Wiki ya AZAKI: Mabunge yetu hayajui kitu kuhusu Ulinzi wa Data

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,001
12,351
Bodi member wa JamiiForums atashiriki mjadala wa Tech, Democracy & Decolonization: Interplay and Impact ambao unafanyika katika wiki ya Azaki, AICC Arusha.

Wazungumzaji wengine ni Deogratias Bwire, Harold Sungusia (Rais wa TLS), Andrew Karamagi (MSCTDC), Aikande Clement Kwayu (Board Member JF).

Endelea kuwa nasi kujua yanayoendelea katika mjadala huu.

Sungusia.jpg

Harold Sungusia - Rais Tanganyika Law Society

Ukoloni
Akitoa ufafanuzi wa ukoloni, Sungusia amesema ukoloni ni hali ambayo taifa lenye nguvu linaitawala nchi nyingine. Tukienda kimsingi; ukoloni ni ile hali ya haki ya mmoja kutoweka, yaani kupoteza uhuru na haki.

Sasa tukiweka demokrasia, maana yake ni kuwa na utawala wa watu. Sasa tunapotumia teknolojia kuifanya demokrasia kuondoa ukoloni, tunaangalia namna ambayo watu wanatumia teknolojia.

Sisi tulianza na mkoloni wa kwanza ambaye alikuwa Mreno, ambapo alipokuja Mwarabu na kumuondoa Mreno, Mwarabu akaitwa Mkoloni, ambapo kwa Zanzibar alikuwa Mwarabu na Bara alikuwa Mjerumani. Alipoondolewa Mjerumani tukabaki na Muingereza ambaye athari yake tuko nayo hadi sasa.

Tukisoma kwenye vitabu utaona mkoloni mmoja anaondoka anatuachia mkoloni mwingine. Hata mwaka 1961 tulipewa uhuru wa bendera hadi mwaka 1962 ambapo sasa tulitangaza Katiba na kuwa Jamhuri, hapo tukawa na ukoloni mwingine unaitwa 'Imperial Presidence' ambapo madaraka ya mkoloni yalihamia kwa Rais.

Katiba ilitangaza Rais ana madaraka yote na hawajibiki kufuata ushauri wa baraza la mawaziri. Hivyo tuliondoa utawala wa Mwingereza tukaleta Utawala wa Rais.

Tunapozungumzia kuondoa ukoloni hatuzungumziii kuondoa mtawala wa nje bali kuondoa uonevu wa mwananchi.

Nchi nyingi zinatunga sheria kubana mzunguko wa taarifa ambao ndio msingi wa demokrasia.

Screenshot 2023-10-27 154434.png

Andrew Karamagi - MSCTDC

Ukoloni wa Kimtandao

Ningeanza kujibu kwa kuwataka mfikirie humu mlipo ni kipande cha ardhi ambacho hakuna hata mmoja anayekimiliki ila inabidi tuishi.

Mnakumbuka 'Feudalism', ambapo mmoja anamiliki ardhi na wengine wanafanyakazi kwa mwenye ardhi ili kuishi? Nitatumia mfano huu kuelezea ukoloni wa kiteknolojia (Techno-Feudalism).

Tuna makampuni yanayoitwa Big Five, ambapo ni pamoja na Google, pia wapo Meta, Amazon, Apple na Microsoft, kampuni hizi zikikuzuia kupakua applications zake unajisikiaje? Tunapopakua apps hizi tunakubali kuwapa taarifa nyingi bila hata kusoma.

Mmekuja hapa kwa njia mbalimbali na mmekuta kamera, mmeambiwa kuwa ni kwa usalama wenu lakini hatujui nani anazitunza taarifa hizi.

Kuna taarifa nyingi tumezitoa ili kupata huduma kama ambavyo ipo kwenye mfumo wa Feudalism, na hatujali sana jinsi taarifa hizi zinavyotumika, hatujui zinapoenda.

Matumizi ya vitu vya ofisi vya google ni makubwa kuliko GDP ya nchi nyingi. Sasa nchi kama Uganda inaweza kutengeneza sheria ya kuzuia hawa ambao wanatuzidi kipato?

Mimi nasema "Hatutafuti Google, Google ndiye anayetutafuta sisi."

Mabunge yetu hayajui kitu kuhusu Ulinzi wa Data. Mfano Uganda imetawaliwa na mtu tangu hakuna internet mpaka sasa kuna internet na bado yupo akidhani anaweza kupitisha sheria zinazohusu internet.

Survailance capitalism; Haya makampuni makubwa yaliyotufanya bidhaa. Unapoenda kununua bidhaa unadhani kile unachonunua ni bidhaa lakini wewe ni ndio bidhaa. Wengi mnadhani Facebook ni bure, si kweli, wewe ni bidhaa.

Namaliza kwa kusema CSO tufikirie jinsi ya kufanya ili kuhakikisha mazingira ya kimtandao yanawafikia wote, lakini tuige mifano mizuri kama Korea na Asia Tigers. Leo Korea ni nchi ya kidemokrasia kwa kuwa imejitoa katika ukoloni wa kitechnolojia.

Screenshot 2023-10-27 154546.png

Aikande Kwayu - Board Member JF

Demokrasia ni utawala wa watu. Kuna watu wanadhani demokrasia ni kitu cha nje, lakini demokrasia ni misingi. Misingi kama uhuru, ujumuishi, haki, na ushiriki. Hivi vyote vinabidi viwe ndani ya utawala wa sheria.

