazingaombwe na mimi nikawa nimerukia dirishani ila bahati mbaya yule mwalimu akawa ameniona. Nilikuwa mdogo lakini hilo tukio lilinifedhehesha muda wote hadi nilipohama shule hiyo nikiwa darasa la sita ndipo nikapata nafuu.
 
Mmmmhh!! Nimekumbuka mbali sana kipindi hiko na kademu kangu baada ya kumaliza chuo yeye alipata kazi kwanza mimi nikawa bado, dah ama kweli kufika kazini huko akaanza dharau kweli kweli na mimi matusi mpaka mengine nilikua siyajui natukanwa kisa sina kazi lakini Mungu si athumani nikapata kasehemu nikajibanza huku yule dada kazini kwake kukiwa kumedorora (kampuni ilifilisika) basi mpaka sasa ananitafuta huku nafsi inamsuta mimi sina kinyongo nae ila kwa sasa acha mama abadili vitenge kwanza na mwenye masikio na asikie
 
Yasikie kwa watu. Niliingia na demu Mazembe guest house Tabata karibu sana na mataa kama unakuja Azam tv. Ile nimemaliza kuvaa ngao demu kaniambia nipe changu kwanza. Mfukoni nilikua na buku 2 nauli ya kurudia. Nilimuona abdala kichwa wazi akisinyaaa ndani ya vazi rasmi la kivita. Sikua na lakufanya ila kuvaa suruali na kuwahi daladala la Ubungo.
 
Mimi napitia hali hiyo mnayosimulia kwa sasa lakin ukiniona niko na furaha sana, majaribu nimeyachukulia positive. Mungu ananiandaa kwa ajil ya mambo makubwa....... Simu nikipiga hazipokelewi hata kwa ndugu wa karibu saa nyingine, wanahis nitakuwa naomba misaada tu
 
Maisha ya sasa ni maisha yanayobadilika kwa kasi sana.Pesa imekua suluisho na kipaumbele kikubwa katika maisha yetu ya kila siku.
Ukija kwenye mapenzi ndio kabisaa hakuna Binti anaweza kukuelewa kwa lolote bila kuwa na Pesa mfukoni.

Naelewa ukiwa kama Mwanaume umeshapitia mazingira fulani ya kudhalilishwa na mwanamke wake kisa pesa ,either kukataliwa,kusalitiwa au kukanwa mbele ya watu kabisa,inaweza ikawa si mapenzi tu ila kwa namna moja pesa inaweza ikawa imeshawahi kukuletea aibu fulani katika mazingira fulani.
Share nasi ni kwa namna gani fedha imewahi kukuletea fedhea .

Vile vile kwa Wanawake mnaweze kushare nasi namna mvilivyowakana na kuwasaliti watu wenu wasio na pesa au walioshiwa gafla , au ni kwa namna gani fedha ilikufanya utoe utu wako kwa ajili ya kupata kitu kama kazi ,nafasi kazini,cheo na mambo kadha wa kadha.

Experience make a person better.

#share .
Ungeanza wewe mkuu ingependeza zaidi.
 
Kuna wakati nikikumbuka kabla ya hapa "Nadondosha hadi machozi"
Nabaki kumlilia Mungu tu na kumshukuru aliponitoa.

Kila aliyenishika mkono wakati wa magumu yangu, ndiye anayefaidi pesa yangu.

Ila kama ulikuwa mgumu kunisaidia zamani; basi hata kama ni ndugu nakusaidia ili ujifunze kuheshimu kila mtu.

Sitaki hata kuyaelezea yaliyonikuta mimi.

Ilifikia hatua najuta kupoteza muda wangu masomoni! Nikicheki nashindwa maisha na niliowaacha kitaa! Dah!

Only God knows.
 
Back
Top Bottom