Je, Ukosefu wa fedha ulishawahi kukudhalilisha? Share experience yako

Siwezi kusahau siku niliyozabwa kofi la nguvu sana sikioni na mwalimu mkuu wa shule yangu ya msingi mbele ya wanafunzi wote hadi nikaanguka chini huku nikihisi sikio kuziba. Hii ilinitokea nikiwa darasa la nne baada ya kuwa nimekosa hela ya kiingilio cha kuangalia mazingaombwe na mimi nikawa nimerukia dirishani ila bahati mbaya yule mwalimu akawa ameniona. Nilikuwa mdogo lakini hilo tukio lilinifedhehesha muda wote hadi nilipohama shule hiyo nikiwa darasa la sita ndipo nikapata nafuu.
hahaaaa daaaahh " huyo teacher " anastahiki " kutunukiwa nishani ya roho mbaya aisee
 
Yasikie kwa watu. Niliingia na demu Mazembe guest house Tabata karibu sana na mataa kama unakuja Azam tv. Ile nimemaliza kuvaa ngao demu kaniambia nipe changu kwanza. Mfukoni nilikua na buku 2 nauli ya kurudia. Nilimuona abdala kichwa wazi akisinyaaa ndani ya vazi rasmi la kivita. Sikua na lakufanya ila kuvaa suruali na kuwahi daladala la Ubungo.
ha hahaa
mazembe napajua hapo " nyumba ya pili toka mazembe alikuwa anaishi demu wangu " mtoto wa kiustaadhati mmoja matata sana"... nyumba yao ili kuwa na madrasa ".... daaahh maisha yanavituko haya
 
Mimi napitia hali hiyo mnayosimulia kwa sasa lakin ukiniona niko na furaha sana, majaribu nimeyachukulia positive. Mungu ananiandaa kwa ajil ya mambo makubwa....... Simu nikipiga hazipokelewi hata kwa ndugu wa karibu saa nyingine, wanahis nitakuwa naomba misaada tu
pole sana aisee "... huu msemo wa kutesa kwa zamu " haujawahi kataa ku-exist ..wakati wako ukifika hao nduguzo wajiandae kunywa panadol
 
"Yule naye si marehemu tu!atanipa nini mimi?
Haya maneno nikiyakumbuka roho inaniuma sana,but my wife ndio mwanamke pekee ambaye alinipenda tangu nakula msosi wa kengere hadi leo nina maisha yangu ambayo sifikirii ntakula nini.Lakini ndiyo mitihani ya maisha kwakuwa ni binadamu
muheshimu sana mkeo "... kuna watu huwa mnabahati ya kupata wanawake aisee
 
hahaaaa daaaahh " huyo teacher " anastahiki " kutunukiwa nishani ya roho mbaya aisee
Halafu mbaya zaidi kwa vile wanafunzi wengi hawakuwa na pesa ya kiingilio na ni wachache sana waliweza kulipa ikamlazimu profesa wa mazingaombwe ahairishe onyesho lake kwa kudai kwamba haitamlipa. Yaani hiyo ndiyo iliyoniumiza zaidi kuona kwamba "aliyefaidi" mazingaombwe ya siku hiyo ni mimi pekee yangu kwa kuzabwa lile kofi adimu.
 
muheshimu sana mkeo "... kuna watu huwa mnabahati ya kupata wanawake aisee
Kaka yaani natamani sana kuoa mke wa pili au kuwa na mchepuko lakini nikikumbuka nilivyoanza na mke wangu uhusiano mpaka leo nakuwa mpole,ndio maana kigezo changu cha mke wa pili lazima awe na kazi,biashara na mwenye uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 70 lakini sio eti yeye anifanye mimi kazi kwakutegemea papuchi yake tu.Mimi na mke wangu tuna miaka kumi ya uhusiano yaani sita ya uchumba na minne ya ndoa na katika miaka sita ya uchumba gharama yangu kubwa ilikuwa kununua vocha na kumpigia lakini zile story sijui simu yangu imeingia kwenye maji wala sikukutana nayo
 
Hili tukio ni la juzi kati tu (mpaka sasa sina hela).
Ninataka kuingia na na dem gest mfukoni nina elf 15 tu picha linaanza dem anataka kula nikimuuliza anataka nini akasema chips yai..

Basi hapo hapo guest kuna kisehemu wanauza chips tukaenda kupata chips..
Akaagiza chips na soda na mimi nikaagiza hivyo hivyo.

Baada ya kula nikatoa elf 10 nikarudishiwa elf 4...ikabidi nimuulize jamaa imekuwaje wananipa buku 4 badala ya buku 5... akasema soda ni buku 1...

Hapo mnyawezi plani zangu zikawa zimeyumba maana mfukoni nikabaki na elf 9 wakati kiingilio cha guest ni elf 10..

Ikabidi niingie hivyo hivyo tu lakini akilini niko napanga mbinu zangu za kivita za kuingia gest kwa elf 9..

pale kaunta nikawaambia wanionyeshe chumba kwanza ndio nilipe waliponinyesha chumba nikamwambia yule dem aingie kwanza room mimi nikamalizie malipo counter fastaa. Dem kaingia chumbani mimi na muhudumu tukarudi kaunta kumaliza malipo tulipofika nikatoa buku 9 niliyokuwa nayo ...muhudumu akagoma..nimembembeleza hadi kidogo nipige magoti hadi akakubali..

Nikarudi room nikamkuta yule dem yupo katulia tu ile nataka kuanza mambo yangu ya kuvunja ile amri pendwa no 6. Manzi anaanza kugoma goma..nikajua hii ni danganya toto tu ...
Lakini huwezi amini hadi naondoka mule mzigo SIKUPATA anasema alikua yuko MP...

Mfukoni nilikua sina hata 100 ya nauli na hapo yule dem ananiomba nauli..

Nilimchenjia fastaa nikamwambia kama vipi tuachane tu (hapo ilikua ni defence mechanism maana sina hela ya nauli aliyoniomba) nikaondoka kwa hasira.

Balaa likaanza la kurudi gheto kwa miguu nimetembea kuanzia saa 11 jioni hadi saa 3 usiku ndo nafika home nimechoka nakuta home maji hakuna nikalala njaa (nilishindia chips ile niliokula mchana)



MJINI USIOMBE UKAWA HUNA PESA UTAPATA TABU
 
Siwezi kusahau siku niliyozabwa kofi la nguvu sana sikioni na mwalimu mkuu wa shule yangu ya msingi mbele ya wanafunzi wote hadi nikaanguka chini huku nikihisi sikio kuziba. Hii ilinitokea nikiwa darasa la nne baada ya kuwa nimekosa hela ya kiingilio cha kuangalia mazingaombwe na mimi nikawa nimerukia dirishani ila bahati mbaya yule mwalimu akawa ameniona. Nilikuwa mdogo lakini hilo tukio lilinifedhehesha muda wote hadi nilipohama shule hiyo nikiwa darasa la sita ndipo nikapata nafuu.
Hahaha sasa Mazingaumbwe ukose ww ...mwalimu akupige ..ila shule za msingi zilikua na uonevu sana
 
Back
Top Bottom