Tukija kwenye decolonization (kuondoa ukoloni) ni mchakato endelevu. Decolonisation ni kumsaidia mwanadamu kujitambua ili kujisimamia mwenyewe.

Hata baada ya uhuru tumeingia kwenye aina fulani ya ukoloni. Ukiangalia kwa ndani kinachofanywa na CSO ni decolonization kwa ngazi zote.

Swali la kujiuliza; ni kwa namna gani tumeweza kufanya kazi kwa vizuri? Je, watu wa chini tumeweza kuwashushia ajenda ya kujitawala (decolonization) ili iwe lugha yao? Sisi sasa kama CSO tumekuwa mawakala wa ukoloni au uhuru wa kujitawala?

Tumetumiaje tecknolojia kufanya decolonization?

20231026_151105.jpg


Michango na Maswali ya wazungumzaji wengine

Abella Bateyunga (TBI): Naomba tujadili ni kwa namna gani tunaondoa Ukoloni katika fedha tunazopokea kama Asasi za Kiraia (AZAKI) kwa sababu tunapokea pesa hizi na nyingine zinakuja na vipaumbele vilivyopangwa kabisa. Tunawezaje kuzipokea lakini tukabaki na Uhuru na Haki zetu?

Alais Morindat (Muanzilishi wa FCS): Decolonization inabidi ianze na kudecolonize mind. Sisi (Wamasai) tumekataa vitu vingi, kuanzia mavazi hadi kwenye damu, lakini tunakatiliwa katika ulimwengu kwa sababu hiyo. Tunakaa hapa wiki nzima kujadili mambo haya lakini ni kwa sababu elimu tuliyopewa imetuingiza katika ukoloni.

Majibu

Sungusisa;

Matatizo yetu yanaenda na utambulisho wetu. Sisi ni kina nani? Tusipojitambua ni rahisi mtu kuua tamaduni zetu na kubaki na tamaduni za nje. Kama hapa naongea Kiingereza wakati najua Kiswahili, hii ni ukandamizani na uuaji tamaduni (cultural genocide na suicide) na tunzifanya kwa wakati mmoja. Hiki kitu kinafanya udhani tamaduni ya mwingine ni bora kuliko yako.

Kuna 'Cultural genocide' inayotokea ukiwa hujui wewe ni nani. Hapa Utu wako utadhalilishwa tu lakini pia, unaweza kufanya 'Cultural suicide'; inayotokana na kuthamini maadili/tamaduni za wengine kuliko zetu wenyewe.

Kuna kitu kinaitwa 'Stockholm Syndrome', hapa ni pale ambapo Mtekaji na Mtekwaji wanapendana; yaani yule Mtekwaji anajikuta anampenda aliyemteka mpaka kuimba nyimbo zake. Wakati wa Uchaguzi tunashuhudia hili, Kiongozi tangu achaguliwe hajarudi kwa Wananchi lakini wakati wa Uchaguzi unakuta anarudi kwao, anawapa khanga nao wanasahau yote yaliyopita.

Mwalimu Nyerere alisema tunatumia tusichokiunda, tunaunda tusichotumia, kwa hiyo tuanze na elimu, nakubaliana naye.

Ili kuondokana na ukoloni, lazima tuanze na kuwa na elimu ya kiukombozi (liberative education). Mfano unakuta mtu ni Profesa, lakini anaenda kwa mganga kuchanjwa chale kabla ya uchaguzi. Yaani anaamini mganga kuliko elimu ya Sayansi ya Siasa aliyoipata. Akiwa katika mazingira tatanishi anadharau hata elimu yake kwa kuishusha chini kabisa kwa kuendana na wakati ule. Mtu kusema ametokea jalalani, unaweza kuwa msomi lakini unafanya vituko kwa kuwa elimu uliyoipata haijakukomboa.

Tupo kwenye njia panda, kuhusu jadi zetu na teknolojia.

Andrew Karamagi;
Kwenye kubadili fikra, sisi sote inabidi tuanze kusoma. Kama CSO unaweza kufanya siku moja iwe ya kusoma na kuwasilisha. Utawaambia watu wako kila siku wasome paper iwe ya Shivji au yeyote na kuipresent.

Wachumi walioko hapa watusaidie kujua namna ya kuwekeza kenye bondi na bili ili kuwa majasiri na thabiti ni lazima tuishi hivyo. Donor wanakuhitaji wewe kuliko wewe unavyowahitaji wao.

Waliopigania uhuru wa Afrika hawakuandika proposals. Kubadilisha Afrika unapaswa kuwa jasiri, hapa hata waliopigania uhuru wakitukuta tunaandika proposals watashangazwa.

Kubadilisha vitu ni lazima kubadili vitu kuanzia chini, hili sio suala la logo yako. Hata manabii hawakubadili vitu kwa kutumia logo.

Aikande Kwayu
Mimi sioni vibaya taasisi kupata fedha kutoka kwa mfadhili (donor), shida ni masharti gani unapewa. Suala hapa ni kusimama kubadili masharti.

Kitu kingine ni ajenda, watu wengi huandika proposal kulingana na ajenda za wanaotoa hela.

Ni muhimu kuwa na critical mass ambapo itatuwezesha kufanya crowdfunding. Wapo baadhi ya watu wanataasisi zinazopata hela kutoka kwa watu. Hii ndio namna ya ukombozi wa kifikra (kudecolonize mind).
 
Back
Top Bottom