Je uchawi una harufu? Unanuka au unanukia?

Je uchawi una harufu? Unanuka au unanukia?

Naweka mjadala huu kwa niaba ya mdau wangu aliyeniomba ufafanuzi juu ya hili na akapenda niwashirikishe nanyi...

Je uchawi una harufu gani?
Unanuka?
Unanukia?
Kama unanuka ni harufu ya nini?
Kama unanukia....! Unanukiaje?

Uchawi kwa maana nzima ya dhana ya ulozi ushirikina na shirki... Haunuki, haunukii wala hauna harufu yoyote.. Uchawi ni nguvu roho.. Huwezi kuuona, kuushika, kuusikia wala kuunusa.... Sanasana unaweza kuhisi nguvu yake hasa pale unapofikia mahali ambako pametekwa na hiyo nguvu... Utahisi hali tofauti, mapigo ya moyo kuongezeka, nywele kusimama na mwili kusisimka! Hakuna harufu.....

Kinachonuka ama kunukia ninini sasa?
Kinachonuka ama kunukia ni vitendea kazi!
Kama ni vitu vinavyotokana na binadamu mfano nywele kucha nguo ngozi mate au haja kubwa na ndogo!

Kinachonuka ama kunukia ni mitishamba, mapembe makombe na zanakazi nyingine za kishirikina....

Uchawi kama uchawi hauna harufu kabisa... Ni jambo la kiroho ambayo matokeo yake ndio ithibati pekee tena kwa wale waamini tuu...

Ukiona mtu ananukia sana hizi ni ishu za majini... A ukipita sehemu ukakuta pana harufu nzuri sana... Fahamu kwamba hilo eneo majini wapi tena wale wapendanao harufu nzuri hasa udi na uturi wa harufu kali na mavumba ya kuvukiza...

Ukikutana na ushirikina huku ananukia sana basi huyo ni mojawapo wa wale wajanja wajanja wanaojaribu kufanya kolabo isiyomatch ya vitu viwili tofauti....

kuna mzungu alijamba kwenye ndege ili bidi tushuke emergency land tukajikuta tumepangiwa juliasi nyerere.na kijiuliza kwa nini wametupangia hapo
 
kuna mzungu alijamba kwenye ndege ili bidi tushuke emergency land tukajikuta tumepangiwa juliasi nyerere.na kijiuliza kwa nini wametupangia hapo
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Uchawi uliumbwa pamoja na dunia lakini kwenye ulimwengu wa roho.. Na ni sehemu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu mwenyewe
Uchawi ama wachawi upo wa kila aina kutoka kwa binadamu mpaka wanyama... Kutoka milimani mapangoni misituni angani ardhini mpaka majini
hivyo chimbuko la uchawi ni kutoka kwa Mungu au shetani??? au kotekote??
 
Uchawi uliumbwa pamoja na dunia lakini kwenye ulimwengu wa roho.. Na ni sehemu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu mwenyewe
Uchawi ama wachawi upo wa kila aina kutoka kwa binadamu mpaka wanyama... Kutoka milimani mapangoni misituni angani ardhini mpaka majini
Ahsante.
 
Nilishawahi kuulizwa hili swali ni nini kinachofanya mtu asisimke wakati wa kitu cha hatari au akiwa amefika sehemu ya hatari nikashindwa kumuelezea alieniuliza hilo swali maana nilikuwa njee ya uwezo nalo japo halikuwa la msingi kwenye hiyo mada niliyokuwa namuelezea je kaka mshana utaweza nitasaidia ili niongeze japo maarifa juu ya hicho kitendo cha nywele na mwili kusisimkaa?
biology form three kunamajibu sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi ni sayansi na uchawi sio kitu kibaya, ila tu mtu anapoamua kuutumia vibaya kama kuua watu, na kutoa kafara. But uchawi upo recognized na ni legal issues, kuna vyuo vinafundisha uchawi kwa level ya degree hadi phd, kimoja kipo south africa

Sahihi kabisa

Jr[emoji769]
 
Naomba msaada wako mkuu mshana, wife alipata tatizo flani hivi lile tatizo lilitusumbua sana bila kupata muahafaka, akaitwa na mama yake cha ajabu kaja na kibangili cha shaba anadai amepewa na mama yake na ameambiwa asiweke chini hiyo bangili, mbaya zaidi Akasema ameambiwa ampe mtoto wake wa mwisho,, naomba kufahamu huo ndo uchawi wenyewe au? Naomba jibu tafadhali bro.
 
Mmh nipe muda
 
Anty yangu Aliniambia ukilima shamba bila kuweka ulinz Msimu wa mavuno unavuniwaa
 
Back
Top Bottom