Ushauri: Nataka kuacha kusoma Bachelor Degree in Computer Science nikasome Diploma in Diagnostic Radiography

Darwin james

Member
Oct 18, 2023
20
12
Habari zenu wakuu,

Naitwa Jason kwa sasa nasoma Chuo Cha uhasibu Arusha (IAA), kozi ni Bachelor Degree in Computer Science naingia sasa mwaka wa pili lakini nina dukuduku nyumbani wanasema hii kozi nitahangaika huko mbeleni kupata kazi ya maslahi ni bora ningekua nasoma Afya kungeweza kuwa na afadhali, lakini Sasa nimeshasoma mwaka mmoja.

Kuna wazo limeniijia kichwani kwamba niachane nayo alafu nikasome Diploma kozi ya Afya (Diagnostic Radiography).

Naombeni ushauri wakuu lipi wazo Bora kuendelea nayo au nikasome hyo Diploma ya kozi ya Afya.

Ahsanteni 🙏🙏🙏
 
Kuna mdogo wangu alichaguliwa SUA akakataa kwenda na kuamua kusomea ualimu kwa kudhani atapata ajira kirahisi. Hadi leo yupo home
Dooo mambo yanaumiza sana haya, me naamini kwenye jitihada tu asee, kila mhali kuna fursa sisi tu ndo hatuonagi tunawaza kuwa waajiriwa sjui tumeumbwaje watanzania. Au ndo tumechukua urithi wa akili kwa chief mangungo wa Msovero na mangi sina wa kibosho uko
 
Kwan mkuu ww mpka unaanza kujadili kuanz kuhama cjuh. Ni kwamb ww hunaga malengo Yan?
 
Broadly speaking haupo sahihi kufuata maelekezo ya watu wa nyumbani. Swali kuu ni je unaipenda kozi ya kompyuta science au hiyo kozi yako wanayotaka wa nyumbani kwenu ukasome. Inaonekana kama bado hujui namna ya kufanya maamuzi.

Mimi ningekuwa nasoma sasa hivi basi katika kozi ambazo ningesoma ni kama ifuatavyo ya kwanza Computer Science, ya pili Law na ya tatu Business Administration.
 
Halafu inakuwaje mtu umesoma Computer science halafu unakosa kazi? Mbona kazi ni nyingi sana nje na kuajiriwa? Hasa kama umesoma masuala ya web development mbona unaweza kujiajiri tu.
 
A

Broadly speaking haupo sahihi kufuata maelekezo ya watu wa nyumbani. Swali kuu ni je unaipenda kozi ya kompyuta science au hiyo kozi yako wanayotaka wa nyumbani kwenu ukasome. Inaonekana kama bado hujui namna ya kufanya maamuzi.
Mimi ningekuwa nasoma sasa hivi basi katika kozi ambazo ningesoma ni kama ifuatavyo ya kwanza Computer Science, ya pili Law na ya tatu Business Administration.
Law inakushawishi nn mkuu
 
Back
Top Bottom