Je, ukimaliza Diploma, unaweza kupata mkopo kwa ngazi ya Degree?

Ivan Breaker

JF-Expert Member
Jun 13, 2020
1,379
5,488
Kama form four ulisomea shule ya serikali na ukafaulu vizuri ukaingia chuo, ukamaliza kusoma diploma kwa miaka mitatu na ukataka uendelee na degree. Unaweza kupata mkopo kutoka serikalini huko utakapofika kwenye ngazi ya degree?
 
Sana tu.

usiwaze mkuu..sema uombaji wake uko tofauti kidogo na walohitimu Advance, wewe utatakiwa uwe na transcript, kama huna hata progressive ya semista 3, na vigezo vilivyobakia ni kama vya walosoma advanced level. Kumbuka pia ktk kuomba vyuo iko tofauti.

Wenye diploma ni lazima upate award verification number (avn) kutoka NACTE, ili kuweza kukuruhusu uombe chuo chochote unachotaka, hii hutolewa baada ya matokeo yako kutoka na chuo wakipeleka matokeo yenu NACTE ndo unaipata, unajisajili then walipia kama 20,000 unaendlea na utaratibu wa kuomba vyuo.

Kila la kheri mkuu.
 
Sana tu.

usiwaze mkuu..sema uombaji wake uko tofauti kidogo na walohitimu Advance, wewe utatakiwa uwe na transcript, kama huna hata progressive ya semista 3, na vigezo vilivyobakia ni kama vya walosoma advanced level. Kumbuka pia ktk kuomba vyuo iko tofauti..
Hv ni 20,000 au 10,000?
 
Kama form four ulisomea shule ya serikali na ukafaulu vizuri ukaingia chuo, ukamaliza kusoma diploma kwa miaka mitatu na ukataka uendelee na degree. Unaweza kupata mkopo kutoka serikalini huko utakapofika kwenye ngazi ya degree?
Tatizo muda umeisha labda heslb wafungue tena hv karibuni..
Kama wakifungua omba
 
mwaka jana ilikuwa 10,000.
mwaka huu 20,000 kwa intake ya march. sasa
sjajua kwa wale ambao wamemaliz dip mwez wa 8 kuwa watashusha au itkuwaje....bt maximum 20,000
Kwani kuna watu wanaingia vyuo vikuu intake ya march..?
Na vp wewe umepata hyo AVN na kama umepata umelilipia sh ngapi..?
 
Wenye diploma ni lazima upate award verification number (avn) kutoka NACTE, ili kuweza kukuruhusu uombe chuo chochote unachotaka, hii hutolewa baada ya matokeo yako kutoka na chuo wakipeleka matokeo yenu NACTE ndo unaipata, unajisajili then walipia kama 20,000 unaendlea na utaratibu wa kuomba vyuo
Nafikiri tatizo kubwa nikupata AVN kama unataka uunganishe Dip kwenda degree moja kwa moja. Ukichelewa kupata AVN, application yako ya mkopo nayo huchelewa na utakuta HESLB wameshatoa batch kubwa ya kwanza, inayofuatia ni shida.

Halafu unakuta vyuo vingine field ya diploma course inafanyika wakati watu ndio wana omba vyuo hivyo automatically inakula kwako kwani majibu ya field yakitoka admission cycle ndio inakata.
 
Kama form four ulisomea shule ya serikali na ukafaulu vizuri ukaingia chuo, ukamaliza kusoma diploma kwa miaka mitatu na ukataka uendelee na degree. Unaweza kupata mkopo kutoka serikalini huko utakapofika kwenye ngazi ya degree?
Ndio unaweza kupata ,usiwe na ofu just tuma maombi yako kwa usahihi
 
Matokeo ya Diploma kwetu bado, Tumemaliza UE tarehe 8 September, nadhani wiki hii kuanzia kesho au kesho kutwa yatakuwa tayari, nitasubiri kuomba chuo dirisha la pili kama watafungua
watafungua....nadhani kwenye tarehe 12 mwezi wa 10..dirisha litagunguliwa tena..
 
Back
Top Bottom